Habari ndugu zangu, pole na uchovu wa siku nzima.
Leo nimeona niwasilishe haya mawazo kwa ufupi, ili tuweze kujadili na kuweza kujua nini cha kufanya ili tuweze kuvuka hatua moja kwenda nyingine.
Twende kwenye mada husika
Kwa kipindi kilefu nimejaribu kupitia na chunguza biashara za mtandaoni, nimeona upende wetu hatujaweza kufanya vizuri.
Kuna baadhi ya kampuni zilijaribu lakini hazikufanikiwa. Mfano Jumia Tanzania alifanya biashara hii kama miaka 2hivi nadhani hapa Tanzania lakini akaamua kufunga biashara yake.
Mwingine ni Michongo kutoka Dudumizi hosting nadhani kama sijakosea. Lakini na yeye biashara bado inajivuta flani hivi.
Biashara hii ya mtandaoni maarufu kama eCommerce imeshindwa kuleta ushawishi mkubwa hapa nchini, na kufanya watu wengi kuagiza mizigo yao kwenye tovuti (website) za nje ambapo wanalipia gharama kubwa, kuliko tungekuwa na tovuti zetu ambapo tungeweza kuingizia serikali yetu mapato zaidi.
Kama Tanzania hapa tungeweza kubuni tovuti kama eBay, Amazon au hata kikuu basi. Watu wakaagiza mzigo kutoka China, USA na nchi nyinginezo. Au watu wakafanya manunuzi ya bidhaa za ndani na kulipia kwa TSH kama vile Jumia anavyo fanya. Nadhani tungeongeza thamani furani katika Nchi yetu.
Maana ndani ya nchi yetu hatuna tovuti za kibiashara, kifedha, nanyinginezo. Tovuti nyingi tunazo tumia ni za Nchi nyingine tena malipo kwa card za benki, inaumiza sana.
Njia za malipo tunazo, tena mitandao ya simu imelahisisha.
Je wewe mwenzangu unaona nini kiweze kufanyika ili tuweza kuleta heshima kwenye Nchi yetu?