Swala la mapenzi kwa kweli hayana mpaka na siwezi kujibu kwa niaba ya wanawake wote. Nahisi wanawake wanaopenda wanaume ambao wapo ndani ya ndoa wanavutwa na ile stability ya mume. sio boyfriend wa kawaida, ni mtu focused, ana mtazamo na mipango ya maisha etc, so he is more "mature".
Swala la tegemeo pia sijui. Kuna ambao wanategemea atamuacha nyumba kubwa aje kwake (wengi) na wengine wanategemea tu kwamba atampa starehe ya mali na mwili ila ataweza kubaki independant kwa mambo mengine.
Ni kweli mwanaume anacheat na mwanamke ila tukumbuke mwanamke huyo wa nje hana ndoa, hivo kosa lake ni kujikosea heshima mwenyewe, ila mwanaume not only anajikosea heshima ila pia anamkosea heshima mke wake wa ndani, anamkosea heshima huyo mke wa nje, na anawakosea heshima watu wokte walio hudhuria kwenye ndoa yake. Na mwisho kabisa (na ndio worse) anamkosea Mungu.
RR thanx kwa kutoa mtazamo wako, ila napenda tuangalie pia reason ya mwanaume kuamua kutoka nje ndoa yake na kuwa na kambi kabisa/nyumba ndogo.
Je ni tamaa tu?
Je wake wa ndoa mnatimiza wajibu wenu ipasavyo?
Mana mm nachekecha mambo pande zote na hapa tukiangalia idadi ya wanaume kutoka nje wengi watakupa sababu kuwa wake zao wamewafanya wao kutoka nje.
Nieleweke kwamba SITETEI huu UOVU ila nataka tuangalie wapi ndio tunapokosea ili tukirekebisha hapo hili tatizo lipungue.
Nakupa mfano huu hai
Anko wangu b4 hajaoa mwanamke alikua mpole sana,mnyenyekevu mwenye huruma,mkarimu mno, msafi kuanzia mwili mpaka nyumba, alionekana na sifa zote nzuri zilizomfanya anko aharakishe mchakato wa kumuoa.
Miezi michache baada ya ndoa mke akabadilika
akawa mjeuri,ule upendo haukuwepo tena,hakujaijali nyumba kwa ujumala,akaanza kuwa mchafu, hafui,hasafishi chumba,hampikii mumewe vizuri kama awali, kutwa ni ugomvi kudai mambo makubwa, zaidi ya yote hatulii nyumba kutwa kuzurura tu.
Familia,wazaz wamemkanya na hataki kubadilika.
Je kwa hili hii huyu Anko wangu akipata wazo la kuwa na bibi nje atakae m care,kumpikia akitakacho,mkumjali nk tutamlaumu?kumbuka nae ni binadamu ana hisia mfano furaha, maudhi,huzuni nk
Je wakati ule huyu mke wa ndoa alipoonyesha kuwa na tabia njema zote je alikua akiigiza tu a WIN suala la kuolewa?
Wanawake wengi b4 hamjaolewa mnafanya maigizo ya kila namna ili kumvutia mume akuoe.
Baada ya hapo mnaanza kuonyesha makucha halisi.
Mnasahau kuwa kuolewa si kazi, kazi ku maintain ndoa.
Napenda tena kupata maoni yako kutokana na hayo niliyo eleza then tuangalie wapi tunarekebisha ili kupunguza haya matatizo.