JF Focus: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Swali langu la tatu ni kwa Mkuu Zomba, ambae ana dakika 15 kulijibu:

Akihojiwa na gazeti la Washington Post hivi karibuni, Rais Kikwete alisema kuwa tatizo kubwa linalomkabili ni upungufu wa resources. Rais alisema kama akipata dola bilioni moja kwa mwezi kama mapato ya serikali, anataifanya Tanzania kuwa mbingu. Unakubaliana na Rais kuwa tatizo linalomkabili kama Rais ni lack of resources? Unadhani akipewa hizo bilioni moja kila mwezi anaweza kuifanya Tanzania kama mbingu?

Karibu Mkuu Zomba

Yes, Dollara Billion moja kwa mwezi ni nyingi sana kwa nchi kama Tanzania na ikiwa tutaipata na nnaona zipo karibu kwani Kikwete kajitahidi sana kuyaalika makampuni ya mafuta na gas na tunaanza kuona mafanikio. Nna uhakika tukiwa nazo hizo tutakuwa kwenye "cloud seven".

Unajuwa Mwali, watu wanapotosha sana wanapojaribu kutafsiri neno kwa neno la Kiingereza kuwa ndicho kilichosemwa, hiyo kuwa kama Mbingu aliiongelea kwa Kiswahili? Kama aliiongea kwa Kiingereza naomba uweke "context" ya hayo maneno ili ieleweke vyema.

Kama nilivyokuonesha hapo juu kuhusu "cloud seven"

According to Brewer's Dictionary of Phrase and Fable:

'The expression derives from terminology used by the United States Weather Bureau. Clouds are divided into classes, and each class into nine types. Cloud nine is cumulonimbus, a cumulus cloud of great vertical extent, topped with shapes of mountains or towers'.

Other people derive it from the ninth circle of heaven in Dante's Divine Comedy (i.e. the nearest to God).

The OED doesn't give a derivation, but notes that 'cloud seven' has also been used. It quotes from Flexner and Wentworth's Dictionary of American Slang (1960), which defines 'On cloud seven' as 'completely happy, perfectly satisfied, in a euphoric state'.

Source: What is the origin of the phrase 'cloud nine' or 'being on cloud nine'?

Kwa hiyo utaona Kikwete alimaanisha kuwa 'completely happy, perfectly satisfied, in a euphoric state' lakini ukiibadili Kiswahili ndio utaishia kuifananisha Tanzania na Mbinguni.
 
Swali langu la tatu ni kwa Mkuu Zomba, ambae ana dakika 15 kulijibu:

Akihojiwa na gazeti la Washington Post hivi karibuni, Rais Kikwete alisema kuwa tatizo kubwa linalomkabili ni upungufu wa resources. Rais alisema kama akipata dola bilioni moja kwa mwezi kama mapato ya serikali, anataifanya Tanzania kuwa mbingu. Unakubaliana na Rais kuwa tatizo linalomkabili kama Rais ni lack of resources? Unadhani akipewa hizo bilioni moja kila mwezi anaweza kuifanya Tanzania kama mbingu?

Karibu Mkuu Zomba

Kamwe Tanzania hatuna tatizo kabisa la Resources bali tuna lack of leadership, tukianza kuhesabu nature resources tulizo nazo unaweza kutokwa na machozi, cha kushangaza viongozi hawa hawa wameshindwa kabisa hata kupata semina ndogo kutoka Rwanda kwamba wenzetu walifanyaje kutoka mauwaji ya kimbali mpaka nchi yao sasa iko stable!?

Angalia hapa, Rose Perot aliyekuwa mgombea urais wa Marekani wakati ni Millionea wa kutupwa, alipoulizwa ni kwa nini sasa anagombea Urais wakati yeye ni Milionea? akawjibu tu kimzaha, "Urais ni utajiri wa mwisho.

Hapa nadhani Rais Kikwete naye ameamuwa kuja na mdhaha wake kwamba licha ya ufisadi wa Ikulu kujihusisha na biashara, watu kujimilikisha mali za umma kama mgodi wa makaa ya mawe kiwira, kukwapuwa fedha za EPA, Miradi ya kitapeli kma Richmond na kama haitoshi hawa wanoitwa waheshimiwa Wabunge nao kujiongezea posho ya kukaa kutoka 70,000 mpaka 200,000 na bado Rais anayeongoza Taifa hilo hilohilo analalama kwamba ni lack of resources!? This is big joke.

Hapa sijaorodhesha twiga wanaosafrishwa wazima wazima na wala hatujagusa migodi yetu na wala hatujaongelea utajili wa Bahari na maziwa yetu, ukisikia mtu mwenye akili timamu anatamka kwamba Tanzania ina lack of resources, basi mimi ili kumsitiri yatosha tu niseme walimnukuu vibaya.
 
Mkuu Zomba, samahani kama tutakua tumetafsiri vibaya maneno ya Rais Kikwete.

"If somebody says, 'What is your wish?' I'd say, 'If I got a billion dollars a month in terms of government revenue, I can turn Tanzania into heaven,'" Mr. Kikwete told The Washington Times in an exclusive interview.

Original context:
Tanzanian plows fertile ground in pitch for aid - Washington Times
 
Mkuu Matola, Asante kwa jibu lako kwa swali la tatu. Una dakika tano kumuuliza Mkuu Zomba ufafanuzi wa jibu alilotoa. Karibu
 
Mkuu Zomba, samahani kama tutakua tumetafsiri vibaya maneno ya Rais Kikwete.

"If somebody says, 'What is your wish?' I'd say, 'If I got a billion dollars a month in terms of government revenue, I can turn Tanzania into heaven,'" Mr. Kikwete told The Washington Times in an exclusive interview.

Original context:
Tanzanian plows fertile ground in pitch for aid - Washington Times

Si unaona Kiingereza na Kiswahili ni shida kutafsiri neno kwa neno. Heaven kwa sisi ni "peponi" kwa wengine "mbinguni". Lakini kama uonavyo alimaanisha atapafanya pawe pazuri.
 
Kwa vile Matola hakuuliza swali lolote la ufafanuzi, nitauliza swali moja:

Mkuu Zomba, kuna members walio pendekeza kua hata Rais Kikwete akipewa hizo dollars Billioni moja kwa mwezi hakutakua na mabadiliko sababu tatizo la Tanzania sio kukosa resources bali ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Unasemaje kuhusiana na hilo?

Naomba uwasilishe majibu ya ufafanuzi ndani ya dakika tano. Baada ya hapo utamuliza Matola swali la ufafanuzi wa jibu lake la tatu, kama unalo. Asante.
 
Taarifa kwa waalikwa na members wote wanao fatilia mjadala huu:

Itakapo fika saa kumi na mbili East African Time (18:00 EAT) tutachukua break ya masaa mawili na kurudi tena saa mbili kuendelea na mjadala. Hii ni kuwapa fursa wale walio funga waweze kufuturu. Asanteni kwa uvumilivu.
 
Tunaendelea na swali la nne:

Hivi karibuni kumekuwa na migomo ya madaktari ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya afya. Katika kujaribu kutatua huu mgogoro Rais Kikwete alikutana na viongozi wa madaktari Ikulu. Hata hivyo, kumekuwa na tena mgomo wa madaktari. Nini maoni yako kuhusiana na jinsi Rais Kikwete na utawala wake alivyo/anavyolishughulia suala zima la mgogoro wa madaktari?

Namkaribisha mkuu Matola ambae ana dakika kumi na tano kuandaa na kupost jibu lake kwa swali hili. Karibu mkuu.
 
Kwa vile Matola hakuuliza swali lolote la ufafanuzi, nitauliza swali moja: Mkuu Zomba, kuna members walio pendekeza kua hata Rais Kikwete akipewa hizo dollars Billioni moja kwa mwezi hakutakua na mabadiliko sababu tatizo la Tanzania sio kukosa resources bali ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Unasemaje kuhusiana na hilo? Naomba uwasilishe majibu ya ufafanuzi ndani ya dakika tano. Baada ya hapo utamuliza Matola swali la ufafanuzi wa jibu lake la tatu, kama unalo. Asante.
Mwali mimi nasubili swali la 5 kuna wanaotaka kufuturu jioni hii, jukumu la kuuliza maswali naawchia Members kwa leo kwa sababu hii thread itakuwa sticky kwa siku kadhaa basi hapo ndio utakuwa uwanja mpana zaidi.
 
Kwa vile Matola hakuuliza swali lolote la ufafanuzi, nitauliza swali moja:

Mkuu Zomba, kuna members walio pendekeza kua hata Rais Kikwete akipewa hizo dollars Billioni moja kwa mwezi hakutakua na mabadiliko sababu tatizo la Tanzania sio kukosa resources bali ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Unasemaje kuhusiana na hilo?

Naomba uwasilishe majibu ya ufafanuzi ndani ya dakika tano. Baada ya hapo utamuliza Matola swali la ufafanuzi wa jibu lake la tatu, kama unalo. Asante.

Hao watakuwa wapinzani, wao si ndio kazi yao rasmi? "upinzani" hakuna jema la Kikwete wanaloliona ingawa rekodi zote zinaonesha kuwa kila nyanja Kikwete kafanya zaidi ya Rais Mwengine yeyote yule.

Tatizo la Watanzania wanafikiri dhahabu ilio chini ya ardhi, kabla ya kuchimbwa, kusafishwa, kufikishwa sokoni ni mali. Kama mali kinawashinda nini kwenda kuchimba wenyewe? kuna mahali Serikali imewazuia? NO.
 
Tunaendelea na swali la nne:

Hivi karibuni kumekuwa na migomo ya madaktari ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya afya. Katika kujaribu kutatua huu mgogoro Rais Kikwete alikutana na viongozi wa madaktari Ikulu. Hata hivyo, kumekuwa na tena mgomo wa madaktari. Nini maoni yako kuhusiana na jinsi Rais Kikwete na utawala wake alivyo/anavyolishughulia suala zima la mgogoro wa madaktari?

Namkaribisha mkuu Matola ambae ana dakika kumi na tano kuandaa na kupost jibu lake kwa swali hili. Karibu mkuu.
Maoni yangu naona tatizo kubwa Serikali inayotawala haijielewi na wala haitambui wajibu wake kwa Umma wa Watanzania, na hata kama ikitokea kuna wakati ikajitambuwa inakuwa ngumu kutekeleza hata yale wanayoahidi wenyewe kwa hiyari yao.

Udhaifu wa Serikali hii uko wazi kabisa hasa pale waliposhindwa kumaliza matatizo haya ya matadaktari na chama cha madaktaari Tanzania (MAT)

Wizara ya afya ina viongozi waandamizi kuanzia Katibu mkuu Naibu Waziri na Waziri mwenyewe, wote hao walishindwa either kwa kiburi na ulevi wa madaraka au dharau tu kama walivyozoea kuwadharau Watanzania kwa miaka yote, issue kubwa ilikuw ni madai ya madaktari waliokuwa wanadai stahiki zao ambazo ni malimbikizo ya miezi mitatu tu.

Hapa tusidanyane wala kutafuna maneno chanzo halisi cha mgogoro huu ni pale Serikali ilipoamuwa kuwaondoa madaktari wote Inters na kuwsambaza kwenye Hospital za mawilayani hiki ndio kikawa chanzo kikuu cha mgogoro huu, na MAT waktangaza kuungana na wnataaluma wenzao.

Hapa ndipo Rais JK alipaswa kuingilia kati kama mkuu wa nchi na badala yake akaendelea na Diplomasia yake ya ukimya na ule usemi wake ni upepo tu utapita.

Cha kushangaza na kama siyo kusikitisha, JK aliweza kuuzima mgomo huu kwa siku moja tu akiwa kama Mkuu wa nchi na Madaktari waksema wazi wana imani na Rais, sasa basi swali linarudi je Rais alitimiza ahadi zake kwa madaktari?
Hapa bila kumung'unya mneno JK ni Rais wa kigeugeu kabisa na haaminiki wale Madaktari si waoo wadogo mkubaliane kitu halafu wje kugeuka si kweli.
Hizi ni Filamu za JK Production na sasa Director ni Kova.
 
Mwali mimi nasubili swali la 5 kuna wanaotaka kufuturu jioni hii, jukumu la kuuliza maswali naawchia Members kwa leo kwa sababu hii thread itakuwa sticky kwa siku kadhaa basi hapo ndio utakuwa uwanja mpana zaidi.
Kufatana na pendekezo hili, na kwavile hakuna swali lolote la ufafanuzi uliulizwa toka kwa waalikwa, naona kuanzia hapa tutaendelea kuuliza swali bila kuwepo nafasi ya ufafanuzi. Ufafanuzi huo utatolewa mwisho wa mjadala. Kuhusiana na wanao taka kufturu, tayari nimesha toa taarifa hapo juu. Asante.
 
Sasa namkaribisha Zomba kujibu swali la tano linalo husiana na mgogoro wa madaktari. Unapewa dakika kumi na tano. Karibu mkuu.
 
Tunaendelea na swali la nne:

Hivi karibuni kumekuwa na migomo ya madaktari ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya afya. Katika kujaribu kutatua huu mgogoro Rais Kikwete alikutana na viongozi wa madaktari Ikulu. Hata hivyo, kumekuwa na tena mgomo wa madaktari. Nini maoni yako kuhusiana na jinsi Rais Kikwete na utawala wake alivyo/anavyolishughulia suala zima la mgogoro wa madaktari?

Namkaribisha mkuu Matola ambae ana dakika kumi na tano kuandaa na kupost jibu lake kwa swali hili. Karibu mkuu.

Mgomo wa madaktari Kikwete kaushughulikia vyema sana. Mwanzo mpaka mwisho na kila hatua alikuwa anawaeleza wananchi hatua iliyochukuliwa.
 
Nawashukuru waalikwa wote kwa majibu yao. na sasa tunaendelea na swali la tano linalo husiana na mapambano dhidi ya ufisadi nchini kwetu:

Mnamo mwaka 2009, akijibu swali la Jacob Mkama wa Ukerewe kwamba serikali yake haijafanya juhudi katika kukabiliana na mafisadi, Rais Kikwete alisema kuwa katika dunia, Tanzania inaweza kuingia kwenye rekodi ya kuthubutu kwa kuweza kuwafikisha mahakamani zaidi ya vigogo 27 wa serikali.

Rais Kikwete alisema, "Tumejenga mazingira ya kuwataja wala rushwa, hivi sasa kuna kesi 578 toka kesi 50 zilizokuwepo mwaka 2005, taarifa nyingi zaidi zinapatikana. Wengine wanasema tunashughulika na dagaa tu, mbona papa hakuna? Tumefanya kesi za EPA, BoT, watendaji wakuu wa serikali 27 wako mahakamani na naweza kusema Tanzania tunaweza kuingia kwenye rekodi duniani ya kuthubutu." Nini maoni yako kuhusiana majibu ya Rais? Unakubali kwamba Rais Kikwete na serikali yake wanakabiliana na tatizo la ufisadi ipaswavyo? Toa sababu.

Karibu mkuu Zomba, una dakika kumi na tano kujibu swali hili. Asante.
 
Mkuu Zomba, bado una dakika tano kuwasilisha majibu yako. Karibu
 
Nawashukuru waalikwa wote kwa majibu yao. na sasa tunaendelea na swali la tano linalo husiana na mapambano dhidi ya ufisadi nchini kwetu:

Mnamo mwaka 2009, akijibu swali la Jacob Mkama wa Ukerewe kwamba serikali yake haijafanya juhudi katika kukabiliana na mafisadi, Rais Kikwete alisema kuwa katika dunia, Tanzania inaweza kuingia kwenye rekodi ya kuthubutu kwa kuweza kuwafikisha mahakamani zaidi ya vigogo 27 wa serikali. Rais Kikwete alisema, "Tumejenga mazingira ya kuwataja wala rushwa, hivi sasa kuna kesi 578 toka kesi 50 zilizokuwepo mwaka 2005, taarifa nyingi zaidi zinapatikana. Wengine wanasema tunashughulika na dagaa tu, mbona papa hakuna? Tumefanya kesi za EPA, BoT, watendaji wakuu wa serikali 27 wako mahakamani na naweza kusema Tanzania tunaweza kuingia kwenye rekodi duniani ya kuthubutu." Nini maoni yako kuhusiana majibu ya Rais? Unakubali kwamba Rais Kikwete na serikali yake wanakabiliana na tatizo la ufisadi ipaswavyo? Toa sababu.

Karibu mkuu Zomba, una dakika kumi na tano kujibu swali hili. Asante.

Hivi mtu kama Mramba ni Dagaa? duh.

Naomba muda wa kujitayarisha kwenda Masjid, naomba tukutane baadae.
 
Serikali ya CCM na hasa hapa tunaongelea utawala wa JK, ni kwamba umefeli kabisa katika swala la Rushwa na Ufisadi, na mfano hai ni Mkurugenzi mwenyewe wa taasisi ya kupamba Rushwa Edward Hosea alinukuliwa na Wikiliks kwamba anakwamishwa na Rais Kikwete kuwashughulikia wala Rushwa wakubwa.

Lakini tunaweza tukasema Wikliks ni wadaku tu na wanamuonea wivu Rais, je JK alipata wapi Mamlaka ya kuwasamehe wezi wa pesa za EPA wakati ni kabisa katiba inazungumza wazi, Mamlaka ya Rais ni kumsamehe mfungwa ambaye ameshahukumiwa?

Je unaweza ukaongea na watu makini na ukawaambia Serikali ya namna hii inapiga vita rushwa kweli? ninachofahamu mimi wengi wa wanaoitwa vigogo waliofikishwa mahakamani wamefikishwa mahakamani kwa visa vyao vya kisiasa na siyo kweli kwamba Taasisi ya Kupamba Rushwa eti iko huru. Big no.

Tukija kwa mtoto wa Rais yeye ndio amezungukw n kundi la maharamia wa uchumi, kijana mdogo kama huyu Ridhiwani ambaye amemliza Chuo kikuu juzi tu na leo hii ni Billione je uthapo kuna vyombo vya kupambana na Ufisadi?

Kwakeli JK na Serikali yake hakuna lolote wanalolifanya kupambana na ufisadi zaidi ya hii taasisi ya Kupamba Rushwa ipo nchini ili kukidhi matakwa ya wafadhili, lakini hawn kazi zaidi ya kujishughulish na Mission town za mjini na kusubili offer za bia na vijiela mbuzi ili watu wenye chuki zao za siku nyingi wakamatishane kwa gia ya Rushwa. ni upuuzi mtupu.
 
Kwa vile mkuu Zomba ameomba nafasi ya kwenda masjid tunaenda mapumzikoni, tutarejea wote saa moja na nusu East African time (19:30 EAT).
Tutakapo rudi tutaendelea na swali la sita. Asanteni wote.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom