JF Get Together Party sasa kufanyika Jumamosi Tarehe 25 Januari 2014…!!!!!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
secret-meeting-women-men-party-sex-delaine.jpg


Haya tena wadau wa JF.
Ndio tunaumaliza mwaka 2013 na tunaukaribisha mwaka 2014.
Kama mnakumbuka January 2013 tulifanya White Party pale Kebby's Hotel Mwenge ambapo ilifana sana.
Kwa mara nyingine tena tunaandaa Party nyingine ambayo itafanyika tarehe 25 January 2014 katika ukumbi utakaotangazwa kadiri muda unavyojongea kwa sababu bado tunao muda wa kutosha.

Kamati ya maandalizi inaundwa na wana JF wafuatao:
1. Paloma
2. Mtambuzi
3. gfsonwin
4. Madame B
5. Vin Diesel
6. jouneGwalu
7. Jiwe Linaloishi
8. cacico
9. lara 1
10 ladyfurahia
11. Kipaji Halisi

Siyo lazima kamati hii ikutane bali wajumbe wa kamati hii watakuwa wakiwasiliana kwa simu au kwa PM au hata kwa kuweka mapendekezo yao katika huu uzi kw aajili ya kufanikisha hafla hii muhimu kwetu.

Hapa chini nitaweka mchanganua wa bajeti inayohitajika ili kufanikisha hafla hii:

Cocktail Menu kwa makadirio ya watu 40 watakaohudhuria

Mahitaji
Idadi
Gharama
Jumla
Ukumbi100
BitesKwa watu 40@15,000/=600,000/=
VinywajiKwa watu 40Beer 4 @3,000/=480,000/=
Mziki1@150,000/=150,000/=
Corkage kwa vinywaji vikaliChupa 5@15,000/=75,000/=
Jumla1,305,000/=

Kwa hiyo kwa makadirio ya bajeti hiyo kila mdau anatakiwa kuchanga kiasi cha shilingi 35,000/=

Au

Dinner Menu kwa makadirio ya watu 40 watakaohudhuria

Mahitaji
Idadi
Gharama
Jumla
Ukumbi100
DinnerKwa watu 40@20,000/=
800,000/=
VinywajiKwa watu 40Beer 4 @3,000/=480,000/=
Mziki1@150,000/=150,000/=
Corkage kwa vinywaji vikaliChupa 5@15,000/=75,000/=
Jumla1,505,000/=

Kwa hiyo kwa makadirio ya bajeti hiyo kila mdau anatakiwa kuchanga kiasi cha shilingi 40,000/=

*Mimi Mzee Mtambuzi nitajitolea chupa tano za vinywaji vikali ambvyo ndivyo vitakachochajiwa Corkage ili viingizwe ukumbini. Hapa nazungumzia vinywaji kama Contesa, Strawberry Lips, Govinder Kumar, Vodka, Jack Daniel, n.k.

Bajeti hii nimeikadiria kwa kuangalia gharama za hoteli zinazofanana na Hoteli ya Kebby's mahali tulipofanya White Party January 2013, kwa hiyo zinaweza kupungua au kupanda kulingana na idadi ya wadau watakaohudhuria au hoteli tutakayoichagua.

Naomba wanakamati washiriki kikamilifu kutoa maoni yao kwa sababu wao ndio wahusika wakuu wa hafla hii. Baadaye nitaweka uzi kueleza yale yaliyoafikiwa na wadau mbalimbali.

Naomba sasa niwakaribishe wadau mbalimbali watoe maoni yao ili twende sawa.

Karibuni sana

spa-party-massage.gif
 
Imekaa sawa mpaka hapo....

Mengine nasubiri mawasiliano ya wadau, japo nafasi yangu unaijua ilivyo ya kimagumashi sana japo sipendi kuangusha watu.
Otherwise tupo pamoja.

Mkuu jouneGwalu maandalizi ya hii hala yatafanyika kwa njia ya Mtandao hakuna umuhimu wa kukutana ttakuwa tunawasiliana kwa simu au kwa PM nadhani kwa njia hizi mbili hutakosekana.....
 
Last edited by a moderator:
Naona kaka mkubwa umerudi...

Last time iliitwa "JF Dar Wing: White Party"

Mwaka huu kuna theme yoyote kuchagiza mjumuiko huu?
Ndio niko hapa kusubiri maoni ya wadau, kama una theme yoyote unaweza kuweka maoni yako hapa na yatazingatiwa....
 
mnaenda kubokoana huko yaani JF kuna member kibao why 40 tu,then mnajuana nyie sio bure
Mkuu hukuwa na haja ya kutukana, ukweli ni kwamba Party ya January mwaka huu tulikadiria wana JF 50 kuwa ndio watakaohudhuria lakini walifika 35 tu, hata hivyo katika uzi wangu hapo juu nimesema kwamba bajeti inaweza kupungua au kuongezeka kulingana na idadi ya wadau watakaojitokeza kuhudhuria hafla hii.

Unakaribishwa
 
Safi sana mkuu wazo zuri ila naona Cocktai naona itakuwa nzuri zaidi ya Dinner,
Nafikiri tukipata sehemu (hoteli) tutakapofanyia garama zingine zitajiseti automatically , kwahiyo nguvu kubwa tuweke kwenye kutafuta sehemu itakayotufaa, na kuhakikisha wadau wote wa Dar na wengineo watakaopenda kuja wanapata taarifa za uhakika

cc
1. Paloma
2. Mtambuzi
3. gfsonwin
4. Madame B
5. Vin Diesel
6. jouneGwalu
7. Jiwe Linaloishi
8. cacico
9. lara 1
10 ladyfurahia
11. Kipaji Halisi

Umesema vyema, Party ya January 2013 bajeti ilikuwa ni 20,000/= kwa kila mdau na tulipewa menu ya Bites kwa shilingi 12,000/= na kwa kuwa bia zilikuwa ni shilingi 2,000 tukaweka bajeti ya bia 3 na kiasi kilichobaki tukakodisha mziki kwa shilingi 80,000/= na ndio sababu bajeti ika balance lakini gharama zimepanda kidogo na ndio maana nadhani kama tukichagua menu ya cocktail ambayo haitofautiani sana na ile menu ya Kebby's kwa kujibana sana tukichanga shilingi 30,000/= tunaweza kufikia malengo. Kumbuka awali nilifanya makadirio ya juu.
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom