Jiji DSM umeme umeshakatika tayari mapema hii!

Jiji DSM umeme umeshakatika tayari mapema hii!

Nilidhani kipindi hiki cha kampeni tuta pakwa mafuta walau kwa mgongo wa chupa ili kubembeleza kura, lakini wapi!!
kama kipindi cha kampeni wanaweza kuwa kibri cha kutufanyia hivi, baada ya uchaguzi wakishinda itakuwaje?
 
Hata huku singida wameuchukua saa mingi, kuna wakat najiuliza, hivi hio gesi inatumia umeme au inazalisha umeme, manake tangu waseme wanaunganisha mitambo ya umeme wa gesi kwenye grid ya taifa hali imekua mbaya zaid, shime watz tusiichague ccm watatumalizia kdogo kilichobaki.

Swali kama hilo ndo hata Mimi linaniumiza kichwa! Manake kabla ya kuwashwa ka mitambo hii angalao nilikuwa tunapata umeme kiasi, lakini sasa imekuwa ni shida! Kuna haja gani yankuiwasha sasa? Bora turudi kule tulikokuwa! Tanesco jamani hv kweli manajilipa mishahara kweli? Mramba unaridhika kabisa Na hali hii? Mtakuwa Na matatizo ya kufukiria!
 
Lowassa>>Rostam >>Richmond >>Dowans>>>Symbian. .....Ni vigumu kumtenganisha Lowassa na hii adha ya umeme, anaujua mchezo mzima ila ndio hivyo tena, wajinga ndio waliwao.

Tatizo lingine tulilonalo watz ndo hilo, kukaririshewa! Richmond Richmond hv kweli unadhani Richmond pekee ndo nimetufikisha hapa? Tuache kuaminishwa vipi vinginevyo visivyokuwa vya msingi, Mara kumi hata hiyo mitambo ya Richmond inazalisha umeme ambao ndo huu mdogo tunapata kuchajia simu zetu!
 
Moro mjini: Ulirejea saa 10:33:23pm na umekatwa tena Saa 04:37:21am alfajiri ya leo hapo tunahesabia masaa 18 kurudi
 
kwenye kampeni namsikia mgombea asema atajenga viwanda hivyo sijui vitakuwa na power bank pengine, kwa hali hii viwanda vya nini, ikiwa uchumi wa mtz sio wa viwanda!?
 
Ukerewe napo hakuna umeme toka saa 10 CCM wanakera sana.
 
Nipo Njombe hapa.Walikata saa nne usiku jana. Lodge yenyewe niliyopo inategemea umeme wa TANESCO. Nimeoga maji ya baridi
 
Singida pia wamekata asubuhi. Yawezekana shida ya umeme ipo nchi nzima.
 
Duuu hapa Geita toka jana alfajiri mpaka leo saa hii hatujaona tone la umeme ni shgdah....
 
Niko VETA Mbeya.....huku tumeshazoea umeme kukatwa na ndio maana tunataka tumesha ifuta CCM muda mrefu. Tuungeni mkono nyie wana Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom