Jiji la Dar es Salaama - Dar es Salaam Tanzania historia yake na Uislam

Libya

JF-Expert Member
Nov 11, 2016
783
1,918
Kabla ya mwaka 1868, Jiji linalofahamika kwa jina la Dar es Salaam, halikuwepo kabisa. Badala yake kulikuwa na mji ulioundwa na miji mitatu maarufu, ambayo ni Kunduchi, Mbwamaji na Tindwa. Kila mji ulijitegemea, huku idadi ya wakazi wake wote kwa jumla haikuzidi watu 2,000.

Kati ya miji hiyo mitatu, miji miwili ya Kunduchi na Mbwamaji bado ipo hadi leo huku mji wa Tindwa, uliokuwa na eneo kubwa zaidi, ulimezwa na nguvu za matukio ya kihistoria yaliyosababishwa na mabadiliko na mpangilio mji mzima wa jiji.

Tukio kubwa la kihistoria lililobadili mpangilio wa miji hiyo mitatu na kuzaliwa kwa Jiji ambalo leo hii linalofahamika kama Dar es Salaam lilitokea mwaka 1865 pale Sultani Majid, aliyekuwa mtawala wa Zanzibar, kununua eneo kubwa la ardhi ya mji wa Tindwa, iliyomilikiwa na Sharif Attas na Jumbe Tambaza (machifu wa Kimashomvi), eneo hilo lilianzia Bustani ya Mnazi Mmoja karibu na Mnara wa Saa (Clock Tower) mpaka Magogoni (Ferri) mpaka kuelekea Daraja la Selender kutokezea Upanga lilikuwa ni Shamba la Jumbe Tambaza.

Lengo la Sultani huyo la kununua ardhi hiyo inayoanzia eneo la Magogoni hadi eneo la Hospitali ya Osheni Rodi (Ocean Road), eneo ambalo lilikuwa pori linalotazama Bahari ya Hindi na ambalo lilikuwa na ukimya, kiasi cha wakazi wa eneo la Tindwa kulipa jina la Mzizima, kwa sababu kila aliyepita eneo hilo alihisi mwili wake kusisimka na kuzizima kwa hofu ya kuwaogopa Wanyama pori.

Alinunua hilo eneo na kujenga majengo makubwa kwa ajili ya kufungua chuo/ shule ya kufundisha dini ya Kiislamu kwa lengo la kueneza Uislamu kutokea hapo kuelekea maeneo mengine ya Mrima, Pwani na Bara hadi Kongo na Burundi na kwa watu wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika ya Kusini na Afrika ya Kati.

Baada ya kununua eneo hilo, mwaka 1865 Sultani Majid aliingiza manuari kubwa za mizigo, zinazokadiriwa kuwa kati ya tatu hadi saba, zikiwa zimesheheni vifaa vya ujenzi na wataalamu wa ujenzi wa majengo ya chokaa na mawe, toka nchi za Bara Hindi na Uajemi. Na ndipo ujenzi wa majengo hayo ulipoanza kwenye eneo hilo la Mzizima mkabala na pwani ya Magogoni, huku majengo mengi yakijengwa eneo la Ocean Road.

Pamoja na Ikulu ile ya Magogoni, Seyyid Majid pia alijenga lile jumba la ‘Ocean Road Cancer Institute’ (ORCI) kwa sasa, ambalo mwanzoni lilikuwa ni Msikiti Mkubwa wa Ijumaa.

Ujenzi wa majengo hayo ulichukua takribani miaka mitatu na kukamilika mwaka 1868 na Sultani Majid mwenyewe alilipa jengo moja kubwa lilipo Magogoni hadi leo, jina la Dar us Salaama (tamka Daru Salaam), maneno ya Kiarabu yenye maana ya Nyumba ya Utulivu au Nyumba ya Amani. Na katika lango kuu pameandikwa maneno kutoka kwenye Qur’an Suuratul Hijr Ayah ya 46 isemayo (ٱدْخُلُوهَا بِسَلَـٰمٍ ءَامِنِينَ) Udkhuluuhaa Bisalaamin Aaminiin (Ingieni kwa salama na amani).

Wakoloni wa Kizungu walipokuja Tanganyika, mahala hapo ambapo palikuwa ni Msikiti Mkubwa wa Ijumaa, pakafanywa hospitali iliyojulikana kama ‘Ocean Road European Hospital’, iliyokuwa ikiwatibia Wazungu peke yao.

Na ndio utaona vijana wengi jiji la Dar es Salaam waliozaliwa baada ya uhuru kati ya miaka ya 60 - 70, wamezaliwa kwenye hospitali ya Ocean Road, ambayo sasa ni maalum wa kutibu saratani (Ocean Road Cancer Hospital), na kabla ya hapo yalikuwa ni majengo ya msikiti na mabweni ya vijana na wazee waliokuja kusoma Dar Us Salaam na bado mpaka leo muonekano wake ni ule ule.

Ikulu ile ya Magogoni wakati huo, ilikuwa imezungukwa na misikiti kadhaa ambayo yote, katika Utawala wa Kijarumani, ilibadilishwa matumizi na kufanywa taasisi nyengine.

Misikiti mingine iliyobaki ikasambaratishwa na kutumiwa kwa shughuli nyengine, ukiwamo Msikiti mkubwa uliokuwa baharini pale Forodhani, jijini Dar es Salaam, ulipogeuzwa kutoka msikiti na kuwa Kanisa la Mtakatifu Joseph mpaka hivi leo.

Kuanzia hapo, wakazi wote wa miji mitatu ya Kunduchi, Mbwamaji na Tindwa, wakabadili jina la Mji wa Tindwa na kuubatiza jina la jumba hilo kubwa kuwa Dar us Salaama, jina ambalo baadae lilimeza hata majina ya miji ya Kunduchi na Mbwamaji na kuifanya iwe vitongoji tu katika mji wa Dar us Salaam.

Kwa takribani miaka kumi tangu kufunguliwa kwa jengo hilo, raia toka nchi mbalimbali kuanzia Tanganyika, Msumbiji, Zaire, Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda, walimiminika katika jumba hilo na kupata elimu ya Uislamu iliyotolewa na masheikh wakubwa toka nchi za Uarabuni, Lamu na Mombasa Kenya na Zanzibar.

Kati ya mwaka 1875 na 1878, Wajerumani walivamia Tanganyika na kuiweka katika himaya ya utawala wao, na jengo hilo lilibadilishwa matumizi yake toka kuwa kitivo cha elimu ya Kiislamu na kuwa makao makuu ya serikali ya Kijerumani na baadae kuwa makazi ya Mtawala wa Kiingereza na leo hii ni Ikulu ya Taifa.

Mbali ya kubadilishwa jina kwa jengo hilo, toka Dar ul Salaam na kuwa Ikulu, hata jina lilipewa mji wake kutokana na jengo hilo pia limebadilishwa toka Dar us Salaama (Nyumba ya Utulivu/Amani) na kuwa Dar es Salaam (Bandari ya Amani) ambayo wajuzi wa lugha ya Kiarabu wanakata kuwa neno hilo Dar es Salaam halina maana ya Bandari salama
 
Bora wajerumani walivyokuja.

Maana nawaza tu kama wazungu wasingekuja ingekuwaje..

Maana waarabu walikuwa wanajenga misikiti tu na vituo vya elimu ya uislamu tu. Kwenye historia uliyoandika Sijaona hospital wala shule ya elimu dunia ambayo wameijenga waarab, ni wazungu ndio walipora majengo na kugeuza hospitali
 
warabu waliporwa miskiti yao ?
 
Mimi sijui Historia vyema, lakini kila nikijaribu kuisoma hii stori ya jiji la Dar iliyowekwa hapa kuna vitu vinakataa, akili onagoma kuikubali, ni kama utunzi fulani uliochanganya ukweli mdogo uliopambwa na uongo mwingi.

Twende taratibu kuweza kuchambua, maana hii ni JF, home of great thinker.

1. Time frame ya matukio haikubaliani na historia.
Yaani Sultani wa Zanzibar kauziwa eneo la Tindwa 1865 likiwa ni pori tupu lenye msitu mnene, ndani ya miaka mitatu tu kaweza kujenga utitiri wa majengo makubwa ambayo mleta mada anadai yalikuwa ni misikiti na kufikia mwaka 1875 Mjerumani alitwaa hilo eneo likiwa ni mji kamili wenye bandari na utitiri wa watu na majengo ambayo hapo hapo akaanza kuyageuza kuwa Ikulu, makanisa na Hospitali kubwa za kutumiwa na watu wakiwemo wazungu! Akili inagoma, nakataa.

2. Dhima ya Sultani kununua eneo la bara na hapo hapo kuligeuza kuwa chuo cha kiislamu kwa ukanda wote wa Afrika inakinzana.
Yaani Sultani wa Zanzibar ambaye alikuwa ana miliki visiwa vya Unguja na Pemba kama mali yake binafsi, aache kujenga chuo kikubwa cha kiislamu kule Zanzibar lakini atafute eneo bara ili kuja kujenga chuo kikubwa cha kiislamu! Akili inagoma, nakataa.

3. Mjerumani kuja kuchukua msikiti mkubwa ili kuufanya kanisa katoliki!
Sote tunajua mkoloni wa kijerumani kidini alikuwa mkristo wa kilutheri, ni vipi atwae msikiti halafu aufanye kuwa kanisa kuu la katoliki! Akili inagoma, nakataa.

4. Sultani wa Zanzibar kumiliki manuwari kadhaa ili kubeba vifaa vya ujenzi kutoka mashariki ya mbali kuja kujenga misikiti Tanganyika!
Kihistoria manuwari ni meli kubwa za kivita zilizokuwa zimilikiwa na mataifa ya Ujerumani na Uingereza, kwa miaka hiyo Sultani alikuwa busy na mashua tu na meli chache za kubeba watumwa (tena meli zikiwa za wazungu). Katika hili la Manuwari za sultani kubeba vifaa vya ujenzi vya kuletwa Tanganyika, Akili inagoma, nakataaa.

5. Idadi ya watu wote wa Dar na uwekezaji wa Sultani havioani.
Ni vipi eneo lenye wakazi wasiozidi 2000 tu (wakiwemo wanawake na watoto, ambao sio waumini wa kila siku kuswali misikitini) likajazwa utitiri wa misikiti mikubwa ndani ya miaka mitatu tu toka Sultani anunue sehemu hiyo? Akili inagoma, nakataa!

6. Sultani kuleta vifaa vya ujenzi kutoka bara hindi ili kujenga misikiti Tanganyika.
Yaani Sultani atoe meli bara hindi likiwa limebeba mpaka mawe na chokaa ili kuja kujenga misikiti Tanganyika huku akiacha rasilimali hizo zikiwa zimejaa tele Tanganyika! wakati Sultani alikuwa anaswaga mpaka watumwa wagonjwa na waliodhoofu kutoka Tanganyika ili kwenda kuwauza ng'ambo, leo awe mwema kuleta vifaa vya kutoka nje kuvileta Tanganyika tena msikitini!

7. Eneo lenye wakazi wasiozidi 2000 kuweza kujenga majengo makubwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu tu!
Hivi nguvu kazi ya kujenga hayo majengo ilitokea wapi?
 
Usilolojuwa ni kuwa Waislam ndio walioanzisha hospital, Waislam ndio waliosnzisha chuo, duniani.

Elimu uliyonayo chanzo chake ni Waislam. Hata herudi unazotumia kuandikia zinaitwa "alphabet" ambayo inatokana na Alif Be Te.

Simu uliotumia kuandikia ujumbe wako chanzo chake ni wasomi wa Kiislaam.

Mzungu kaja kukugawa akutawale, wewe unamuona wa maana. Muislam aliyeingia cha kwanza kabisa kajenga chuo ili uelimike, hilo hulioni! Hakika huo ni ujinga wa asili, ni wa kukupa pole tu.
 
Usilolojuwa ni kuwa Waislqm ndio walioanzisha hospitality, waislqm ndio waliosnzisha chuo, suniani.

Elimu uliyonayo chanzo chake ni Waislam. Hata herudi unazotumia kuandikia zinaitwa "alphabet" ambayo inatokana Alif Be Te.

Simu ukutumia kuandikia ujumbe wake chanzo chqke ni wasomi wa Kiislaam.

Mzungu kaja kukugawa akutawale, wewe unamuona wa maana. Muislam aliyeingia cha kwanza kabisa kajenga chuo ili uelimike hilo hulioni¹. Hakika huo ni ujinga wa asili, ni wa kukupa pole tu.
Ujinga mtupu umeandika hapa..hivi shule ulienda kusomea upopoma ....soma tena ulichoandika.
 
Usilolojuwa ni kuwa Waislqm ndio walioanzisha hospitality, waislqm ndio waliosnzisha chuo, suniani.

Elimu uliyonayo chanzo chake ni Waislam. Hata herudi unazotumia kuandikia zinaitwa "alphabet" ambayo inatokana Alif Be Te.

Simu ukutumia kuandikia ujumbe wake chanzo chqke ni wasomi wa Kiislaam.

Mzungu kaja kukugawa akutawale, wewe unamuona wa maana. Muislam aliyeingia cha kwanza kabisa kajenga chuo ili uelimike hilo hulioni¹. Hakika huo ni ujinga wa asili, ni wa kukupa pole tu.
images (9) - 2022-05-11T165831.838.jpeg
 
Bora mjerumani alivyo kuja kuingilia kati...itoshe kusema dsm ya sasa niya kila mtu haina mmiliki.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi sijui Historia vyema, lakini kila nikijaribu kuisoma hii stori ya jiji la Dar iliyowekwa hapa kuna vitu vinakataa, akili onagoma kuikubali, ni kama utunzi fulani uliochanganya ukweli mdogo uliopambwa na uongo mwingi.

Twende taratibu kuweza kuchambua, maana hii ni JF, home of great thinker.

1. Time frame ya matukio haikubaliani na historia.
Yaani Sultani wa Zanzibar kauziwa eneo la Tindwa 1865 likiwa ni pori tupu lenye msitu mnene, ndani ya miaka mitatu tu kaweza kujenga utitiri wa majengo makubwa ambayo mleta mada anadai yalikuwa ni misikiti na kufikia mwaka 1875 Mjerumani alitwaa hilo eneo likiwa ni mji kamili wenye bandari na utitiri wa watu na majengo ambayo hapo hapo akaanza kuyageuza kuwa Ikulu, makanisa na Hospitali kubwa za kutumiwa na watu wakiwemo wazungu! Akili inagoma, nakataa.

2. Dhima ya Sultani kununua eneo la bara na hapo hapo kuligeuza kuwa chuo cha kiislamu kwa ukanda wote wa Afrika inakinzana.
Yaani Sultani wa Zanzibar ambaye alikuwa ana miliki visiwa vya Unguja na Pemba kama mali yake binafsi, aache kujenga chuo kikubwa cha kiislamu kule Zanzibar lakini atafute eneo bara ili kuja kujenga chuo kikubwa cha kiislamu! Akili inagoma, nakataa.

3. Mjerumani kuja kuchukua msikiti mkubwa ili kuufanya kanisa katoliki!
Sote tunajua mkoloni wa kijerumani kidini alikuwa mkristo wa kilutheri, ni vipi atwae msikiti halafu aufanye kuwa kanisa kuu la katoliki! Akili inagoma, nakataa.

4. Sultani wa Zanzibar kumiliki manuwari kadhaa ili kubeba vifaa vya ujenzi kutoka mashariki ya mbali kuja kujenga misikiti Tanganyika!
Kihistoria manuwari ni meli kubwa za kivita zilizokuwa zimilikiwa na mataifa ya Ujerumani na Uingereza, kwa miaka hiyo Sultani alikuwa busy na mashua tu na meli chache za kubeba watumwa (tena meli zikiwa za wazungu). Katika hili la Manuwari za sultani kubeba vifaa vya ujenzi vya kuletwa Tanganyika, Akili inagoma, nakataaa.

5. Idadi ya watu wote wa Dar na uwekezaji wa Sultani havioani.
Ni vipi eneo lenye wakazi wasiozidi 2000 tu (wakiwemo wanawake na watoto, ambao sio waumini wa kila siku kuswali misikitini) likajazwa utitiri wa misikiti mikubwa ndani ya miaka mitatu tu toka Sultani anunue sehemu hiyo? Akili inagoma, nakataa!

6. Sultani kuleta vifaa vya ujenzi kutoka bara hindi ili kujenga misikiti Tanganyika.
Yaani Sultani atoe meli bara hindi likiwa limebeba mpaka mawe na chokaa ili kuja kujenga misikiti Tanganyika huku akiacha rasilimali hizo zikiwa zimejaa tele Tanganyika! wakati Sultani alikuwa anaswaga mpaka watumwa wagonjwa na waliodhoofu kutoka Tanganyika ili kwenda kuwauza ng'ambo, leo awe mwema kuleta vifaa vya kutoka nje kuvileta Tanganyika tena msikitini!

7. Eneo lenye wakazi wasiozidi 2000 kuweza kujenga majengo makubwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu tu!
Hivi nguvu kazi ya kujenga hayo majengo ilitokea wapi?
FaizaFoxy na mwenzako Mohamed Said mjibu huyu jamaa maswali yake. Tuache kuudanganya Umma kwa kutukuza udini hapa JF
 
Usilolojuwa ni kuwa Waislqm ndio walioanzisha hospitality, waislqm ndio waliosnzisha chuo, suniani.

Elimu uliyonayo chanzo chake ni Waislam. Hata herudi unazotumia kuandikia zinaitwa "alphabet" ambayo inatokana Alif Be Te.

Simu ukutumia kuandikia ujumbe wake chanzo chqke ni wasomi wa Kiislaam.

Mzungu kaja kukugawa akutawale, wewe unamuona wa maana. Muislam aliyeingia cha kwanza kabisa kajenga chuo ili uelimike hilo hulioni¹. Hakika huo ni ujinga wa asili, ni wa kukupa pole tu.

Naomba ujibu hoja za Zanzibar-ASP
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom