Jiji la Mbeya: Hapa Wabongo tumechemka

Jiji la Mbeya: Hapa Wabongo tumechemka

5urvtrhki
Sasa mbeya ni jiji lile la matope tu nyumba za udongo tu
Hata Dar es Salaam kuna vibanda mbavu za mbwa maeneo kama Vingunguti, Buguruni Kwa Mnyamani, Kiwalani, Kigogo etc.

Huwezi kuihukumu Dar kwa maeneo hayo na vivyo hivyo huwezi kuihukumu Mbeya kwa hizo nyumba za matope.

Nikuwekea hapa nyumba za vitongoji vya pembezoni mwa Nairobi kama kilomita 6 toka town centre huwezi kuamini kama wanaishi binadamu

Screenshot_20250927_211753_Google.jpg
 
Shule mlienda kufanya nini?.
Huwa mnadhani sifa mojawapo ya mahali kuwa jiji ni majengo? Hamfikilii suala la idadi ya watu, pato lake na , maendeleo ya watu wa mahala hapo?.

Hivi hujui huo mkoa una hadhi ya jiji tangu miaka ya nyuma lakini siasa zenu za CCM ndizo zinarudisha nyuma mkoa.

Inawezekana vipi Mkoa nambari 3-5 ktk uchangiaji wa pato la taifa lkn kodi hazirudi kukarabati miundombinu, Central government unajua inakomba kodi kubwa kutoka Mbeya ,lkn hakuna maendeleo yoyote yanayorudi hapo mkoani, si kimiundombinu hakuna linalofanyika

Huo ndio mkoa pekee maendeleo yake yanabebwa na wananchi by 90%, tofauti na hiyo mikoa yenu mnayopewa vipaumbele lkn bado wananchi wenu wananuka umasikini.

Masikini wa Mbeya anauwezo wa kuwa tajiri mikoa ya kanda ya kati, Kusini, pwani yote na takataka za huko visiwani mnakojaza kodi
Hii sentensi ya mwisho sio sahihi. Masikini wa Mbeya akienda Kusini (let's say Lindi au Mtwara) hawi tajiri, kama akiwa na uchumi uleule wa Mbeya
Huko Lindi au Mtwara ndizi tatu buku, parachichi elfu 2 unampeleka mkazi masikini wa Mbeya kufanya nini. Yeye kazoea Mbeya viazi vya jero anashiba ukimpeleka Kusini utamtesa tu na hizo bei.
Ila huko juu upo sahihi
 
Tanzania miji yote ina ujenzi holela tu ila kwenye jiji la Mbeya tumechemka 😂😂😂
Actually sitaki kuonesha picha za ujenzi holela hapa Mbeya lakini ukiingia Google, search tu "Mbeya" halafu nenda kwenye images, utakachokiona ndio Mbeya iko hivyohivyo
View attachment 3480023
Hili suala linaniuma mno, kwa sababu hapa Mbeya kuna mandhari nzuri sana, pia kwa maeneo niliyotembea sijawahi kuona sehemu yenye hali ya hewa nzuri kama Mbeya (hapa naongelea Mbeya mjini)
Huku kuna ardhi yenye rutuba, hali ya hewa ya baridi kidogo, msimu wa mvua zinanyesha za kutosha, pia kuna milima mizuri sana. Yani huku Mungu alipapendelea
Lakini sisi Wabongo tulivyoanza tu kujenga Mbeya, tukaharibu kabisa.
View attachment 3480024
Kwa sehemu ambayo ni nzuri hivi, hatukupaswa kujenga kiholela, tena nyumba za matofali mabichi
View attachment 3480028
Hebu angalia Uzunguni na Uhindini, huku walijenga wazungu. Pamepangiliwa vizuri hadi raha, ukipita huku pamependeza mno mpaka ukishuka Jakaranda Street nako mambo ni safi, lakini ni eneo dogo tu

Lakini sasa karibia 80% ya Mbeya ni ujenzi holela, Angalia Mabatini, Nzovwe, Iyunga kote huko na viunga vyake Ikuti, Inyala na Kalobe ni uswazi tupu, ukitoka Mwanjelwa kwenda nanenane hapa kati Ilomba ni uswazi tupu, watu wanajenga milimani hadi milima inapoteza mvuto. Trust me, milima ya Mbeya ni mizuri sana, lakini tusipoangalia itazidi kuchafuka siku zinavyozidi kwenda
Pia haya malori ya mizigo, ni heri yangetafutiwa njia ya kupita tu, yasikatize hapa mjini maana ndio chanzo cha msongamano na ajali kuwa nyingi hapa Mbeya.View attachment 3480029
View attachment 3480026
Mi naona Mbeya ingejengwa vizuri, plus ile milima, mvua, kabaridi na ukijani ingekuwa ni Switzerland ndogo kabisa. Lakini ona tumejenga uswazi tu. Ardhi ya Mbeya inatudai Watanzania, hatujaitendea haki kwa kweli. Sehemu nzuri kama ile tumeiharibu haribu tu
Kwa nature kitu kibaya Mbeya ni vumbi tu msimu wa Kiangazi, vingine vyote viko poa, sisi ndio tunapaharibu.
View attachment 3480027
View attachment 3480025View attachment 3480030
Ila sio Mbeya yote ni mbaya, kuna maeneo Isiese, Forest, Jakaranda, Uzunguni, kipande kidogo cha Mafiati pale maeneo ya CUoM, maeneo ya BOT, JB na kwa huku Iwambi kuna mtaa unaitwa Maziwa, ni mpya watu wanajenga sasahivi, (huku Maziwa watu wanajenga nyumba za maana kama za Ulaya vile, mpaka miaka 5 ijayo patapendeza sana)
Sasa kama wenye Jiji hawaoni umuhimu wa kulipanga pia Wenyeji wa huko ni wabishi sana kukubali maelekezo ya serikali.

Mbeya wapunguze na kuacha ukuaji Ili mambo yaende.

Anyway Mbeya

View: https://www.instagram.com/reel/DWiaB8JjGft/?igsh=MW1pMnA1aGcyejByYg==
 
Back
Top Bottom