Jiji la Mbeya: Hapa Wabongo tumechemka

Jiji la Mbeya: Hapa Wabongo tumechemka

Shule mlienda kufanya nini?.
Huwa mnadhani sifa mojawapo ya mahali kuwa jiji ni majengo? Hamfikilii suala la idadi ya watu, pato lake na , maendeleo ya watu wa mahala hapo?.

Hivi hujui huo mkoa una hadhi ya jiji tangu miaka ya nyuma lakini siasa zenu za CCM ndizo zinarudisha nyuma mkoa.

Inawezekana vipi Mkoa nambari 3-5 ktk uchangiaji wa pato la taifa lkn kodi hazirudi kukarabati miundombinu, Central government unajua inakomba kodi kubwa kutoka Mbeya ,lkn hakuna maendeleo yoyote yanayorudi hapo mkoani, si kimiundombinu hakuna linalofanyika

Huo ndio mkoa pekee maendeleo yake yanabebwa na wananchi by 90%, tofauti na hiyo mikoa yenu mnayopewa vipaumbele lkn bado wananchi wenu wananuka umasikini.

Masikini wa Mbeya anauwezo wa kuwa tajiri mikoa ya kanda ya kati, Kusini, pwani yote na takataka za huko visiwani mnakojaza kodi
Mbeya hapana kuna miji inaidadi kubwa ya watu kuliko hio mbeya na mapato makubwa kuliko hio mbeya lkn still ni manispaa tu
 
Tanzania miji yote ina ujenzi holela tu ila kwenye jiji la Mbeya tumechemka 😂😂😂
Actually sitaki kuonesha picha za ujenzi holela hapa Mbeya lakini ukiingia Google, search tu "Mbeya" halafu nenda kwenye images, utakachokiona ndio Mbeya iko hivyohivyo
View attachment 3480023
Hili suala linaniuma mno, kwa sababu hapa Mbeya kuna mandhari nzuri sana, pia kwa maeneo niliyotembea sijawahi kuona sehemu yenye hali ya hewa nzuri kama Mbeya (hapa naongelea Mbeya mjini)
Huku kuna ardhi yenye rutuba, hali ya hewa ya baridi kidogo, msimu wa mvua zinanyesha za kutosha, pia kuna milima mizuri sana. Yani huku Mungu alipapendelea
Lakini sisi Wabongo tulivyoanza tu kujenga Mbeya, tukaharibu kabisa.
View attachment 3480024
Kwa sehemu ambayo ni nzuri hivi, hatukupaswa kujenga kiholela, tena nyumba za matofali mabichi
View attachment 3480028
Hebu angalia Uzunguni na Uhindini, huku walijenga wazungu. Pamepangiliwa vizuri hadi raha, ukipita huku pamependeza mno mpaka ukishuka Jakaranda Street nako mambo ni safi, lakini ni eneo dogo tu

Lakini sasa karibia 80% ya Mbeya ni ujenzi holela, Angalia Mabatini, Nzovwe, Iyunga kote huko na viunga vyake Ikuti, Inyala na Kalobe ni uswazi tupu, ukitoka Mwanjelwa kwenda nanenane hapa kati Ilomba ni uswazi tupu, watu wanajenga milimani hadi milima inapoteza mvuto. Trust me, milima ya Mbeya ni mizuri sana, lakini tusipoangalia itazidi kuchafuka siku zinavyozidi kwenda
Pia haya malori ya mizigo, ni heri yangetafutiwa njia ya kupita tu, yasikatize hapa mjini maana ndio chanzo cha msongamano na ajali kuwa nyingi hapa Mbeya.View attachment 3480029
View attachment 3480026
Mi naona Mbeya ingejengwa vizuri, plus ile milima, mvua, kabaridi na ukijani ingekuwa ni Switzerland ndogo kabisa. Lakini ona tumejenga uswazi tu. Ardhi ya Mbeya inatudai Watanzania, hatujaitendea haki kwa kweli. Sehemu nzuri kama ile tumeiharibu haribu tu
Kwa nature kitu kibaya Mbeya ni vumbi tu msimu wa Kiangazi, vingine vyote viko poa, sisi ndio tunapaharibu.
View attachment 3480027
View attachment 3480025View attachment 3480030
Ila sio Mbeya yote ni mbaya, kuna maeneo Isiese, Forest, Jakaranda, Uzunguni, kipande kidogo cha Mafiati pale maeneo ya CUoM, maeneo ya BOT, JB na kwa huku Iwambi kuna mtaa unaitwa Maziwa, ni mpya watu wanajenga sasahivi, (huku Maziwa watu wanajenga nyumba za maana kama za Ulaya vile, mpaka miaka 5 ijayo patapendeza sana)
Hapa duniani kila jiji hata NewYork kuna makazi yasiyopangiliwa wanakoishi watu maskini. Tena kuna majiji kuna watu hawana nyumna wanaishi mitaani.

Mbeya yaweza kuwa haijapangiliwa vizuri kwenye makazi ya watu wa chini, lakini wote wanaishi kwenye nyumba na siyo kwenye maboksi kama Mathare Nairobi, au mitaani kwenye madaraja kama ilivyo Mumbai India.

Mimi ni mzaliwa Mbeya ila naishi DSM, na nimetembea duniani zaidi ya nchi 20. Bado Mbeya iko vizuri, tuendelee kujivunia Mbeya yetu
 
Hapa duniani kila jiji hata NewYork kuna makazi yasiyopangiliwa wanakoishi watu maskini. Tena kuna majiji kuna watu hawana nyumna wanaishi mitaani.

Mbeya yaweza kuwa haijapangiliwa vizuri kwenye makazi ya watu wa chini, lakini wote wanaishi kwenye nyumba na siyo kwenye maboksi kama Mathare Nairobi, au mitaani kwenye madaraja kama ilivyo Mumbai India.

Mimi ni mzaliwa Mbeya ila naishi DSM, na nimetembea duniani zaidi ya nchi 20. Bado Mbeya iko vizuri, tuendelee kujivunia Mbeya yetu
Ushawahi fika mbeya??
 
Kama hapo ni kijiji, na huko vijijini kwenu kigoma, singida, morogoro kutakuwaje?, tuache lawama za kitoto badala yake tudeal na serikali ambayo ndio inajukumu la maendeleo ktk miji

Wanaojenga nyumba holela ni serikali au wananchi wasiotaka kutumia akili...

Mbeya imejengwa vibaya na haina hadhi ya kuitwa jiji...

Naona unataka kuweka ligi na mtu anayeijua Mbeya toka utawala wa Nyerere hadi sasa Samia...
 
Wanaojenga nyumba holela ni serikali au wananchi wasiotaka kutumia akili...

Mbeya imejengwa vibaya na haina hadhi ya kuitwa jiji...

Naona unataka kuweka ligi na mtu anayeijua Mbeya toka utawala wa Nyerere hadi sasa Samia...
Ndiyo limekuwa jiji sasa na huna la kufanya, wewe unatoka mkoa/ mji gani nami nikueleze vitingoji vibaya vya kwenu.
 
Mbeya hapana kuna miji inaidadi kubwa ya watu kuliko hio mbeya na mapato makubwa kuliko hio mbeya lkn still ni manispaa tu
Weka Data hapa acha longo longo, hivi unajua machokoraa wa mbeya wana maisha mazuri kuliko omba omba wa hapo singida na dodoma?.

Anyway twende kwa data weka hapa Top 10 ya mikoa inayoongoza kwa idadi ya watu na pato kwa Taifa, bila kusahau makadilio ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja, then utaona kuwa Mbeya ilishaendelea kitambo ktk maisha ya mtu mmoja mmoja, lkn kimiundombinu kawalaumu CCM na serikali inayokusanya kodi.
 
Kahama kailinganishe na Shinyanga acha mzaha.

Mbeya iko kwenye top 5 cities za Tanzania pamoja na Dar, Mwanza, Dodoma, Arusha.

Hiyo unayotaka kufananisha nayo wewe ni mawazo ya mvuta bangi.

Ukivuta bangi unaweza hata ukamkaripia baba yako mzazi ukidhani ni mshikaji wako
Sasa mbeya ni jiji lile la matope tu nyumba za udongo tu
 
Back
Top Bottom