Maoni yangu uchaguzi 2025: CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vilekeze nguvu viti vingi vya ubunge walenge Spika umilki wa Bunge

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
992
1,155
Wakuu mtazamo wangu ni kuona tunakuwa na vyama vyenye nguvu Zinazolingana au kukaribiana sana
Ili ikitokea chama kimoja kikizingua inakuwa rahisi wanachi kukiondoa na kuweka kingine

Mwisho wa siku tunakuwa na ushindani wa hoja zenye kuleta maendeleo makubwa Kwa wananchi
Lakini pia tutaongeza uwajibikaji kwa chama tawala na viongozi wao kuwa na hofu Kwa wananchi wao ambao ndio waajiri wao

Wakuu najua lengo la Cdm no katiba mpya ,

Nashauri hili liwe lengo la muda mrefu waendelee kudai ila napendekeza mikakati ifuatayo

Maana Kwa muda mfupi uliobakia sioni kama Kuna muda wa kutosha kuleta katiba Bora

Mchakato unahitaji muda kidogo

Naona wajielekeze

1. Kupata tume huru ya uchaguzi
hata kama itashindikana bado nashauri wasisusie uchaguzi angalau kuna mazingira mazuri kidogo na tulikotoka

2.Kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na Kisha kushiriki bila kususa bila kujali mazingira yaliyopo

3. kujiandaa na uchaguzi mkuu Kwa kulenga nafasi nyingi za ubunge , zitakazowawezesha
A.kuchukua nafasi ya spika ya bunge na hivyo kuchukua mamlaka ya bunge
B. Itawawezesha kuchukua nafasi ya waziri mkuu hivyo itapelekea kuundwa serikali ya mseto
C.Itawawezesha kutunga Sheria nyingi zenye maslahi Kwa taifa
Ikiwemo sheria ya mchakato wa kupata katiba mpya
D. Watapata nafasi ya kujiandaa kuunda serikali kamili 2030 kama watashinda uchaguzi mkuu

4. Waweke nguvu kupata nafasi nyingi za madiwani Ili kukamata halmashauri
Ili kuonyesha wananchi mbadala was maendeleo wanayoyataka

Mwisho nashauri umoja wa vyama vya upinzani ni muhimu bila kujali ukubwa au udogo wa chama
 
Mkuu kwa katiba na tume hii ni kupoteza muda kwenda kupiga kura. Kwa ujumla hakuna uchaguzi Tanzania, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ni mtu mjinga tu ataweza kupoteza muda wake kwenda kupiga kura kwa mazingira haya. Ni aidha kutokee machafuko tuanze upya, au mapinduzi ya kijeshi. Hizo nyingine ni porojo tu za kufarahisha genge.
 
Mkuu naheshimu mawazo yako
Isipokuwa unaonyesha dalili mbaya sana ya kukata tamaa ,
Kitu ambacho ni kibaya sana

Unapofika mahali pa kuamini mpaka machafuko au mapinduzi ya kijeshi ndo mabadiliko ya kisiasa yatokee badala nguvu ya hoja unakuwa umetoka kwenye mrengo wa demokrasia na siasa za vyama vingi na

kuwa kikundi Cha kihuni au Cha kigaidi au kundi la waasi,
Hiki ni kitu ambacho hatuombei Wala hakipaswi kutokea kwenye nchi yetu

Kwa sasa bado naamini mazingira yanazidi kuboreka tangu kuondoka kwa awamu iliyopita, ila tusitegemee Chama tawala kukuwekea mazingira marahisi ili ufunge kirahisi noo,
Kilichopo ni kutumia fursa hata kidogo inayopatikana bila kuipoteza
Mfano kipindi Cha ukoloni baba wa taifa waliweza kushiriki uchaguzi kwenye Yale mazingira ya ukoloni na kujinyakulia viti vingi licha ya mazingira ya ukoloni
Na hii ilimpa nguvu zaidi katika harakati za kupata mamlaka kamili
Hivyo naamini bado unayo nafasi ya kufanya vizuri

Nikuombe uachane na hizo fikra mkuu
 
Kwanza sijakata tamaa, bali numepuuza zoezi zima liitwalo uchaguzi. Ni mtu mjinga tu ataendelea kushiriki uchaguzi kwa tume na katiba hii. Tunachofanya sasa ni kuhakikisha zoezi zima linakosa uhalali wa umma hata kama litafanyika kisheria. Hapo itawezekana kushawishi watu kutafuta viongozi kwa njia mbadala, nayo ni hiyo ya machafuko, au mapinduzi.

Somo sahihi lilishapatikana hapo Kenya baada ya machafuko. Lakini kuendelea kushiriki uchaguzi unaochezewa kila mara, kisha baada ya uchaguzi vyama vinakutana kufanya muafaka fake haiingii akilini. Zoezi la kuhakikisha watu wanapuuza zoezi la uchaguzi linaendelea vizuri, kwani kwa sasa wapiga kura wanazidi kupungua kwa kasi ya kufurahisha. Vyama vinaweza kushiriki hizo chaguzi za kihuni, lakini sio wapiga kura.
 
Wakuu mtazamo wangu ni kuona tunakuwa na vyama vyenye nguvu Zinazolingana au kukaribiana sana
Ili ikitokea chama kimoja kikizingua inakuwa rahisi wanachi kukiondoa na kuweka kingine
Mwisho wa siku tunakuwa na ushindani wa hoja zenye kuleta maendeleo makubwa Kwa wananchi
Lakini pia tutaongeza uwajibikaji kwa chama tawala na viongozi wao kuwa na hofu Kwa wananchi wao ambao ndio waajiri wao
Wakuu najua lengo la Cdm no katiba mpya ,
Nashauri hili liwe lengo la muda mrefu waendelee kudai ila napendekeza mikakati ifuatayo
Maana Kwa muda mfupi uliobakia sioni kama Kuna muda wa kutosha kuleta katiba Bora
Mchakato unahitaji muda kidogo

Naona wajielekeze
1. Kupata tume huru ya uchaguzi
hata kama itashindikana bado nashauri wasisusie uchaguzi angalau kuna mazingira mazuri kidogo na tulikotoka
2.Kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na Kisha kushiriki bila kususa bila kujali mazingira yaliyopo
3. kujiandaa na uchaguzi mkuu Kwa kulenga nafasi nyingi za ubunge , zitakazowawezesha
A.kuchukua nafasi ya spika ya bunge na hivyo kuchukua mamlaka ya bunge
B. Itawawezesha kuchukua nafasi ya waziri mkuu hivyo itapelekea kuundwa serikali ya mseto
C.Itawawezesha kutunga Sheria nyingi zenye maslahi Kwa taifa
Ikiwemo sheria ya mchakato wa kupata katiba mpya
D. Watapata nafasi ya kujiandaa kuunda serikali kamili 2030 kama watashinda uchaguzi mkuu

4. Waweke nguvu kupata nafasi nyingi za madiwani Ili kukamata halmashauri
Ili kuonyesha wananchi mbadala was maendeleo wanayoyataka

Mwisho nashauri umoja wa vyama vya upinzani ni muhimu bila kujali ukubwa au udogo wa chama
Zaidi ya CCM hakuna chama chochote kilichowahi kuweka wagombea ubunge katika majimbo ya uchaguzi kwenye uchaguzi wowote wa vyama vingi. Sasa huo uwezo wa kuwa na Spika na PM wanautoa wapi?
 
Hujaeleweka vizuri mkuu
Kila uchaguzi chadema inaweka wagombea kwenye majimbo ya uchaguzi Kwa asilimia kubwa

Lakini kama unamanisha hukuna chama Cha upinzani kilichoweka wanachama kwenye majimbo yote ya uchafuzi ni sawa
Ndo maana nikashauri waanze kuweka nguvu kwenye ub unge tu
Waachane kupoteza muda kwenye nafasi ya urais kwa sasa
Pili washirikiane na vyama vingine kuwaachia baadhi ya majimbo yenye nguvu
 
Tupo pamoja. Ila sidhani kama hilo wanaliweza.
 
Mkuu naheshimu mawazo yako
Isipokuwa unaonyesha dalili mbaya sana ya kukata tamaa ,
Kitu ambacho ni kibaya sana

Unapofika mahali pa kuamini mpaka machafuko au mapinduzi ya kijeshi ndo mabadiliko ya kisiasa yatokee badala nguvu ya hoja unakuwa umetoka kwenye mrengo wa demokrasia na siasa za vyama vingi na

kuwa kikundi Cha kihuni au Cha kigaidi au kundi la waasi,
Hiki ni kitu ambacho hatuombei Wala hakipaswi kutokea kwenye nchi yetu

Kwa sasa bado naamini mazingira yanazidi kuboreka tangu kuondoka kwa awamu iliyopita, ila tusitegemee Chama tawala kukuwekea mazingira marahisi ili ufunge kirahisi noo,
Kilichopo ni kutumia fursa hata kidogo inayopatikana bila kuipoteza
Mfano kipindi Cha ukoloni baba wa taifa waliweza kushiriki uchaguzi kwenye Yale mazingira ya ukoloni na kujinyakulia viti vingi licha ya mazingira ya ukoloni
Na hii ilimpa nguvu zaidi katika harakati za kupata mamlaka kamili
Hivyo naamini bado unayo nafasi ya kufanya vizuri

Nikuombe uachane na hizo fikra mkuu
Marekani na Ufaransa ni mataifa ya kidemokrasia ? Ndio au Hapana.
 
Naona wajielekeze
1. Kupata tume huru ya uchaguzi
hata kama itashindikana bado nashauri wasisusie uchaguzi angalau kuna mazingira mazuri kidogo na tulikotoka
2.Kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na Kisha kushiriki bila kususa bila kujali mazingira yaliyopo
4. Waweke nguvu kupata nafasi nyingi za madiwani Ili kukamata halmashauri
Ili kuonyesha wananchi mbadala was maendeleo wanayoyataka

Mwisho nashauri umoja wa vyama vya upinzani ni muhimu bila kujali ukubwa au udogo wa chama
Naunga mkono hoja
P
 
Wakuu mtazamo wangu ni kuona tunakuwa na vyama vyenye nguvu Zinazolingana au kukaribiana sana
Ili ikitokea chama kimoja kikizingua inakuwa rahisi wanachi kukiondoa na kuweka kingine
Mwisho wa siku tunakuwa na ushindani wa hoja zenye kuleta maendeleo makubwa Kwa wananchi
Lakini pia tutaongeza uwajibikaji kwa chama tawala na viongozi wao kuwa na hofu Kwa wananchi wao ambao ndio waajiri wao
Wakuu najua lengo la Cdm no katiba mpya ,
Nashauri hili liwe lengo la muda mrefu waendelee kudai ila napendekeza mikakati ifuatayo
Maana Kwa muda mfupi uliobakia sioni kama Kuna muda wa kutosha kuleta katiba Bora
Mchakato unahitaji muda kidogo

Naona wajielekeze
1. Kupata tume huru ya uchaguzi
hata kama itashindikana bado nashauri wasisusie uchaguzi angalau kuna mazingira mazuri kidogo na tulikotoka
2.Kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na Kisha kushiriki bila kususa bila kujali mazingira yaliyopo
3. kujiandaa na uchaguzi mkuu Kwa kulenga nafasi nyingi za ubunge , zitakazowawezesha
A.kuchukua nafasi ya spika ya bunge na hivyo kuchukua mamlaka ya bunge
B. Itawawezesha kuchukua nafasi ya waziri mkuu hivyo itapelekea kuundwa serikali ya mseto
C.Itawawezesha kutunga Sheria nyingi zenye maslahi Kwa taifa
Ikiwemo sheria ya mchakato wa kupata katiba mpya
D. Watapata nafasi ya kujiandaa kuunda serikali kamili 2030 kama watashinda uchaguzi mkuu

4. Waweke nguvu kupata nafasi nyingi za madiwani Ili kukamata halmashauri
Ili kuonyesha wananchi mbadala was maendeleo wanayoyataka

Mwisho nashauri umoja wa vyama vya upinzani ni muhimu bila kujali ukubwa au udogo wa chama
Ushauri mzuri Sasa kazi kwao
 
Chadema wakijidanganya susia uchaguzi ndo inakula kwao. Waanze Serikali za Mitaa Mwakani, matokeo ndio yatakuwa matokeo ya 2025
 
[QUOTE="Cannabis, post: 45053486, member: 201681"] Mkuu Pasco unaunga mkono hoja inayolenga kufanya chama chetu kipoteze majimbo ? unataka tuchanganye magunzi na betri unafikiri kurunzi litawaka ?😡 [/QUOTE] Mkuu Kila jambo lina mwanzo wake , Kuliko kuweka malengo makubwa Kila mwaka yasiyofikika ni Bora kuweka malengo madogo yanatimizika kudlekea malengo makubwa Hii dhana ya kuona vyama vingine kama magunzi ni dhana ya kibaguzi ambayo inazidi kuua vyama vya upinzani, huko Dunia ya kwanza vyama vinaungana kuunda serikali ya mseto na wanamaendeleo makubwa Leo utasikia Republic imekamata udhibiti wa bunge while government ni ya Democrats Hivyo Kila chama kinakuwa makini kutumikia wananchi Tuachane na dhana za kibinafsi na kibaguzi
 
Mkuu Pasco unaunga mkono hoja inayolenga kufanya chama chetu kipoteze majimbo ? unataka tuchanganye magunzi na betri unafikiri kurunzi litawaka ?😡
Vyama vya upinzani vipo kisheria, ili nchi yetu uende vizuri, inahitaji upinzani imara, ndani ya wapinzani kuna baadhi ya watu wazuri kama Zitto, Lissu, JJ Mnyika, Mbowe, wanahitajika wawepo Bungeni kulisaidia taifa. Hivyo it's healthy kwa chama chetu kuwaachia wapinzani baadhi ya majimbo!.
Ndio maana nilishauri https://www.jamiiforums.com/threads...a-na-kambi-rasmi-ya-upinzani-bungeni.1807591/
P
 
Hujaeleweka vizuri mkuu
Kila uchaguzi chadema inaweka wagombea kwenye majimbo ya uchaguzi Kwa asilimia kubwa

Lakini kama unamanisha hukuna chama Cha upinzani kilichoweka wanachama kwenye majimbo yote ya uchafuzi ni sawa
Ndo maana nikashauri waanze kuweka nguvu kwenye ub unge tu
Waachane kupoteza muda kwenye nafasi ya urais kwa sasa
Pili washirikiane na vyama vingine kuwaachia baadhi ya majimbo yenye nguvu

..wakiweza kuweka wagombea ubunge Tanganyika yote kwanini washindwe kuwa na mgombea Uraisi?
 
Mkuu kwa katiba na tume hii ni kupoteza muda kwenda kupiga kura. Kwa ujumla hakuna uchaguzi Tanzania, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ni mtu mjinga tu ataweza kupoteza muda wake kwenda kupiga kura kwa mazingira haya. Ni aidha kutokee machafuko tuanze upya, au mapinduzi ya kijeshi. Hizo nyingine ni porojo tu za kufarahisha genge.
Mzee kwan Magufuli si kashaondoka ambae akiiba kura? Vip tena unaanza kusema hivi wakati mbaya wenu hayupo?
 
Jeuri yote ya Magufuli kunajisi uchaguzi aliipata kupitia udhaifu wa katiba hii hii. Ameshatengeneza bad presidence, sioni kiongozi mwingine wa CCM akiacha kutumia mbinu hiyo hiyo.
 
Mkuu kwa katiba na tume hii ni kupoteza muda kwenda kupiga kura. Kwa ujumla hakuna uchaguzi Tanzania, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ni mtu mjinga tu ataweza kupoteza muda wake kwenda kupiga kura kwa mazingira haya. Ni aidha kutokee machafuko tuanze upya, au mapinduzi ya kijeshi. Hizo nyingine ni porojo tu za kufarahisha genge.
Loading........
 
Jeuri yote ya Magufuli kunajisi uchaguzi aliipata kupitia udhaifu wa katiba hii hii. Ameshatengeneza bad presidence, sioni kiongozi mwingine wa CCM akiacha kutumia mbinu hiyo hiyo.
Dkt Slaa kwenye kitabu chake cha nyuma ya Pazia anaelezea pia juu ya uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo kwa mujibu wake vyanzo vyake vya habar zikiwemo taasisi nyeti zilimpenyezea habari kuwa kulikuwa na makontena ya kura Feki yakiingizwa kupitia Tunduma.

Inakuaje malalamiko yenu yanasahau chaguzi zote juu ya kuibiwa kwa uchaguzi ila mnajikita tu katika uchaguzi wa 2020?

2. Ni Uchaguzi gani kati ya mwaka 2015 na mwaka 2020 ambao ulikuwa u atoa matumaini kwenu wa kushinda ata mkiwa katika kipindi cha kampeni?

3. Ikiwa unaamini kuwa M/K alifanya makosa kumpokea Edwad Lowasa mwaka 2015 na kumpa nafasi ya ugombea, kwanini usihisi makosa hayohayo ndiyo yalipelekea mpate kura chache zaidi mwaka 2020 maana wanaanchi walishakuwa na mashakha nanyinyi?

4. Mwaka 2005 Mh Mbowe aligombea kiti cha urais na akaambulia kura laki 5+, mwaka 2010 Dkt Slaa aligombea akaambulia kura milion 2+, mwaka 2015 Edward Lowasa aligombea akapata kura milion 6+, mwaka 2020 Lissu anagombea anapata kura million 1.9! Tukimtoa Lowasa ambae alikuwa na ushawishi binafsi na kundi lake, Je! Unaamini Lissu angeweza kufikisha kura million 8? Kama ndiyo ni yupi kati ya ao wagombea wachadema alikuwa na ushawishi zaidi kwa wananchi? Ni Lissu?
 
Back
Top Bottom