Jihadhari na mtu usiyemjua anayekushobokea

Jihadhari na mtu usiyemjua anayekushobokea

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,144
Reaction score
166,082
Tahadhari tumepewa,

Habari zenu mabibi na mabwana! Poleni na majukumu,

Napenda niwashirikishe jambo lililo nikuta ili kukuokoa wewe au mwingine. kuna wizi wa ajabu wa aina fulani ya madawa ya kupoteza ufahamu.

Jana nikiwa natoka kazini mida ya jioni nikapita Mlimani City. Baada ya kufika Mlimani City ghafla nilisikia mtu akiniita jina langu nilipogeuka nilimuona mtu akinichangamkia sana na kuniuliza habari za siku, uko wapi zikuhizi? Nikawa nimepigwa namshangao mana nikimuangalia simkumbuki kabisa anae nichangamkia. Mara yule bwana akanisogelea na kuniambia hunikumbuki tulisoma wote? Kabla sijamjibu Mara akatokea mtu mwingine kama wanafahamiana wakachangamkiana kisha yule bwana akaanza kunitabulisha kwa huyu bwana alietukuta pale.

Ghafla yule bwana akaniambia kuna mdudu kwenye jicho lako la kulia nilipotaka kutoa akaniambia samahani naomba nikutoe kama hutojali. Kabla sijamruhusu akachukua kitambaa chake akanipangusa nacho kwenye jicho na puani. Gafla nikaanza kujisikia vibaya na baada ya hapo sijajielewa tena mpaka nilipojikuta niko hospital Rabininsia Dar.

Nikaelezwa kuwa nimepelekwa hapo na wasamaria wakiwa wameniokota maeneo ya Vikawe nikiwa sijitambui pembezoni mwa barabara. Nilikuwa na pesa kama laki 320000 walichukua pamoja na card yangu ya crdb. Cha ajabu nilipotoka hospitali nikaenda moja kwa moja bank nikawaelezea wakaniambia nikaripoti police.

Kabla hawaja iblock ile card waliniangalizia balance wakakuta card imetoa pesa ATM mbili Jana na Leo sh. milioni 2. Tulipofatilia kwenye ATM mojawapo ya Jana yake ikakuwa aliezitoa hizo pesa ni mimi mwenyewe nikiwa na mtu alikuwa ameficha sura yake na kwenye ATM ya pili ikakutwa ni yule mtu aliye ficha sura yake.

So my Dear friend, usimruhusu mtu yeyote usiyemjua kukugusa au kukutoa kitu machoni. Maana si kukuibia tu bali wanaweza kukulewesha na wakakufanye vitendo vya wakakuingilia vibaya wakakuambukiza hata magonjwa hatari.
 
Unapokuwa unapost huwa unampigia nani kumwambia unapost ndugu...?
Wewe KIOO, naamini ni mzuri sana kwenye ushauri wa thread, maana una historia ya thread zote zinazoanzishwa majukwaa yote Jf.
Halafu nina swali, mbona siku hizi silioni jukwaa la Mambo ya Wakubwa? Nataka nikajiachie kule Na MBITIYAZA
 
Kweli wanaweza kuchukua hela wakala na ndogo yako tena getoni kwako
 
Back
Top Bottom