Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Kwanza hujui maana yashiriki .pia Mungu anapokea dua ndo maana akasema Adukhun astajiblakum .Nahiyo Albadry nidua yakumomba Mungu kama duwa zingine .so ww hujui kitu hata kur an hujasoma so tusibishane mambo ya Dino wakati hujui .chochocte mm nakwambia mameno yaMungu ww unaropoka unasema mambo yakijiweni .
Kaka usipotoshe umma, tubia kwa Allah, ahlul badri isomwayo kukaagizwa ndimu nyembe sindano na chungu na vyengine kisha vitu vikakaangwa pamoja katika chungu huku kukinuizwa maneno huo ni uchawi na hilo ni jambo ovu kuliko yote katika uislam,maana katika uislam hakuna dua yenye kuambatana na mambo hayo
Tafadhali tafuta elimu halisi ya dini yako wacha kurithi uovu utakao kuangamiza milele kama utakufa na uovu huo.
 
kwa ufupi ukisoma historia ya vita vya badru ni funzo kubwa mno kwa nguvu ya haki kupambana na nguvu ya washirikina

reference.

Quran: Al Imran 3:123–125 (Yusuf Ali). "Allah had helped you at Badr, when ye were a contemptible little force; then fear Allah; thus May ye show your gratitude. Remember thou saidst to the Faithful: "Is it not enough for you that Allah should help you with three thousand angels (Specially) sent down? "Yea, – if ye remain firm, and act aright, even if the enemy should rush here on you in hot haste, your Lord would help you with five thousand angels Making a terrific onslaught."
 
sio ifike kesho waanze kusema wanamuachia mungu aamua, au wanaepusha madhara kwa watu wasiojulikana ... Hiyo itakuwa sababu tosha ya kusema wasomaji walisema tu iki kutafuta kick au kutoa vitisho..
Hiyo kesho dude liamshwe tu, wasome hiyo kitu, kama ni mtu kudhurika na adhurike tu hatutaki visingizio.
Majibu ya Halbadiri ni ndani ya siku tatu hadi wiki mmoja.
 
kwa ufupi ukisoma historia ya vita vya badru ni funzo kubwa mno kwa nguvu ya haki kupambana na nguvu ya washirikina

reference.

Quran: Al Imran 3:123–125 (Yusuf Ali). "Allah had helped you at Badr, when ye were a contemptible little force; then fear Allah; thus May ye show your gratitude. Remember thou saidst to the Faithful: "Is it not enough for you that Allah should help you with three thousand angels (Specially) sent down? "Yea, – if ye remain firm, and act aright, even if the enemy should rush here on you in hot haste, your Lord would help you with five thousand angels Making a terrific onslaught."

Ni Kweli ina Mafunzo lakini yako Mbali na Huo Ushirikina (Uchawi)
Mnaounasibisha na Maswahaba Allah awaridhie
Ilhali wao wako Mbali nao

Na Mkitaka Kuthibitisha Juu ya Upuuzi huo wa Albadiri
Rejeeni HISTORIA ni Wapi Maswahaba Walifanya Ujinga huo
Na kizazi kilichofata baada ya Maswahaba na Karne zote tatu tukufu Hamtokuta mahala Upuuzi huo (Albadil) umesomwa
Bali ni Mambo yalokuja Zuliwa
 
Ni Kweli ina Mafunzo lakini yako Mbali na Huo Ushirikina (Uchawi)
Mnaounasibisha na Maswahaba Allah awaridhie
Ilhali wao wako Mbali nao

Na Mkitaka Kuthibitisha Juu ya Upuuzi huo wa Albadiri
Rejeeni HISTORIA ni Wapi Maswahaba Walifanya Ujinga huo
Na kizazi kilichofata baada ya Maswahaba na Karne zote tatu tukufu Hamtokuta mahala Upuuzi huo (Albadil) umesomwa
Bali ni Mambo yalokuja Zuliwa

hoja ni watu wajue maana ya neno albadir..
lakini pia warejee waangalie hali ilikuwaje kabla ya hivyo vita, na nini kilitokea vitani..
mwisho ninani alizua huu uzushi...


point ya herufi kubwa ni kwamba kwa waislam kuna aina za dua ambazo majibu yake ni fasta sana kurejeshewa
-kuna maombi ya aliyedhulumiwa...
-kuna maombi ya istikhara
-kuna dua ya ambao chombo kinasumbua baharini..

kingine ni kwamba allah anapenda mtu anaye muomba..na yupo karibu na muombaji...

nijuavyo kwa muislam anayejua dini najua anajua kuwa albadir ni uzushi, ila anaweza asijue baadhi ya dua mtume (rehema na amani ziwe juu yake alizisoma akiwa katika hali ngumu na zilijibiwa palepale , miungoni mwa dua hizo ni aya na tunazisoma daily..lakini watu hawajui.
 
Sasa wewe mfu mtarajiwa ni kama insolvency person u can't enter any valid agreement

"Insolvency person" tehe tehe tehe.

Hata kamaunaamini huo ujinga wa Al-badr na kuwepo kwa Mungu,kuna wimbo wa kipindi cha "Pole" una mashairi yanayosema.

"Ajuaye bwana Mola, kwa mzimakuwa mfu, mgonjwa kuwa salaaamaaa , eeeeh tunawapapole"

Kwa hiyo usishangae ukafa wewe msoma al-badr halafu miminadunda.

Weka hela hapa tuone kama unamaanisha unachosema au unapiga kelele tu.

That is, assuming una hela at all.

Inawezekana kelele nyingi kumbe majalala matupu.
 
Uchawi uliotukuka si bora mngeshika matunguri tuelewe moja acheni kumshirikisha mungu na mambo ya kijinga ....
 
Usilolijua ni kama usiku wa giza , wabongo tumezoea kuhukumu kila kitu badala ya kuangalia vitu vinavoleta maendeleo
 
Kwanza hujui maana yashiriki .pia Mungu anapokea dua ndo maana akasema Adukhun astajiblakum .Nahiyo Albadry nidua yakumomba Mungu kama duwa zingine .so ww hujui kitu hata kur an hujasoma so tusibishane mambo ya Dino wakati hujui .chochocte mm nakwambia mameno yaMungu ww unaropoka unasema mambo yakijiweni .
Ulicho andika hapo kwa kiarabu labda ni kinyaturu. Hakuna aya hapo.
Albadiri ni uchawi sio dua.
 
UBAINIFU JUU YA ALBADIRI

Ni kwa kipindi kirefu waislam na wasio kuwa waislam wanaamini kuwa "Albadir" ni Dua maalum ndani ya Uislam yenye lengo la kumuombea aliyekudhulumu nk kwa makusudio makubwa apate madhara imma kufa au kuwa kichaa nk.

Kiukweli hakuna Dua kama hii katika Uislam,hutaipata katika mafundisho(Hadith) ya Mtume Swalla llahu alayhi wasallam,si katika hadithi sahihi wala dhaifu.

Jambo hili au ushirkina huu uliopewa jina la Dua umepata umaarufu katika Nchi zetu za Afrika Mashariki hususani miji ya Pwani na mpaka unaaminika kwa baadhi ya uislam wasiotaka kujifunza dini yao katika vyanzo sahihi kiasi hata jamiii ya waislam wakiamini kweli waislam wanazo dua za namna hizi.

[HASHTAG]#Albadiri[/HASHTAG] ni nini????

Ni maombi ya kishirikina anayoomba mtu(muislam au asiye muislam) kwa lengo la kumdhuru aliyemdhulumu(au hata bila kumdhulumu) imma katika mambo kijamii,kiuchumi au kisiasa.

Maombi haya yanapelekwa kwa Majini yaende kwa muhusika kwenda kumtia ukichaa muhusika au kumvurugia mambo yake nk.

Albadiri ni kwa usahihi ni AHLUL BADR maana yake ni WATU WA BADR yaani Maswahaba walipigana Jihaad katika Viwanja Vya Badri nao walikuwa 314 wakiwa dhaifu mno na silaha duni wakawashinda Makafiri zaidi ya elfu moja waliojidhatiti mno kwa maandalizi na silaha nzito na wanyama.

Maswahaba hawa ni watukufu na wameridhiwa na ALLA hapa duniani na kesho Akhera.

[HASHTAG]#USHIRIKINA[/HASHTAG] huu umepewa jina hili kwa lengo la kuwazuga waislam ili waone kuwa hii ni Dua sahihi kama ilivyo dua zingine,na wanajifanya katika huo UCHAWI wao walioupa jina la Dua kuwa wanataja majina ya Maswahaba hawa kupitia Baraka zao wakubaliwa dua yao(Hili nalo ni makosa) hali ni uongo hawamuombi ALLAH na wanaomba Majini yao.

Washirikina hawa wanaoshrikikiana na MAJINI wote duniani ni wajanja sana na wana mbinu nyingi za kutaka kuwapeleka watu motoni.
Huwa wanamuendea Mtu kwa njia nzuri sana lakini malengo yao mwisho wa siku kuwaingiza motoni wafuasi wao.

Wanaweza kuja kwa staili kuwa tunataka huyu Kiti aswali SWALA tano,asiwe mlevi yaani wanataka awe mtu wa Ibada na ajiepushe na Maovu kisha baadae wanamzimisha katika JANGA KUBWA LA SHIRK.

Hii mbinu Baba yao Iblis ndio muasisi mkubwa...

Al araaf:21

فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَـٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ ﴿٢٠﴾
"Basi shaytwaan (naye ni Ibliys) akawatia wasiwasi ili awafichulie yaliyofichwa kwao ya sehemu zao za siri. Na akasema: “Rabb wenu Hakukukatazeni huu mti isipokuwa msijekuwa Malaika wawili au kuwa miongoni mwa wenye kudumu milele.”



وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ﴿٢١﴾

"Naye akawaapia: “Hakika mimi kwenu nyinyi wawili ni mwenye kukunasihini kidhati.”

Haya tufanye kweli wanamwomba Allah kama wanavyodai JE HII NI NJIA SAHIHI YA KUMUOMBA ALLAH????

Mtume swalla llahu alayhi wasallam ametufundisha kuomba Dua kwa namna hii??

Je ni swahaba gani aliwahi kuomba Dua kwa kupitia Baraka za Ahlu Badr(atakayenitajiwa Swahaba mmoja tu aliyefanya haya NITAMPA MILION MOJA TASLIM)

Haifai kuomba Dua kwa kupitia Baraka za Watu hata Mitume hata kitu chochote.

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

" Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah."

Na kusema kuwa watu hawaombi wale Maswahaba bali anaombwa Allah ila wale kule kuwataja ni kutaka Baraka zao tu kujikurubisha kwa Allah huu ni USHIRIKINA(Shirq) maana huna tofauti na wale waabudu MASANAMU....Hebu wasikie mwenyewe hapa wanavyosema

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٦١﴾

61. Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Basi vipi wanavyoghilibiwa?



HAPA WANAUA KABISA.....

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١٨﴾

"Na wanaabudu pasi na Allaah ambavyo haviwadhuru wala haviwanufaishi na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” Sema: “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini? Subhaanah! Utakasifu ni Wake Na Ametukuka kwa ‘Uluwa kwa yale yote wanayomshirikisha"

Sasa hapa tofauti ipo wapi na wale waabudu MASANAMU???!!!!!!

ALLAH anasemaje juu ya yeye kuombwa....????

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖأُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖفَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦

"Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka"


Watu wanapaswa kuomba kwa kupitia majina ya Allah na Amali njema walizofanya.

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖوَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚسَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٨٠﴾
"Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanamili katika kukadhibisha Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda."

Halafu jiulize Dua gani inaambatana na mambo ya Sindano,wembe na Ndimu????
Kama waislam tungekuwa tunaomba Dua kwa Wembe na Ndimu msikitini si kungejaa ndimu na Wembe au tungekuwa tunaenda nayo????!

Hapa kuna kitu NYUMA YA PAZIA???
Na si kingine ni haya mambo ya uchawi kama tulivyoyabainisha huko nyuma.

NASAHA ZANGU

Waislam wajiweke mbali na hayo mambo ya sheikh yaliyopewa jina la dua na muislam hupaswi hata kufurahia kwa moyoni wanaofanya haya tuwe na msimamo wa nabii Ibrahim

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَآؤُاْ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖرَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ﴿٤﴾

4. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni, na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha abadi mpaka mumuamini Allaah Pekee.” Isipokuwa kauli ya Ibraahiym kwa baba yake: “Nitakuombea maghfirah, na wala sikumilikii chochote kile mbele ya Allaah. Rabb wetu! Tumetawakali Kwako, na Kwako Tunarudia kutubia, na Kwako ni mahali pa kuishia.
 
Huu uzi ukichangiwa hadi page 10 itakuwa ajabu....maana ukweli umejificha ndani ya maandishi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom