Jifunze kutengeneza scrub ya kahawa" Coffee Scrub" kwa ajili ya biashara au matumizi binafsi

Beeb

JF-Expert Member
Aug 18, 2018
29,402
58,951
Mahitaji

-Sukari ya brown kikombe kimoja
-Kahawa ya brown nusu kikombe
-Mafuta ya mzeituni nusu kikombe
-Lemon essential oil kijiko kimoja Cha chai(1tsp)

Hapo kwenye kikombe waweza tumia kikombe Cha chai(mug)au vile vikombe maalum vya kupimia malighafi vile ambavyo vina alama za vipimo.

Hii scrub ni nzuri mno na inafanya kazi vizuri pia..inatumika kwaa jinsia zote.

Inafanya ngozi kua clear
Inaglow
Inafifisha michirizi na cellulite
Inaondoa wrinkles
Alama nyeusi mwilini mfano mabaka nk.
Kiufupi hii scrub ni nzuri mno utakapoitumia.

Angalizo: Kama una tatizo na kahawa hii scrub haikufai.

Niwatakie asubuhi njema.
Ahsanteni.
 
Kuna dada alikua na chunusiiiiii nikawa namuona Amepaka mavitu meusi usoni

sikua najua ni kitu gani,kuna siku nikamuuliza kulikon unatutsha na masinzi usoni

ndio akaniambia huwa anapaka scrub ya "cofee" ili imsaidie kuondoa chunusi asee

kweli yule dada alikua na chunusi ila siku hizi ule uso n mzuriiiii,nadhan hizi scrub zina faida sana
 
Saana...
 
JIFUNZE KUTENGENEZA MAFUTA MAZURI YA KUJAZA NA KUKUZA NYWELE KWA AJILI YA BIASHARA AU MATUMIZI BINAFSI

heyloooow!!!!..
Weekend inasemaje babes...nawapenda

Malighafi

Mafuta ya Nazi nusu kikombe
Mafuta ya mnyonyo Yale gold nusu kikombe
Mafuta ya vitamin E mls 14
Rosemary essential oil 7 drops..

Changanya hayo mafuta kwa pamoja yachanganyike.

Tayari kwa matumizi

Yanakuza nywele
Yanajaza nywele
Yanaondoa mba na muwasho katika ngozi
Yanazuia nywele kukatika
Ni mazuri mnoo😊

Nb:Kama utatumia haya Mafuta kwa mtoto tumia lavender essential oil drops 7 Kama ilivyo apo juu.. Rosemary essential oil si mazuri kwa watoto.

Tumia vikombe maalum vile vyenye alama za vipimo.

Naamini mtafaidika.. niwatakie weekend na jioni njema..
🙏🏿🙏🏿
 
Back
Top Bottom