Jikumbushe Haya 9 Wakati Unaishi Na Mwanamke, Ili Uishi Kwa Amani.

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Kuishi na mwanamke inapaswa iwe raha.
Ukiona huna raha kuishi naye, tambua kuna sehemu umeyumba.
Kosa kubwa wengi hufanya ni kuishi na mwanamke anayemtesa sababu anaogopa kumuacha. Anaogopa kuanza upya kutafuta mwanamke mwingine.
Anaona aishi na huyo hivyo hivyo tu, maisha yasonge.
Lakini tambua amani yako ni muhimu.
Ukiwa na amani, utaijenga jamii kirahisi na utatimiza malengo yako kirahisi.
Sasa ili kuitunza amani yako jikumbushe haya wakati wa kuishi na mwanamke.
.
Wewe ndio kiongozi.
Wewe ndo unamaamuzi mahusiano yaendaje.
Wewe ndo unamaamuzi mfanye nini wakati fulani.
Wewe ndo unamaamuzi ya kumfanya astawi.
Wewe ndo unamaamuzi ya kumfanya akupende zaidi na zaidi.
Ukimuachia maamuzi mwanamke atakuchukia. Ukiona anakuendesha ujue umemuachia uongozi yeye.
Usikae kumuuliza mwanamke twende wapi, tufanye nini, apendezeje, mle nini leo usiku, au mfanye staili gani. We tangulia yeye atafata.

Kama mwanamke mmoja hataki kuwa chini ya uongozi wako, piga moyo konde tafuta aliye tayari.
.
Wanategemea hisia kufanya maamuzi.
Ndio maana hawatabiriki.
Na huwezi ukamsimamia kwa kile alichokisema jana. Kama mwanaume. Mwanaume ukisema kitu inabidi ndo kiwe ichoicho.
Anaweza kuwa na mudi mzuri na mkakubaliana kitu lakini baadae mkazozana, mudi imebadilika.
Ilo lisikupe mawazo. Mwache, mudi itabadilika tu na mtaongea vizuri.
Usije ukaendeshwa na mudi zake.
Pia wanakutegemea wewe kihisia kwenye kufanya maamuzi kwa ajili yao.
Wao wenyewe wanajijua.
.
Jali malengo yako.
Mwanamke awe msindikizaji/ mpambe kwenye maisha yako.
Wanawake wengi wapo tayari kuwa upande wako wakati unajenga maisha yako. Usihangaike na anayetaka kuharibu maisha yako.
Mwanamke asiwe kipaumbele chako.
Ukimuweka namba moja, atakuacha haraka.
Namba moja ni malengo yako.
.
Usijaribu kumlazimisha kufikiria kama unavyofikiria.
Usijaribu kumlazimisha kutatua matatizo kama wewe.
Usijaribu kumlazimisha;
Akupende kama umpendavyo, au
Aone umuhimu wako kama unavyojiona una umuhimu kwake, au
Kumlazimisha kila ukimpigia lazima apokee/ ajibu sms.
Ukimlazimisha vitu atakuacha.
Kulazimisha ni tofauti na kuongoza na kuweka misimamo.
Pia usibishane na mwanamke.
.
Jifunze kupotezea visivyo na msingi.
Sio lazima kila akuambiacho mwanamke ufanye maamuzi.
Kuna vingine anavisema tu sababu anapenda kuongea.
Kuna vingine anafanya ili umuone tu.
Kuna vingine anafanya ili akupime kama we ni jasiri.
Kama mwanaume umebeba jukumu la kuongoza mahusiano.
Vitu visivyo na msingi achana navyo usije ukapoteza mwelekeo wa mahusiano.
.
Simamia mipaka uliyomwekea.
Usikubali aivunje mipaka yako hata kidogo.
Anaweza akaivunja alafu akakuambia ni utani. Lakini anakupima tu kama kweli utasimamia mipaka yako au la.
Usipomwekea mwanamke mipaka atakushusha thamani.
.
Sio kila muda unahitaji kufanya kitu.
Sio kila muda ufanye kitu ili akupende.
Kuna ule msemo kufanya kitu ni bora kuliko kukaa tu.
Ukweli ni kwamba sio kila muda/ kila kitu kinahitaji vitendo vyako. Vingine acha vikue vyenyewe.

Mfano, unakutana na mwanamke (upo naye) mkaongea vizuri na mkapanga muda wa kukutana. Lakini unahisi hiyo haitoshi, unaanza kuwaza
‘atanisahau nimchombeze zaidi ili anikumbuke’/
‘anaonekana kunikubali, acha niongee naye zaidi ili anipende zaidi’/
‘ngoja niongee naye ili nimshawishi zaidi’/
‘ngoja niongee naye zaidi wajanja wasije wakamchukua’.
Utaongea naye masaa kwa masaa, utajiona unahsinda lakini haukusaidii yeye kukukubali zaidi.
Atakuona huna changamoto kwake mana ni mrahisi. Ikifika muda wa kukutana, atakupa sababu nzuri ili msikutane huo muda.

Pia umemzoesha kuongea nawe kwenye simu badala ya kukutana.
Unachotakiwa kufanya, kama umeshapanga muda, siku na sehemu we tulia subiri huo muda mliokubaliana.
.
Misukosuko inachochea upendo.
Misuko suko inasababisha hisia tofauti.
Kadri unavyompa mwanamke hisia nyingi, ndivyo anazidi kukupenda.
Usije ukajifunga kwamba, inabidi umpe hisia za upendo tu kila siku ili akupende. Hapana. Mpe hisia tofauti mana unajua ye ni mtu wa hisia sana.

Pia mwache mwanamke apitie hisia bila kumlazimisha kitu.
Atakupotezea leo, kesho ataonesha kukupenda, kesho kutwa atakua haeleweki.
We baki kama mwamba imara usioyumbishwa.
We baki na ujasiri na kujiamini kuwa unampatia kitu kizuri.

Hata muvi unayoipenda ina misukosuko tofauti, na unapata hisia tofauti ndo mana unaipenda.
.
Anataka afurahi kwako.
Sawa misukosuko ya kihisia ipo lakini anataka kufurahi kwako.
Haina maana ya kipesa tu.
Kwamba umfurahishe kwa kumvesha, kumlisha na kumtunza. Bali mfurahishe kihisia pia.
Mfanye ache, asahau shida zake akiwa nawe, ajisikie kujiachia kwako na mpe mapenzi moto moto kitandani.
Usiwe kama mtoto kwake au kumtegemea mwanamke ili ujisikie raha.
Usimlilie mwanamke shida zako mara kwa mara.

Ila utapata urahisi ukielewa chanzo cha kwanini amefanya kitu fulani. Utaelewa kwa kuangalia vitendo vyake zaidi ya maneno yake. Wanawake wanalugha ya kuficha ficha, ni wewe kutambua kilichomsukuma kufanya kitu fulani. Lakini kama huyo mwanamke unaona haupati amani ukiwa naye, heri utafute mwingine amani utapata amani kuishi naye.

Nikutakie Weekend Njema, Maandalizi Mema Ya Wiki Ijayo.

Na Sikukuu Njema Pia Yenye Amani.
 
Afadhali sasa wanaume wana madarasa yao, hapo awali ilikuwa ni kitchen parts tu na kufundana.
Ahsante mitandao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom