Jiji DSM umeme umeshakatika tayari mapema hii!

Jiji DSM umeme umeshakatika tayari mapema hii!

Nipo katikati ya mji hapa dar mgao siku ya 4 sasa,
 
Mwanza saizi ni masaa manne tu kwa siku. Simu inalala kwenye chaji maana umeme unapokuja tumelala fofofo na umeme unakatwa tumelala fofofo. Unajua kama umeme ulirudi unaona simu ina chaji, baaaasssii

Kwa heri ccm, hatutakaa kuikumbuka hili lichama
 
Acha matatizo ya zidi.. TARehe 25/10 iwakute wananchi bado wana hasira..
 
Inawezekana maana kuna mdau wa moro naye anasema umekatika!

nadhani hii ni operation endelevu kabisaah see
Yaani hawa jamaa mwisho wao sijui utakuaje aisee maana nadhani hata staffs wa TANESCO nafsi zinawasuta maana wanalazimishwa kusema uongo, maana tulianza na sababu ya MAFUTA MAZITO HAKUNA tukapigwa na mgao tukaendelea nao akaja Prof. Muongo akatuambia mgao ni historia pia kinachoendelea ni MITAMBO NA MIUNDOMBINU MICHAKAVU hivyo wanabadilisha nguzo na vitu vingine wakati ukipita mitaa mbalimbali huoni kama kuna kubadilisha miundombinu (unless kama miundombinu iliyochaa ilikuwa porini), sasa hivi tunaambiwa WANAUNGA MTAMBO WA GAS hivyo hali itatengemaa mpaka tarehe 20 wanaogopa kusema tarehe 26 October na kuendelea
 
Huku pia wameshakata...daaah!
Sasa hivi usiku inabidi ugeuke mchana maana shughuli zote zinafanyika usiku!

arusha kama kawa wameleta saa 4 usiku saa 10 hii asubuh wameshakata tayari

Huku tangu saa kumi alfajiri, Tanesco imefilisika na mgao mkali zaidi unakuja

Word mkuu umekata mapemaaaaa,.na jana nasikia ulirudi usiku sana,

Kuna faida gani ya kuwasha umeme usiku wa manane watu wamelala na kukata swalaaa saa kumi alfajiri bado watu wamelala? Ni Bora wazime kabisa umeme wajiapange na gesi zao za uongo na kweli.
 
Yaani hawa jamaa mwisho wao sijui utakuaje aisee maana nadhani hata staffs wa TANESCO nafsi zinawasuta maana wanalazimishwa kusema uongo, maana tulianza na sababu ya MAFUTA MAZITO HAKUNA tukapigwa na mgao tukaendelea nao akaja Prof. Muongo akatuambia mgao ni historia pia kinachoendelea ni MITAMBO NA MIUNDOMBINU MICHAKAVU hivyo wanabadilisha nguzo na vitu vingine wakati ukipita mitaa mbalimbali huoni kama kuna kubadilisha miundombinu (unless kama miundombinu iliyochaa ilikuwa porini), sasa hivi tunaambiwa WANAUNGA MTAMBO WA GAS hivyo hali itatengemaa mpaka tarehe 20 wanaogopa kusema tarehe 26 October na kuendelea

Wameshatufanya si watoto...walisema mwisho 1st sept ikafika wakasema katika ya sept kwasababu eti wanacompress gesi kwenye mitambo, tarehe 15 sept mkurugezi wa tanesco akaonyeshwa wakimalizia washa mitambo ya ubungo sasa sijui ule usanii walikuwa wanamuoneshea nani!?
 
Lowassa anazidi kuwabana Tanesco wamlipe hela zake kila siku tunaumia wananchi kumlipa
Hana huruma kabisa huyu fisadi.
 
Si unajua kibanda maiti imetapika,wanajaribu kufunuka jua kwa UNGO
 
Kahama tunateseka bila umeme. biashara nyingi zimesimama. tatizo ni nini nyie Tanesco. miaka 50 Serukali ya CCM haijui maana ya umeme. shame on you
 
Huku kwetu sijui ni muujiza gani umetokea leo.Tumezoe kila alfajir wanakata wanaleta usiku.
Leo nashangaa au mkata umeme anaumwa? Au wana kikao muhimu kinachofanyika upande wa huku kwetu? Au ni muujiza tu wamejisahau?
 
Kichwa cha habari kinajieleza!

Serikali ya ccm imechoka na kuchakaa mwili, roho na nafsi yake!

Hiki ni kipindi muhimu sana cha kubembeleza kura, lakini bado imeshindwa kuhimili uchovu na uchakavu wake!

Matangazo makubwa makubwa ya dhihaka na ya gharama kubwa kubwa yaliyoandaliwa dhidi ya Lowassa kupitia TBCccm na StarTVccm yatatazamwaje bila umeme?

Serikali imechoka na inahitaji kupumzishwa kwa amani na upendo!

Iombe msamaha kwa wananchi wake kwa matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa!

Kuchagua tena serikali ya CCM ni sawa na kuchagua gharama kubwa za maisha, kuporomoka kwa uchumi kila uchwao!

CCM imechoka na inajua hili! Kwamba eti inaingiza gesi kwenye mitambo yake ni danganya toto!

Ukweli ni kuwa mgao wa escrow hasa ule uliobebwa na masantarusi kupitia stanbic ndio iliyofikisha shirika hapa lilipo! Kile kipande cha rugemalila kilikuwa hela ya kunywa maji!

Kwa hali ya maisha tuliyonayo sasa kwa upande tu wa mgao wa umeme inatosha kusema mtu yeyote anaeshabikia CCM ama ana matatizo sugu ya akili ama amelaaniwa!

Halafu eti Dr Slaa ama Mzee Mwanakijiji wanatuponda wapenda mabadiliko! Hakika nimewadharau sana!

Watu wapo marekani huko halafu wanabembea kwenye mapikipiki makubwa akina akina Steven Seagar halafu anatuambia sisi tusio na umeme tuwachague CCM!

Mnatudharau sana! Sijui mnatuonaje vile!



SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWENYE GRIDI YA TAIFA OKTOBA 3, 2015

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wote walioungwa kwenye gridi ya taifa kuwa leo Oktoba 3, 2015 majira ya saa 11 kasoro alfajiri kulitokea hitilafu-kwenye njia kuu ya kusafirisha umeme kati ya Hale na Kiyungi na kusababisha mikoa yote iliyoungwa kwenye gridi kukosa umeme.-

Umeme-ulianza kurejeshwa-majira ya saa moja asubuhi baada ya kuondoa hitilafu hiyo.-

Hata hivyo baadhi ya maeneo yataendelea kukosa umeme kwa sababu ya upungufu katika uzalishaji wa umeme hasa katika vituo vya maji.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.-

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao
 
Lowassa anazidi kuwabana Tanesco wamlipe hela zake kila siku tunaumia wananchi kumlipa
Hana huruma kabisa huyu fisadi.
Mijitu mipuuzi kama wewe ningekuwa karibu na wewe ningekupiga jambia la mk**d*ni ili iwe fundisho...

Watu tunalala na njaa na biashara zetu tumefunga kwa sababu ya umeme wewe unaleta utani. Huyo Magufuli wako anasema ataleta viwanda lakini hajawahi hata kutamka neno umeme kwenye kampeni zake sijui hivyo viwanda atawasha kwa kuni...
 
Back
Top Bottom