Jiji la Mbeya: Hapa Wabongo tumechemka

Jiji la Mbeya: Hapa Wabongo tumechemka

Kahama kailinganishe na Shinyanga acha mzaha.

Mbeya iko kwenye top 5 cities za Tanzania pamoja na Dar, Mwanza, Dodoma, Arusha.

Hiyo unayotaka kufananisha nayo wewe ni mawazo ya mvuta bangi.

Ukivuta bangi unaweza hata ukamkaripia baba yako mzazi ukidhani ni mshikaji wako
Awa madogo wanajua hadhi ya jiji ni magorofa na hizo barabara za njia 4 wanazopita wakiwa kwenye mabasi, hawajui kuna mambo mengi ya kuzingatia ikiwepo idadi ya watu na pato lao, kiasi cha kodi wanachochangia, na mengine mengi ambayo kwa baadhi ya hizo sehemu wanazotaja haziufikii mkoa wa mbeya.

Kiuhalisia kwa Tanzania kimiundombinu tuko nyuma sana, inawezekana vipi hivyo vimanispaa na vihalmashauri kuwa na miundombinu mizuri kuliko majiji kama Tanga+Mbeya?.

Siasa za bongo ni haramu
 
Wapi Chunya?
Hata Chunya tu, kuna madini ya kutosha baadhi ya watu wanatafuta hela huko. Kuna watu wanadili na kilimo cha mpunga Mbarali, wengine wanasafirisha mpunga kutoka Kyela na kuja kuuza Mbeya mjini. Wengine wanasafirisha maharage kutoka Mbeya kupeleka mikoa mingine. Watu wanapiga mishe za kilimo na uuzaji wa mazao na ndio zinasaidia kuboresha maisha yao
 
Sawa mkazi wa ikuti, ivi ikuti mmeshajengewa soko pale??🤣🤣
 
Hata Chunya tu, kuna madini ya kutosha baadhi ya watu wanatafuta hela huko. Kuna watu wanadili na kilimo cha mpunga Mbarali, wengine wanasafirisha mpunga kutoka Kyela na kuja kuuza Mbeya mjini. Wengine wanasafirisha maharage kutoka Mbeya kupeleka mikoa mingine. Watu wanapiga mishe za kilimo na uuzaji wa mazao na ndio zinasaidia kuboresha maisha yao
Labda huko Mbalali, Rujewa nk kwenye shughuli za kiliimo cha mpunga ambako sijawahi kufika.

Ila kwa Chunya hapana.
 
Sasa kwa nchi nzima wapi pamejengwa kwa mpangilio?
Mini kikongwe iliyo fanyiwa planning na wakoloni mfano Yanga angalau mpangilio wa mitaa, nyumba na maeneo wazi ipo vizuri.
Kuanzia Mwinyi ndiyo mambo ya uswahili yalianza. Wote wsliofuata hawakuweka pesa ya urban planning.
 
Mbeya patamu kasoro NONDO tu!

Miaka ya 2006-10 nimekoswa kupigwa nondo mara kibao mitaa ya sinde na airport.
Wenyeji wa Mbeya usoni ni kama watu ila mioyoni hawana utu kabisa.
Mtu haona tabu kumuua mwanae au mtoto wa nduguye kisa katangaziwa dau la hela!
Kuhusu ujenzi holela, hilo ni tatizo la kitaifa na ni uzembe wa viongozi wa maeneo husika.
 
Hivi umewahi fika Mbeya? Hivi kuna sehemu pana matofari mazuri kama ya Mbeya hapa Tanzania. Matofari ya Mbeya ni matofari ya kuchoma, hayo ndio matofari mazuri na imara kuliko matofari yoyote duniani. Nyumba zote za zamani ambazo zipo mpaka leo zilijengewa matofali ya kuchoma.
 
Mmh, mbona matofali ya kuchoma kwenye nyumba nyingi za uswazi Mbeya sio imara kihivyo. Kuta hadi zinaota nyasi
Kama ni imara wangetumia kujenga na maghorofa marefu kama GR City Hotel, tuone kweli hayo matofali ni imara
 
Sijatembea mikoa mingi ila nina uzoefu na Jiji la Mbeya kiasi chake.

Ndio maana nilitoa maoni kuhusu Mbeya na sikupinga maoni yako kuhusu shughuli za kilimo kwenye influence ya biashara.
Sawa
 
Mbeya ukiisikia Kwenye radio na magazetini na Mbeya utakayoikuta live.

Unaweza kusema uko Baghdad Iraq
 
Tanzania miji yote ina ujenzi holela tu ila kwenye jiji la Mbeya tumechemka 😂😂😂
Actually sitaki kuonesha picha za ujenzi holela hapa Mbeya lakini ukiingia Google, search tu "Mbeya" halafu nenda kwenye images, utakachokiona ndio Mbeya iko hivyohivyo
View attachment 3480023
Hili suala linaniuma mno, kwa sababu hapa Mbeya kuna mandhari nzuri sana, pia kwa maeneo niliyotembea sijawahi kuona sehemu yenye hali ya hewa nzuri kama Mbeya (hapa naongelea Mbeya mjini)
Huku kuna ardhi yenye rutuba, hali ya hewa ya baridi kidogo, msimu wa mvua zinanyesha za kutosha, pia kuna milima mizuri sana. Yani huku Mungu alipapendelea
Lakini sisi Wabongo tulivyoanza tu kujenga Mbeya, tukaharibu kabisa.
View attachment 3480024
Kwa sehemu ambayo ni nzuri hivi, hatukupaswa kujenga kiholela, tena nyumba za matofali mabichi
View attachment 3480028
Hebu angalia Uzunguni na Uhindini, huku walijenga wazungu. Pamepangiliwa vizuri hadi raha, ukipita huku pamependeza mno mpaka ukishuka Jakaranda Street nako mambo ni safi, lakini ni eneo dogo tu

Lakini sasa karibia 80% ya Mbeya ni ujenzi holela, Angalia Mabatini, Nzovwe, Iyunga kote huko na viunga vyake Ikuti, Inyala na Kalobe ni uswazi tupu, ukitoka Mwanjelwa kwenda nanenane hapa kati Ilomba ni uswazi tupu, watu wanajenga milimani hadi milima inapoteza mvuto. Trust me, milima ya Mbeya ni mizuri sana, lakini tusipoangalia itazidi kuchafuka siku zinavyozidi kwenda
Pia haya malori ya mizigo, ni heri yangetafutiwa njia ya kupita tu, yasikatize hapa mjini maana ndio chanzo cha msongamano na ajali kuwa nyingi hapa Mbeya.View attachment 3480029
View attachment 3480026
Mi naona Mbeya ingejengwa vizuri, plus ile milima, mvua, kabaridi na ukijani ingekuwa ni Switzerland ndogo kabisa. Lakini ona tumejenga uswazi tu. Ardhi ya Mbeya inatudai Watanzania, hatujaitendea haki kwa kweli. Sehemu nzuri kama ile tumeiharibu haribu tu
Kwa nature kitu kibaya Mbeya ni vumbi tu msimu wa Kiangazi, vingine vyote viko poa, sisi ndio tunapaharibu.
View attachment 3480027
View attachment 3480025View attachment 3480030
Ila sio Mbeya yote ni mbaya, kuna maeneo Isiese, Forest, Jakaranda, Uzunguni, kipande kidogo cha Mafiati pale maeneo ya CUoM, maeneo ya BOT, JB na kwa huku Iwambi kuna mtaa unaitwa Maziwa, ni mpya watu wanajenga sasahivi, (huku Maziwa watu wanajenga nyumba za maana kama za Ulaya vile, mpaka miaka 5 ijayo patapendeza sana)
Ni mji mzuri sana kama ungepangiliwa
 
Back
Top Bottom