Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,401
Haya tena wadau wa JF.
Ndio tunaumaliza mwaka 2013 na tunaukaribisha mwaka 2014.
Kama mnakumbuka January 2013 tulifanya White Party pale Kebby's Hotel Mwenge ambapo ilifana sana.
Kwa mara nyingine tena tunaandaa Party nyingine ambayo itafanyika tarehe 25 January 2014 katika ukumbi utakaotangazwa kadiri muda unavyojongea kwa sababu bado tunao muda wa kutosha.
Kamati ya maandalizi inaundwa na wana JF wafuatao:
1. Paloma
2. Mtambuzi
3. gfsonwin
4. Madame B
5. Vin Diesel
6. jouneGwalu
7. Jiwe Linaloishi
8. cacico
9. lara 1
10 ladyfurahia
11. Kipaji Halisi
Siyo lazima kamati hii ikutane bali wajumbe wa kamati hii watakuwa wakiwasiliana kwa simu au kwa PM au hata kwa kuweka mapendekezo yao katika huu uzi kw aajili ya kufanikisha hafla hii muhimu kwetu.
Hapa chini nitaweka mchanganua wa bajeti inayohitajika ili kufanikisha hafla hii:
Cocktail Menu kwa makadirio ya watu 40 watakaohudhuria
Mahitaji | Idadi | Gharama | Jumla |
Ukumbi | 1 | 0 | 0 |
Bites | Kwa watu 40 | @15,000/= | 600,000/= |
Vinywaji | Kwa watu 40 | Beer 4 @3,000/= | 480,000/= |
Mziki | 1 | @150,000/= | 150,000/= |
Corkage kwa vinywaji vikali | Chupa 5 | @15,000/= | 75,000/= |
Jumla | 1,305,000/= |
Kwa hiyo kwa makadirio ya bajeti hiyo kila mdau anatakiwa kuchanga kiasi cha shilingi 35,000/=
Au
Dinner Menu kwa makadirio ya watu 40 watakaohudhuria
Mahitaji | Idadi | Gharama | Jumla |
Ukumbi | 1 | 0 | 0 |
Dinner | Kwa watu 40 | @20,000/= | 800,000/= |
Vinywaji | Kwa watu 40 | Beer 4 @3,000/= | 480,000/= |
Mziki | 1 | @150,000/= | 150,000/= |
Corkage kwa vinywaji vikali | Chupa 5 | @15,000/= | 75,000/= |
Jumla | 1,505,000/= |
Kwa hiyo kwa makadirio ya bajeti hiyo kila mdau anatakiwa kuchanga kiasi cha shilingi 40,000/=
*Mimi Mzee Mtambuzi nitajitolea chupa tano za vinywaji vikali ambvyo ndivyo vitakachochajiwa Corkage ili viingizwe ukumbini. Hapa nazungumzia vinywaji kama Contesa, Strawberry Lips, Govinder Kumar, Vodka, Jack Daniel, n.k.
Bajeti hii nimeikadiria kwa kuangalia gharama za hoteli zinazofanana na Hoteli ya Kebby's mahali tulipofanya White Party January 2013, kwa hiyo zinaweza kupungua au kupanda kulingana na idadi ya wadau watakaohudhuria au hoteli tutakayoichagua.
Naomba wanakamati washiriki kikamilifu kutoa maoni yao kwa sababu wao ndio wahusika wakuu wa hafla hii. Baadaye nitaweka uzi kueleza yale yaliyoafikiwa na wadau mbalimbali.
Naomba sasa niwakaribishe wadau mbalimbali watoe maoni yao ili twende sawa.
Karibuni sana