msukuma.com
JF-Expert Member
- Joined
- Jan 21, 2016
- Messages
- 1,286
- Points
- 2,000
Mkuu ilikuwa ngumu ni sana mtu kukuelekeza kuna muda unaenda PM kwa mtu hakujibu au anajibu shortcut nikaona isiwe tabu nikaenda kwa kwa mwalimu wangu [Youtube] nikacheki video nyingi almost 3GB zilifia huko mwisho siku nikaelewa jinsi ya kununua Alibaba, Globalsources na Made in China.Mwagika sasa kk me bado c elewi
Baada ya hapo nikaanza ku-make deal na Suppliers , nikaona bado sielewi malipo yanakuaje bcoz nilijua huku ni kama Aliexpress, ikanibidi kurudi tena Youtube nikapua video nyingi za jinsi ya ku make payments alibaba baada ya hapo ndio nikajua kumbe ni lazima ku make payment kupitia Trade Insurance ili Mpunga wako uwe salama.
Baada ya hapo nikaanza ku chat na seller nia yangu ni kupata Shipping iliyo bora nikagundua Supplier wengi wanasema DHL Ndio Cheapest kwenye shipping ila kuna mmoja alisema nitumia HK [hongkong Shippinh], sikutaka mzigo upitie Kwenye meli.
Alibaba inahitaji umakini sana wa kumjua yupi ni Supplier bora na amekuwa verified na ana muda gani kwenye Game na je anakubali ku make payament kupitia TRADE INSUARANCE?. usipo angalia unapigwa Fasta kama Kariakoo vile.
Kama una wasiwasi na bidhaa husika unaweza kuomba kutumiwa sample.