Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Napenda kuwaleza mapema juu ya utabiri wangu huu ili yakianza kutokea msishangae na pengine kufadhaika bali mjipange kuyapokea yatayotokea.
Katika kutekeleza makakati/mpango huo,wanaoweza kuwa wanasiasa wa mwanzo kushawishiwa kukubali teuzi hizo ni watu/wanasiasa kama Prof.Jay, Sugu, Msigwa na wengineo ambao wanaweza kupewa vyeo kama U-RC, U-DC,U-RAS n.k.
Watu kama Lema na Mdee itakuwa vigumu kuwashawishi ingawa nao wanaweza kufuatwa kwa lengo hilo hilo la kuwataka wakubali teuzi.
Huu kwao utakuwa ni mtihani kwani kwa sasa hawana ubunge na pia hiki kitakuwa kipimo cha wao kusimama na vyama vyao na zaidi kusimamia msimamo wao kuwa Uchaguzi hakuwa halali(haukuwa huru na wa haki) kwani kukubali uteuzi maana yake umekubali kuwa aliekuteua alishinda kihalali na hivyo unakubali kuwa uchaguzi ilikuwa huru na wa haki.
Mbowe, Lissu na Zitto wanaweza kuwa treated tofauti ili kurudisha Umoja wa Kitaifa kwa lengo la kutuliza kama sio kumaliza kabisa kelele za nchi wahisani juu ya uchaguzi huu ambapo hata kesi zinazowakabili zitafutwa.
Mbowe na Lissu kupewa teuzi hizo sio rahisi kwani ni vigumu kwa wao kukubali hizo nafasi(hata wakipewa ubalozi bado watakataa) labda zitto ingawa hata nae sio rahisi kukubali.
Kuhusu Zitto,kama chama kitamruhusu Maalim Seif na yeye mwenyewe akakubali kuwa makamu wa Rais huko Zanzibar, basi tunaweza pia kufikiria uwezekano wa Zitto kupewa ubalozi ila ajue tu kama ikitokea hivyo na yeye akakubali, huo ndio utakuwa mwanzo wa yeye na chama chake kujimaliza kisiasa.
Malengo yatakuwa ni matatu: kupoza wahisani, kujaribu kurudisha Umoja wa Kitaifa na kupoza hasira au machungu ya dhuluma za Uchaguzi na tatu ni kuendeleza mkakati wa kudhoofisha upinzani kwa wataokubali uteuzi.
Tunaingia katika awamu nyingine ngumu zaidi kwa upinzani na silaha pekee ya kushinda vita hii ni kuzishinda kwanza njaa zetu maana njaa kila mtu anayo ingawa kila mtu na kiwango chake.
Hard times for opposition is not yet over.
Time will tell.