Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Mkuu samahani nina swali maana nimeona wewe unaijua Skrill vizuri. Nimetuma pesa kupitia skrill na mpokeaji ni account crdb, katika kujaza nilipoweka tu Tanzania ikaniletea list za bank za kuchagua nikachagua CRDB na kuweka akaunti inayopokea na jina la anayepokea lakini hakuna iliponitaka niweke SWIFT CODE na nikatuma hiyo pesa.
Haiwezi kusumbua, au wanajaza hizo code automatically wenyewe?
 
CRDB na kuweka akaunti inayopokea na jina la anayepokea lakini hakuna iliponitaka niweke SWIFT CODE na nikatuma hiyo pesa.
Baada ya siku 2, iwapo hujapokea fedha wasilinana na pande zote mbili, Skrill na benki husika.

Ni kweli ukurasa wa skrill wa kutuma fedha benki hauna kipengele cha swiftcode.

1695162497570.png
 
Wakuu ebay ni sehemu ambayo wauzaji(Seller) na wanunuaji(Buyer) wanakutana
Muuzaji(Seller) anajiunga kwa kufungua Account ebay na kisha anatangaza kitu anachokiuza akiwa popote pale Duniani
Mnunuzi(Buyer) anajiunga kwa kufungua Account ebay popote alipo Duniani kisha anachagua bidhaa nayoitaka iliyotangazwa na Muuzaji(Seller) ana inunua online.

Ili kukamilisha zoezi la malipo na kuuziana bila kuibiana ndio sasa anaingia Pay pal
Pay Pal
ni njia ya malipo ambapo mtu yeyote anajiunga ili mradi awe ni mteja wa Bank inayotoa Card za Master au Visa Card
Kibongo Bongo CRDB wapo vizuri, baada ya kufungua Acc na kupewa Master/Visa Card yako unarudi tena CRDB kuomba wai link Master/Visa Card yako iweze kufanya online Transaction kwa kujaza form maalumu then you're done

Baada ya kadi yako kuwa Linked unajiunga kwa kufungua Acc Pay Pal kwa maana ya kwamba unawapa details za Account yako na kuwapa ruhusa kutoa pesa kwenye account unapo waomba kufanya hivyo

Jinsi ebay na Pay Pal wanavyofanya kukamilisha mpango mzima
ebay
ni kama soko ambalo watu hawaonani, mmoja yupo Hong Kong anauza iphone mwaingine Yupo Manzese Tz anataka kuinunua lakini wanakuta online through ebay. so huwezi ukamtumia tu mtu hela kwenye acc ya bank maana anaweza kuingia mitini na asiwepo wa kufuatilia
Sasa wanapotaka kulipana Pay Pal anaingia katikati kama bima wa malipo kwa kuhakikisha anamjua vyema Muuzaji(Seller) ambaye ndio mlipwaji

Mlipaji aka Mnunuzi(Buyer) aliyeko Manzese hamlipi direct mlipwaji aka Muuzaji(Seller) aliyeko Hong Kong,
Anachofanya Mnunuzi(Buyer) anampa ruhusa Pay Pal atoe pesa kwenye Acc yake ya bank kutumia Master/Visa kisha amlipe Muuzaji(Seller)
Kwakuwa Pay Pal anakuwa amechukua dhamana ya malipo ya mauziano yenu anawajibika kuhakikisha Muuzaji(Seller) ana bidhaa kweli anayouza na anaaminika atatuma kwa Mnunuzi(Buyer) kile alicho tangaza,....Fail to do so basi Pay Pal atawajibika kumrudishia Mnunuzi(Buyer) pesa yake, na baada ya hapo Pay Pal kushirikiana na ebay ndio watao mtafuta na kumbana Muuzaji(Seller) kwa utapeli alioufanya lakini wewe utakuwa tayari umerudishiwa pesa yako iwapo watajiridhisha kuna uvunjifu wa makubaliano.

CHANGAMOTO

Mara chache sana inaweza kutoke Muuzaji(Seller) akawa tapeli maana ili uwe Muuzaji ni lazima lazima ebay na Pay Pal watataka kujirisha lakini changamoto ipo baada ya kurudishiwa pesa zako
Mifumo ya Pay Pal yetu wanasema hairuhusu kupokea Pesa maana mabank nasikia sijui hayajaingia mikataba gani I dont know, so kibongo bongo acc zetu za pay pal ni kwa kulipia tu na si kupokea pesa(wataalamu watatusaidia katika hili)

Jambo lingine ni wizi wa mizigo Posta, binafsi ni muhanga wa hili.
Mwaka juzi niliagiza BlackBerry yangu lakini ilipotelea Posta na sijaipata hadi leo, nilianza kumsumbua Buyer lakini alinithibitishi mzigo umetumwa na hadi tarehe ulipopekelewa Bongo, nilipo wabana Posta wakaanza kunizungusha tu.
Na hii ndio maana Buyer wengi hawatumi(ship) mizigo Africa maana Posta za kiafrica ni majanga kwa wizi na hasa ukituma vitu vidogodogo vya thamani ya kuonekana kama Simu kamera nk, mara nyingi wana iba

Kuna baadhi ya items ukiagiza utakutana na mkono wa TRA, hawa jamaa ni wasumbufu balaa ukiingia kwenye kumi nanane zao, watakutwanga makodi hadi uchanganyike au la sivyo ukate "kitu kidogo"

Hakikisha unaangalia Feed back na Reputation ya Muuzaji(Seller)
Hakikisha unasoma kwa makini na kuelewa discription ya item, ikiwezekana muulize Buyer kama hujaelewa.
Epuka kutumia njia zingine zaidi ya Pay Pal kama means ya malipo.Unaweza ku bid item alafu ukashangaa unapoke email ianakuambia ipo items kama hiyo kwa bei ndogo......usi jaribu

Shipping nayo ni topic ndefu kidogo natumai wapo wadau wataifafanua vizuri
Hii fii sijaielewa ndugu...! Yaan kila unapolupia mtandaon bidhaa yoyote wanakata hiyo 22000/=?
 
Wakuu mambo vipi kama kuna mtu kashawahi fanya manunuzi kwenye mtandao wa 1688 akiwa Tanzania naomba msaada nimekwama sana.
 
Njia za malipo zipoje ? Hapa ndipo ninapokwama.

Tumia hizi virtual card za mitandao ya simu inakuwa rahisi zaidi.
So far nimeshatumia Master Card ya Airtel na Visa Card ya Vodacom, I think Tigo watakuwa na Master Card pia.

Cha kufanya ingia kwenye menu za pesa za mtandao husika tafuta hiyo huduma then tengeneza kadi utatumiwa message ya taarifa za card ambazo ni namba ya card, CVV number na tarehe ya card ku-expire,
Pia, huko kwenye hiyo menu utakutana na namna ya kuweka hela kwenye card.

Ukija huku ebay utakuja kuiweka taarifa za ile card kwa ajili ya malipo.

Note.
Malipo yote kupitia hizi Virtual Card wanakata 10% ya ile bei ya kitu unachonunua.
Mfano unanunua kitu bei yake pamoja na usafiri ni 100$ ambayo sawa na sh 254,500 wao watakukata sh 279,950 kwenye card yako.
Pia usisahau za wenzetu huwa zinabadilika thamani muda wowote. Huo mfano nimeutoa katika exchange rate ya 1$ sawa na sh 2,545
 
Wakuu hawa Speedaf kwa AliExpress wanafanya vizuri sana kwenye swala nzima la Delivery.
Naomba kuuliza vipi kwa upande wa mnaogazia vitu kutoka Ebay Je nako wapo hawa Speedaf ?
 
Back
Top Bottom