@Aspin mi naanza kama hivi:
jina langu ni
Idd Ninga au ukipenda waweza kuniita
NINGA nimezaliwa Tanzania mwaka 1989.
Napenda kuuliza maswali na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa watu mbalimbali.
Ninatumia
ID YA UKWELI hali inayonifanya kuwa muoga katika kucomment mada katika majukwaa ya
SIASA na HABARI MCHANGANYIKO Hiyo yote ni katika hali ya kuwa salama zaidi.
Sijaoa mpaka sasa kwa kuwa nipo najiendeleza kielimu ingawa niliishia darasa la saba lakini namshukuru mungu aliweza kunipa maarifa mengine na uwezo wa kuzungumza lugha 3 ambazo ni
KISWAHILI,KINGEREZA na KIISPANIA lugha ninazozipenda.
Nina fani katika mambo ya utalii.
Kipaji changu ni sanaa ya utengenezaji filamu ikiwemo film editing and acting pamoja uandishi wa mashairi na mara nyingi huwa naandika mashairi katika gazeti la
MWANANCHI Kila ijumaa.
Malengo yangu ni kufungua kampuni yangu au kujiajiri na ninachukia sana kuajiriwa.
Napenda watu watu wapole,wenye busara,hekima na watu ambao wanaweza kunishauri na kunifunza mambo mbalimbali.
Napenda kukosolewa na kuonyeshwa njia sahihi ya mimi kufanya ili nifanye vizuri.
Sipendi sana kujihusisha na mambo ya mapenzi ya wakati huu ingawa na mpenzi wangu anaeanziwa na herufi
V nampenda sana kwani anaonekana kuwa ni mvumilivu.
Nawapenda wote wa
Jf kwani wamekuwa wakinipa changamoto na kujifunza mambo mbalimbali.
Napenda kukutana na member wote wa Jf kama:
mshana jr
Rakims
Mzizi mkavu
miss chagga
na wengine wengi.
Napenda kusema tena "
USIOGOPE KUNIKOSOA NA KUNISHAURI NA MAMBO NINAYOKOSEA "
nakaribisha mashwali na ushauri.