Mwanamke uliyeolewa, usifanye makosa haya

MLIMAWANYOKA

JF-Expert Member
Oct 25, 2019
487
1,633
Na. John- Baptist Ngatunga
___________________________

Kwa kawaida, kila binadamu anayafanya makosa. Lakini yapo makosa mengine ambayo pamoja na ubinadamu wetu hatupaswi kuyafanya. Tunatakiwa kuwa makini sana kuyaepuka ili tusikutwe na lawama. Ndivyo ilivyo pia kwa Mwanamke aliyeolewa kujiepusha sana na makosa yafuata:

1. KUOMBA HELA KWA MWANAUME MWINGINE
Kuna baadhi ya Wanawake wamekuwa la hulka ya kupenda kuombaomba Pesa kwa Wanaume tofauti na Waume zao. Akilini mwao wanaamini kuwa Mwanaume anaweza akawasaidia tu kama Msaada. Hii inatokana na Ukweli kwamba wengi wa Wanawake hao hawajui madhara yanayoweza kutokea kutokana na tabia hii.

Baadhi ya madhara yatokanayo na kufanya hivo ni haya yafuatayo:

Kwanza; unaiharibu sifa, utu na heshima ya Mume wako kwa kumdhalilisha kwamba ni Masikini asiyekuwa na uwezo wa kukuhudumia wewe na kukidhi au kukutimizia mahitaji yako. Kwa kufanya hivyo ni sawa sawa pia na kumtangaza Mume wako kwa Wanaume wengine kwamba yeye ni Dhaifu na hivyo umewasaidia Wanaume wengine kuyajua madhaifu ya Mume wako ya kushindwa kukuhudumia wewe.

Pili; unamdhalilisha Mumeo kwa kuoa Mwanamke 'Ombaomba' na automatically umejidhalilisha pia wewe Mwenyewe kwasababu huyu Ombaomba ninayemzungumzia hapa ni wewe Mwenyewe.

Tatu; Asilimia zaidi ya Sitini (60%+) ya Wanaume, hawawezi kumsaidia Mwanamke bila kutegemea kupata kitu kutoka kwao. Kumbuka huyo Mwanaume unayemwomba Pesa sio Ndugu yako. Ni Mwanaume tu ambaye hana kizuizi chochote cha kidamu kitakachoweza kumzuia pindi na yeye atakapoamua kukuomba Mwili wako.

Ni lazima tu na yeye atahitaji 'Marejesho' ya Mwili wako kwa Hela anazokupa. Wanaume ni wazuri sana katika Masuala ya biashara ya win win situation (yaani sote tunufaike).

Nne; utakuwa umewaambia Wanaume hao kwamba Mume wako anatakiwa asaidiwe Majukumu yake ya kukuhudumia wewe kwasababu hayajui ipasavyo Majukumu yake na wajibu wake kwako au ameshindwa kuyatimiza Mahitaji yako.

Na kitendo cha Wanaume au Mwanaume huyo mwingine kukupatia hela, kinafungua Rasmi ukurasa wa Mume wako kusaidiwa majukumu yake na Wanaume wenzie. Na akisaidiwa Majukumu ya Mahitaji yako ya kawaida, automatically anatakiwa asaidiwe pia na Majukumu ya kukutimizia Mahitaji yako ya kihisia.

Hii yote ni kwasababu haiwezekani "Ng'ombe alishwe na John, maziwa akamue Abdul". Hayo yote utakuwa umeyasema wewe kwa matendo yako ya kuwaomba Hela Wanaume hao wengine nje ya Mume wako.

Kama kuna shida yoyote ya Msingi, inayohitaji Msaada wa kifedha nje ya Familia yako, ni Heri Mume wako ndiye aende kuomba au kukopa hizo fedha kwa Wanaume wenzie.

2. KUTOKA 'OUT' NA MWANAUME MWINGINE

Usitoke out na Mwanaume yeyote nje ya Mume wako. Hata kama Mwanaume huyo ni Shemeji yako au Rafiki wa Karibu sana wa Mume wako. Unaweza ukakiona au kukichukulia kuwa ni kitu cha kawaida tu kwamba hamjaenda sehemu ya Faragha na mlikuwa mnaongea tu mambo ya kawaida au mbona ni Shemeji yako na hawezi kukuambia chochote 'kibaya'.

Lakini Mume wako akigundua au akiona ni mwendelezo au na ni Mazoea unatengeneza ya kufanya hivo, anaweza asiipende hiyo Tabia na ukawa unamkwaza na asikuambie kwasababu anaweza akaanza kuwa mdadisi juu yako.

Usitake mpaka siku Mumeo akukaripie au akuoneshe kuwa haipendi hiyo tabia. Ukisubiri mpaka afanye hivo, ni ishara tosha utakuwa umeionesha kwamba huwezi kujiongeza.

Wakati mwingine kitendo hicho kinaweza kikamtengenezea Maswali Mumeo na kutokana na Asili ya Wivu wa kila Mwaume kwa Mwanamke, Mume wako anaweza akaanza kutilia Mashaka ukaribu wenu na kutokana na Mashaka hayo kwako na kwa huyo Shemeji yako, Mumeo anaweza akaanza kukufuatilia kimya kimya bila kukuuliza au kumfuatilia huyo Ndugu yake au Rafiki yake kimya kimya.

Hata kama Mume wako hana 'wivu wa kihivo' epuka sana Mazoea ya kufanya hivo. Wanaume wote kwa Asili yao ni critical na reasoning. Mazoea yanaweza yakatengeneza tabia ambayo baadae ikamfanya Mumeo awe suspicious na akaanza kudevelop tabia ya kukufuatilia na kukuchunguza na vitu vingine ambavyo havikuwa Akili mwake.

Lakini pia, Mitoko Mitoko kama hii imewafikisha Wanandoa wengi sana katika mazingira ambayo hawakuwahi kuwaza kama yangeweza kujitokeza mambo mengine makubwa ambayo hawakuyawaza. Halafu mwishowe lawama anatupiwa Shetani au yanakuja maneno, "Ningejua nisinge......"

Itaendelea.......
 
MWANAMKE ULIYEOLEWA, USIFANYE MAKOSA YAFUATAYO: (2)

Na. John- Baptist Ngatunga
___________________________
Sehemu ya Pili

Sehemu ya kwanza tuliyaona Makosa mawili yaani: Kuomba Hela kwa Mwanaume mwingine na Kutoka 'Out' na Mwanaume mwingine. Sasa tuendelee na Makosa mengine:

3. KUCHAT NA MWANAUME MWINGINE

Kwa kawaida Mahusiano mengi yanaanzia na Chats. Ni kwenye kuchat ndiko watu wengi wanadhani kuna utulivu na Uhuru wa kusema ya Moyoni kwa wepesi zaidi. Hakikisha unajiepusha na mazingira kama haya.

Usimpe nafasi Mwanaume yeyote kujipatia Mazoea ya kukuchatisha bila sababu ya Msingi. Kama anakutumia Message, basi iwe ni message ambayo inahitaji suluhisho au msaada wa haraka na dharura au kukupatia taarifa au kutaka kupata taarifa kwako. Mfano: "Habari za Asubuhi! Naomba nisaidie jambo hili......"

Lakini isiwe ni messages za kutaka kujua vitu vya kawaida ambavyo ni binafsi au vyenye elements za umbea. Mfano: "Mambo! Umeamkaje au umeshindaje? Siku yako imeendaje? Mambo mengine vipi? Nipe stori? Umekula? Mambo yanaendaje?"

Messages au chattings za aina hii zinaonesha wazi kabisa huyu Mwanaume hana cha maana cha kujadiliana na wewe (Mke wa Mtu). Mtu kama huyu unahitaji kujiepusha naye aidha kwa kumwambia Ukweli kuwa hautegemei au kutamani wala kuhitaji siku nyingine akutumie texts za aina hiyo.

Ukiona unamheshimu sana na huhitaji kumwambia au kumblock, ni heri usiwe unazijibu sms zake. Itakuepusha na Mambo mengi ambayo katika Hali ya kawaida haukuwaza kuja kuyafanya. Wengi wameanguka kwa Mazoea ya mambo madogo madogo kama haya ya kumruhusu Mwanaume mwingine akuchatishe.

4. KUTOA NAMBA ZA SIMU KWA MWANAUME

Mwanamke anayejiheshimu na anayemheshimu Mume wake na Ndoa yake kwa ujumla, hawezi kutoa Namba zake za Simu kwa Wanaume wengine huku akijua kabisa kwamba hawana kitu chochote cha kipekee watakachojadiliana na Wanaume hao zaidi ya kujitengenezea mazingira ya kutongozwa.

Maana hawana biashara kwamba wanajadiliana Masuala ya kibiashara, hawana Mahusiano ya Kikazi wala aina yoyote ya Mawasiliano yatakayokuwa na ulazima nje au zaidi ya pale walipokutana.

Kitendo cha kuwapatia Wanaume wengine Namba zako za Simu ni ishara tosha ya kukubali kuwa tayari kuanzisha majadiliano mengine ambayo ni ngumu kidogo kuyatenganisha na majadiliano ya kimapenzi.

Kama atakuomba Namba ya simu kwa lengo muwe Marafiki, basi kama ana shida sana ya Marafiki, mwambie Mumeo naye anataka Marafiki ni Heri awe Rafiki wa Mume wako. Hii ni kwasababu siku zote "Matendo mengi mabaya yalianza na nia Njema"

Epuka kumsogeza Binadamu katika mazingira yatakayoweza kuihatarisha Ndoa yako kwa mambo madogo madogo kama haya halafu ukimbilie kumtupia lawama Shetani. Yapo makosa mengine ni 'dhambi' mbele ya Shetani kumsingizia yeye wakati dalili zote zinaonekana. Kumbuka, "Dudu liumalo, usilipe wala kulisogezea kidole".

5. KUJIPOST POST PICHA AU VIDEO ZAKO MITANDAONI

Unaweza ukawa unaliona ni Jambo la kawaida sana kwa upande wako kubadilisha badilisha picha mara kwa mara kwenye Display Picture (DP) kwenye Mitandao mbalimbali ya Kijamii, kupost post picha na au video zako status za Whatsapp, Stories za FB au sehemu nyingine za Mitandao mbalimbali ya Kijamii.

Lakini Ukweli ni kwamba Kitendo hiki kufanywa na Mwanamke aliyeolewa kinatuma ujumbe usiokuwa wa moja kwa moja (Indirect Message) kwa Mume wake kwamba yeye bado anatafuta na anahitaji attentions za Wanaume wengine. Anapenda Wanaume wengine wamwone.

Attentions hizo kutoka kwa hao Wanaume wengine ni pamoja na kutaka kuonekana, kusifiwa kwa uzuri wako wa sura au maumbile yako, Mavazi yako kwa kupata comments, likes, followers, na reactions zingine.

Ni kweli kwamba ni Asili ya Mwanamke kutafuta attentions directly au indirectly lakini Maswali ya kukuuliza hapa ni je, Mwanamke uliyeolewa, unatafuta attentions za nini tena wakati tayari ulishasitiriwa kwa kuwekwa Ndani?

Unaendeleaje kuiweka bidhaa sokoni na kwenye Matangazo wakati tayari ilishanunuliwa? Unawezaje kuendelea kupiga Kampeni wakati Uchaguzi ulishafanyika? Je, haujaridhika na Mumeo? Au una mpango wa kumsaliti? Unahangaika tena Mitandaoni na mapicha na video ya nini wakati umeshaolewa? Kwanini unapenda kujionesha?

Ukweli usiopingika ni kwamba Mwanamke aliyeolewa na anayeiheshimu na kuijali Ndoa yake, hawezi kuwa ni Mtu wa kujioneshaonesha kwa watu kwa kutafuta attentions za Wanaume wengine Mitandaoni au Mitaani wakati tayari ameshampata Mwaume wake.

Na Ukweli mwingine ni kwamba, kila Mwanaume anayejitambua, anapenda sana kumwona Mke wake anayempenda akijisitiri kwa kutokupenda kujiwekaweka hadharani mara nyingi bila sababu za Msingi. Hapendi sana Mke wake awe ni Mtu wa kujioneshaonesha sana kwa watu japo anaweza asikuambie ila hapendi.
 
_20240228_195236.JPG
 
Lakini cha ajabu utakuta mwanaume anaambiwa ni sawa yeye kufanya hayo na wanawake wengine, ukiuliza ni kwa misingi gani hutapewa jibu la maana zaidi ya kuambiwa usishindane na mwanaume na kuitwa majina ya ajabu ajabu sijui feminist sijui single mother, nonsense!!
 
Dada'angu una hasira sana na wanaume!

Huyo uliyegombana nae kwa sababu amekutaka uishi kadiri ya asili inavyotaka (mke kuwa chini ya mume) huku hutaki kwa sababu unazo sababu zako (kazi nzuri mshahara ect) jitenge nae kidogo utulize akili maana utawehuka.
 
MWANAMKE ULIYEOLEWA, USIFANYE MAKOSA YAFUATAYO: (1)

Na. John- Baptist Ngatunga
___________________________

Kwa kawaida, kila binadamu anayafanya makosa. Lakini yapo makosa mengine ambayo pamoja na ubinadamu wetu hatupaswi kuyafanya. Tunatakiwa kuwa makini sana kuyaepuka ili tusikutwe na lawama. Ndivyo ilivyo pia kwa Mwanamke aliyeolewa kujiepusha sana na makosa yafuata:

1. KUOMBA HELA KWA MWANAUME MWINGINE

Kuna baadhi ya Wanawake wamekuwa la hulka ya kupenda kuombaomba Pesa kwa Wanaume tofauti na Waume zao. Akilini mwao wanaamini kuwa Mwanaume anaweza akawasaidia tu kama Msaada. Hii inatokana na Ukweli kwamba wengi wa Wanawake hao hawajui madhara yanayoweza kutokea kutokana na tabia hii.

Baadhi ya madhara yatokanayo na kufanya hivo ni haya yafuatayo:

Kwanza; unaiharibu sifa, utu na heshima ya Mume wako kwa kumdhalilisha kwamba ni Masikini asiyekuwa na uwezo wa kukuhudumia wewe na kukidhi au kukutimizia mahitaji yako. Kwa kufanya hivyo ni sawa sawa pia na kumtangaza Mume wako kwa Wanaume wengine kwamba yeye ni Dhaifu na hivyo umewasaidia Wanaume wengine kuyajua madhaifu ya Mume wako ya kushindwa kukuhudumia wewe.

Pili; unamdhalilisha Mumeo kwa kuoa Mwanamke 'Ombaomba' na automatically umejidhalilisha pia wewe Mwenyewe kwasababu huyu Ombaomba ninayemzungumzia hapa ni wewe Mwenyewe.

Tatu; Asilimia zaidi ya Sitini (60%+) ya Wanaume, hawawezi kumsaidia Mwanamke bila kutegemea kupata kitu kutoka kwao. Kumbuka huyo Mwanaume unayemwomba Pesa sio Ndugu yako. Ni Mwanaume tu ambaye hana kizuizi chochote cha kidamu kitakachoweza kumzuia pindi na yeye atakapoamua kukuomba Mwili wako.

Ni lazima tu na yeye atahitaji 'Marejesho' ya Mwili wako kwa Hela anazokupa. Wanaume ni wazuri sana katika Masuala ya biashara ya win win situation (yaani sote tunufaike).

Nne; utakuwa umewaambia Wanaume hao kwamba Mume wako anatakiwa asaidiwe Majukumu yake ya kukuhudumia wewe kwasababu hayajui ipasavyo Majukumu yake na wajibu wake kwako au ameshindwa kuyatimiza Mahitaji yako.

Na kitendo cha Wanaume au Mwanaume huyo mwingine kukupatia hela, kinafungua Rasmi ukurasa wa Mume wako kusaidiwa majukumu yake na Wanaume wenzie. Na akisaidiwa Majukumu ya Mahitaji yako ya kawaida, automatically anatakiwa asaidiwe pia na Majukumu ya kukutimizia Mahitaji yako ya kihisia.

Hii yote ni kwasababu haiwezekani "Ng'ombe alishwe na John, maziwa akamue Abdul". Hayo yote utakuwa umeyasema wewe kwa matendo yako ya kuwaomba Hela Wanaume hao wengine nje ya Mume wako.

Kama kuna shida yoyote ya Msingi, inayohitaji Msaada wa kifedha nje ya Familia yako, ni Heri Mume wako ndiye aende kuomba au kukopa hizo fedha kwa Wanaume wenzie.

2. KUTOKA 'OUT' NA MWANAUME MWINGINE

Usitoke out na Mwanaume yeyote nje ya Mume wako. Hata kama Mwanaume huyo ni Shemeji yako au Rafiki wa Karibu sana wa Mume wako. Unaweza ukakiona au kukichukulia kuwa ni kitu cha kawaida tu kwamba hamjaenda sehemu ya Faragha na mlikuwa mnaongea tu mambo ya kawaida au mbona ni Shemeji yako na hawezi kukuambia chochote 'kibaya'.

Lakini Mume wako akigundua au akiona ni mwendelezo au na ni Mazoea unatengeneza ya kufanya hivo, anaweza asiipende hiyo Tabia na ukawa unamkwaza na asikuambie kwasababu anaweza akaanza kuwa mdadisi juu yako.

Usitake mpaka siku Mumeo akukaripie au akuoneshe kuwa haipendi hiyo tabia. Ukisubiri mpaka afanye hivo, ni ishara tosha utakuwa umeionesha kwamba huwezi kujiongeza.

Wakati mwingine kitendo hicho kinaweza kikamtengenezea Maswali Mumeo na kutokana na Asili ya Wivu wa kila Mwaume kwa Mwanamke, Mume wako anaweza akaanza kutilia Mashaka ukaribu wenu na kutokana na Mashaka hayo kwako na kwa huyo Shemeji yako, Mumeo anaweza akaanza kukufuatilia kimya kimya bila kukuuliza au kumfuatilia huyo Ndugu yake au Rafiki yake kimya kimya.

Hata kama Mume wako hana 'wivu wa kihivo' epuka sana Mazoea ya kufanya hivo. Wanaume wote kwa Asili yao ni critical na reasoning. Mazoea yanaweza yakatengeneza tabia ambayo baadae ikamfanya Mumeo awe suspicious na akaanza kudevelop tabia ya kukufuatilia na kukuchunguza na vitu vingine ambavyo havikuwa Akili mwake.

Lakini pia, Mitoko Mitoko kama hii imewafikisha Wanandoa wengi sana katika mazingira ambayo hawakuwahi kuwaza kama yangeweza kujitokeza mambo mengine makubwa ambayo hawakuyawaza. Halafu mwishowe lawama anatupiwa Shetani au yanakuja maneno, "Ningejua nisinge......"

Itaendelea.......

Waambie na mume wa mtu hatakiwi kufanya yapi?

Ama huku ni exemptions kote.
 
MWANAMKE ULIYEOLEWA, USIFANYE MAKOSA YAFUATAYO: (2)

Na. John- Baptist Ngatunga
___________________________
Sehemu ya Pili

Sehemu ya kwanza tuliyaona Makosa mawili yaani: Kuomba Hela kwa Mwanaume mwingine na Kutoka 'Out' na Mwanaume mwingine. Sasa tuendelee na Makosa mengine:

3. KUCHAT NA MWANAUME MWINGINE

Kwa kawaida Mahusiano mengi yanaanzia na Chats. Ni kwenye kuchat ndiko watu wengi wanadhani kuna utulivu na Uhuru wa kusema ya Moyoni kwa wepesi zaidi. Hakikisha unajiepusha na mazingira kama haya.

Usimpe nafasi Mwanaume yeyote kujipatia Mazoea ya kukuchatisha bila sababu ya Msingi. Kama anakutumia Message, basi iwe ni message ambayo inahitaji suluhisho au msaada wa haraka na dharura au kukupatia taarifa au kutaka kupata taarifa kwako. Mfano: "Habari za Asubuhi! Naomba nisaidie jambo hili......"

Lakini isiwe ni messages za kutaka kujua vitu vya kawaida ambavyo ni binafsi au vyenye elements za umbea. Mfano: "Mambo! Umeamkaje au umeshindaje? Siku yako imeendaje? Mambo mengine vipi? Nipe stori? Umekula? Mambo yanaendaje?"

Messages au chattings za aina hii zinaonesha wazi kabisa huyu Mwanaume hana cha maana cha kujadiliana na wewe (Mke wa Mtu). Mtu kama huyu unahitaji kujiepusha naye aidha kwa kumwambia Ukweli kuwa hautegemei au kutamani wala kuhitaji siku nyingine akutumie texts za aina hiyo.

Ukiona unamheshimu sana na huhitaji kumwambia au kumblock, ni heri usiwe unazijibu sms zake. Itakuepusha na Mambo mengi ambayo katika Hali ya kawaida haukuwaza kuja kuyafanya. Wengi wameanguka kwa Mazoea ya mambo madogo madogo kama haya ya kumruhusu Mwanaume mwingine akuchatishe.

4. KUTOA NAMBA ZA SIMU KWA MWANAUME

Mwanamke anayejiheshimu na anayemheshimu Mume wake na Ndoa yake kwa ujumla, hawezi kutoa Namba zake za Simu kwa Wanaume wengine huku akijua kabisa kwamba hawana kitu chochote cha kipekee watakachojadiliana na Wanaume hao zaidi ya kujitengenezea mazingira ya kutongozwa.

Maana hawana biashara kwamba wanajadiliana Masuala ya kibiashara, hawana Mahusiano ya Kikazi wala aina yoyote ya Mawasiliano yatakayokuwa na ulazima nje au zaidi ya pale walipokutana.

Kitendo cha kuwapatia Wanaume wengine Namba zako za Simu ni ishara tosha ya kukubali kuwa tayari kuanzisha majadiliano mengine ambayo ni ngumu kidogo kuyatenganisha na majadiliano ya kimapenzi.

Kama atakuomba Namba ya simu kwa lengo muwe Marafiki, basi kama ana shida sana ya Marafiki, mwambie Mumeo naye anataka Marafiki ni Heri awe Rafiki wa Mume wako. Hii ni kwasababu siku zote "Matendo mengi mabaya yalianza na nia Njema"

Epuka kumsogeza Binadamu katika mazingira yatakayoweza kuihatarisha Ndoa yako kwa mambo madogo madogo kama haya halafu ukimbilie kumtupia lawama Shetani. Yapo makosa mengine ni 'dhambi' mbele ya Shetani kumsingizia yeye wakati dalili zote zinaonekana. Kumbuka, "Dudu liumalo, usilipe wala kulisogezea kidole".

5. KUJIPOST POST PICHA AU VIDEO ZAKO MITANDAONI

Unaweza ukawa unaliona ni Jambo la kawaida sana kwa upande wako kubadilisha badilisha picha mara kwa mara kwenye Display Picture (DP) kwenye Mitandao mbalimbali ya Kijamii, kupost post picha na au video zako status za Whatsapp, Stories za FB au sehemu nyingine za Mitandao mbalimbali ya Kijamii.

Lakini Ukweli ni kwamba Kitendo hiki kufanywa na Mwanamke aliyeolewa kinatuma ujumbe usiokuwa wa moja kwa moja (Indirect Message) kwa Mume wake kwamba yeye bado anatafuta na anahitaji attentions za Wanaume wengine. Anapenda Wanaume wengine wamwone.

Attentions hizo kutoka kwa hao Wanaume wengine ni pamoja na kutaka kuonekana, kusifiwa kwa uzuri wako wa sura au maumbile yako, Mavazi yako kwa kupata comments, likes, followers, na reactions zingine.

Ni kweli kwamba ni Asili ya Mwanamke kutafuta attentions directly au indirectly lakini Maswali ya kukuuliza hapa ni je, Mwanamke uliyeolewa, unatafuta attentions za nini tena wakati tayari ulishasitiriwa kwa kuwekwa Ndani?

Unaendeleaje kuiweka bidhaa sokoni na kwenye Matangazo wakati tayari ilishanunuliwa? Unawezaje kuendelea kupiga Kampeni wakati Uchaguzi ulishafanyika? Je, haujaridhika na Mumeo? Au una mpango wa kumsaliti? Unahangaika tena Mitandaoni na mapicha na video ya nini wakati umeshaolewa? Kwanini unapenda kujionesha?

Ukweli usiopingika ni kwamba Mwanamke aliyeolewa na anayeiheshimu na kuijali Ndoa yake, hawezi kuwa ni Mtu wa kujioneshaonesha kwa watu kwa kutafuta attentions za Wanaume wengine Mitandaoni au Mitaani wakati tayari ameshampata Mwaume wake.

Na Ukweli mwingine ni kwamba, kila Mwanaume anayejitambua, anapenda sana kumwona Mke wake anayempenda akijisitiri kwa kutokupenda kujiwekaweka hadharani mara nyingi bila sababu za Msingi. Hapendi sana Mke wake awe ni Mtu wa kujioneshaonesha sana kwa watu japo anaweza asikuambie ila hapendi.
🤣 🤣 🤣 Je kikombe hiki kinatuhusu tunao selfika pya? (in mafarisayo's voice) Kama ni ndiwo ninywe Pepsi. Aiiiiiikwo
 
Back
Top Bottom