Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo)

Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo)

Akiwa mke wa mtu huyo ni hawara.... Take note: Kuna infidelity na nyumba ndogo... Nyumba ndogo ina epukika... Infidelity in most cases ni inevitable....
Huo ni mtazamo wako dada yangu ila mimi bado nasisitiza kua infidelity is not a must. Mtu unauwezo wakuchagua at any time na sababu Mungu anasema hato mruhusu shetani atujaribie kuliko nguvu zetu naamini kabisa kua tunaweza kushinda temptation ya kwenda nje ya ndoa na in fact kuna watu wanaweza!
 
Siku kadhaa zilizo pita kuna member alitoa post kuhusu utaratibu wa ku-manage nyumba ndogo ili asi lete utata. Member huyo anaitwa The Boss.
Pamoja na kumshukuru kwa kutoa maoni na shauri zake kuhusu Nyumba ndogo, mimi kama mwanamke nimeona siwezi kujibu kwenye post lile ila nifungue tu thread mpya sababu mtazamo wangu na wake ni tofauti kabisa.
  1. Kwanza namlaumu kwa kutoa thread kama hiyo sababu ina halalisha kitu kilicho haram. nikijieleza kwa mfano, ni kama kusema inakatazwa kuua mtu ila kama utaamua kumchinja kumbuka kutoa carpet usilijaze damu. Mtasema hana influence ya kuhalalisha au kuharamisha kitu, na ni kweli, ila yeye ndie alitoa mwelekeo wa thread na kila alie changia kwa kumsupport (na kila alie “like” thread yake) ameongeza sauti lake kwenye mada na hivo msomaji wa kawaida (mimi na wewe) tunahisi kuna watu wengi sana wanamtazamo huo. Kwa mtu alie kua na nia ya kwenda nje, au Yule tayari anatembea nje ya ndoa, ni ruhsa tosha ya kuendelea katika njia hiyo.
  2. Pili, kama ikitokea mtu aanguke na atoke nje ya ndoa, shauri la kumpa sio namna gani aifanya hali hiyo iwe shwari na idumu, bali nikumshauri namna gani anaweza kujitoa katika mtego huo. maada ya thread hii sio kutoa huo ushauri, labda nitarudi baadae.
  3. La tatu na lililo nikwaza zaidi ni heshima ndogo ya utaratibu mzima kwa wanawake, iwe nyumba kubwa au nyumba ndogo. Kwa namna nilisoma thread (kama nilikosea naomba anikosoe) kila kitu kina husisha kugawa hela kati ya nyumba kubwa na nyumba ndogo (material distribution) na heshima/mtazamo wa ndugu na rafiki. sikuona katika thread hiyo mapenzi yanawekwa wapi, heshima ya muhusika kwa nyumba kubwa, au nyumba ndogo, watoto, tegemeo za watu wengine na kadhalika vikija katika hesabu.
Katika dunia ya JF, ni sawa kuanzisha thread kama hiyo ila dunia ya kweli ambayo ninaishi mimi, na wengine wengi, hivyo vitu vipo. Mtu anaheshima yake na akienda kwa nyumba ndogo conscience yake inamsumbua. kuna mapenzi kati ya yeye na nyumba kubwa, au kati ya yeye na nyumba ndogo, au yuko in transition, akitoa mapenzi kwa bimkubwa kwenda kwa nyumba ndogo(or whatever the case). Pia wanawake hao ni binadamu na wana akili, tumaini, na hisia zote za kawaida. wanapiga hesabu za maisha na kusema kesho nataka mimi na mpenzi wangu tuwe hivi, na hivi, na hivi. na wanatumia njia mbali mbali za kumshawishi mwanaume afate hizo njia.
Kwa kumalizia nataka kukumbusha kama kila mtu ana mtazamo wake wa haya mambo na nina heshimu mtazamo wa kila mtu. Huu hapa ni mtazamo wangu na naomba uheshimiwe pia. Sijakataza kutoa maoni yenye kupinga mtazamo, nimeomba tu tuchangie kwa heshima.
Asanteni.

hata sijui nianzie wapi....but subirini nakuja.....
 
Some men have thousands of
reasons why they cannot do what
they want to; all they need is one
reason why they can.
And a thread like that has just given them one....
 
Yaani sasa hapa ndio umenichanganya kabisaaaaaa..Kwa hiyo mke wa mtu kumegwa na mume wa mtu RUKHSA. Ila mume wa mtu kuwa na mwanamke ambae hajaolewa hairuhusiwi kwa kuwa atakuwa nyumba ndogo?

Mbona sielewi! ??
Got confused!!!
 
Shem bana....... you think hatujui? Tunajua sana mna vidumu na mko smart sana mnapoamua kucheat........ uzuri wetu ni kuwa tunafahamu lakini we dont bother kwakuwa hata tufanyeje "binadamu hachungwi".......... My wife will remain innocent mpaka ntakapomfumania, na yeye anapaswa kuwa na imani hiyo. Vinginevyo dunia hii haitokalika.

dah unamenitisha mkuu, so niendelee kuwa bachela tu!kwa kweli haya mambo yanachanganya.
 
hata sijui nianzie wapi....but subirini nakuja.....
I said the same thing when I first saw your post, and I decided to start from a new angle all together. but it would be interesting to see what you think of what I said.
 
We uje kukonkludi tu, kazi tumeshamaliza na kimeeleweka!
Hakuna kilichoeleweka. Umesema sana ila msimamo wako ni kwamba wanaume karibu wote wanacheat so it is ok to cheat. Na mimi nimesema kuchukulia watu wote wanacheat kama msingi wa kutoa ushauri on how to do it effectively ni kuhalalisha kilicho haram.
Kama una point contrary to that, I am yet to read it!
 
dah unamenitisha mkuu, so niendelee kuwa bachela tu!kwa kweli haya mambo yanachanganya.
Wanataka ufikirie kua mwanaume wote anacheat, na mwanamke wote anacheat, ili tabia ikigundulika au picha ikitoka ionekane it is not so bad because we all do it. the fact is it is bad and we DON'T all do it, we don't all agree with it and it is something we can live and we should live without!
 
With these parting words,

‘al jununi fununi alwakh khalfan wakheed'

I say so long amigos.
 
The boss alitoa guide nzuri,
kwani kila mtu ana haki ya kuchagua namna ya kuishi mfano ,kutokuoa/kutokuolewa,kuoa mke mmoja au wawili,nk
so nyumba kubwa au ndogo yote ni sawa kwa mmiliki sema mmoja alimtangulia mwenzie tu,
ila swala kwamba nani mwenye nafasi zaid hilo ni swala mmiliki tena...
Narudi
 
Akiwa mke wa mtu huyo ni hawara.... Take note: Kuna infidelity na nyumba ndogo... Nyumba ndogo ina epukika... Infidelity in most cases ni inevitable....

Taking notes:

Mke wa Mtu = Hawara

Sio Mke wa Mtu = Nyumba Ndogo...

Naomba mnijulishe kipindi (duration of relationship) ambapo mtu ana-qualify kuitwa small house, medium house, big house au concubine..
 
Nilisahau kidogo, hivi Nyani Ngabu umeoa? Maana kama umeoa na % ya wanawake wanao cheat ni hiyo kuna uwezekano mkubwa wa mkeo kuwa kwenye kundi hilo, na kwa kulijua hilo umechukua hatua gani? Kama hujaoa kwa mtazamo huo utaoa kweli!?
 
Back
Top Bottom