JF Focus: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mwali

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
7,014
5,610
Rejea thread ya Roulette ya tarehe 19 mwezi huu (Link) kua leo kutakua na mjadala kati ya Matola na zomba kuhusu tathmini ya utawala wa Rais Kikwete tokea aingie madarakani mwaka 2005 hadi sasa.

Nimeandaa maswali kumi ambayo nimeyatafuta kupitia kwa members wengine wa Jamii Forums na kwa kupitia mijadala ya nyuma katika jukwaa la siasa, yanayo husiana na utawala wa Rais Kikwete.

Inawezekana sitauliza maswali yote ambayo wana Jamii Forum wangependa niwaulize wawili hawa kutokana na idadi ya maswali nilio pewa na muandaaji wa mjadala huu (Moderator), ila baada ya Matola na Zomba kujibu hayo maswali kumi wanajamii forum watapewa nafasi ya kuwauliza waalikwa maswali. Tutajaribu kuchagua maswali yenye mantiki, kwa hiyo taafdhali uliza maswali ambayo yataonesha uwezo wako wa kufikiri na kuhoji.

Mjadala utaenda kama ifwatavyo:

  • Nitsweka swali moja moja, na swali la kwanza ataanza kujibu Zomba, la pili ataanza kujibu Matola na tuta-alternate hivo hadi tutakapo maliza maswali yote.
  • Baada ya kila mwalikwa kujibu swali toka kwangu, kila mwalika atapewa nafasi ya kumuuliza mwenzie swali la ufafanuzi ya yale alio jibu. Ni matarajio yetu kwamba waalikwa watahojiana kwa kufata kanuni za mjadala na hasa kuzingatia sheria za Jamii Forums.
  • Kwa mtiririko mzuri wa mjadala huu ningewaomba wanajamii forum wengine wasichangii kwanza hadi pale tutakapo maliza kuwahoji waalikwa wetu. Kwa wakati huu, kuna thread maalum imeandaliwa jukwaa la siasa ambapo members watakua huru kuchangia, na kuuliza maswali. (Link to the thread)

Nawashukuru Mods kwa kunipa nafasi hii ya kuwahoji Great Thinkers wawili hawa, na pia nawashukuru mmbers wote watakao fatilia mjadala huu.

Kama Matola na Zomba wako tayar, naomba waseme neno fupi, na baada ya hapo nitaanza na wali la kwanza.

Karibuni na asanteni.

Updates:

Update Muhimu:
Jamani wana JF kuna mambo ni personal zaidi, lakini hili lililonipata naona ni janga, mama yangu mzazi amefail step na alikuwa amefanyiwa oparesheni ya neuron surgeon sasa ametonenesha ile sehemu aliyofanyiwa oparesheni, nimeshinda MOI leo na sikuweza kufanya chochote, Nampenda Mama yangu siwezi kumteleza.

Natumia fursa hii kuwaomba radhi wana JF kwamba wanisamehe kwa kutokupatikana leo, nadhani kwa waelewa wanajuwa vyema uchungu wa Mama. Roulette mimi ndio nimerudi nyumbani sasa hivi wakati waliofunga wanajiandaa kupata daku. tusameheehane ndugu zangu, nina majonzi.
 
Swali la kwanza:

Rais Kikwete amekuwa madarakani tokea mwaka 2005. Ukilinganisha na utawala wa Marais wastaafu, Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa, nini maoni yako kuhusiana na utawala Rais Kikwete? Rais Kikwete ana yapi ya kujivunia aliyofanya katika kipindi cha miaka aliyokaa madarakani? Jibu la swali liguse sekta zote kuanzia ya uchumi, afya, usafiri,sheria na utawala, michezo, n.k.

Una dakika kumi kujibu swali hili, kisha hapo nitamwelekeza Matola.
 
Asalaam Aleykum, kwanza nawapongeza kwa mara nyingine tena wale wote ambao wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, nawapongeza na wale wengine wote wasiopo kwenye mfungo lakini wanauheshimu mwezi huu, wanaheshimu uamuzi wetu wakufunga na tunawashukuru zaidi kwa kutupa hamasa sisi tulio kwenye swaum.
Natamani kuingia moja kwa moja kwenye kujibu swali la kwanza, lakini uungwana hauniachi kufanya hivyo bali unanilazimisha kutoa pongezi zangu za dhati kwa walioubuni mnakasha huu. Natoa shukrani zangu pia kwa mshiriki mwenzangu wa mnakasha huu al maaruf Matola kwa kukubali kushiriki, halikadhalika natoa shukrani zangu kwa wote waliojitolea kuufatilia mnakasha huu.

Kwa kuwa swali ni refu na limegusa mambo mengi nilikuwa naomba nilijibu kwa zaidi ya post moja ili wasomaji wapate raha.
 
Swali la kwanza:

Rais Kikwete amekuwa madarakani tokea mwaka 2005. Ukilinganisha na utawala wa Marais wastaafu, Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa, nini maoni yako kuhusiana na utawala Rais Kikwete? Rais Kikwete ana yapi ya kujivunia aliyofanya katika kipindi cha miaka aliyokaa madarakani? Jibu la swali liguse sekta zote kuanzia ya uchumi, afya, usafiri,sheria na utawala, michezo, n.k.

Una dakika kumi kujibu swali hili, kisha hapo nitamwelekeza Matola.

Kwanza kabisa napenda kuelezea kuwa nimefurahi sana kuwa swali limelenga moja kwa moja kwenye kulinganisha madaraka ya Rais wa sasa mpendwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na awamu zilizopita za "Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa". Kama swali linavyojionesha "ana yapi ya kujivunia aliyofanya katika kipindi cha miaka aliyokaa madarakani?" katika nyanja tofauti, hususan "uchumi, afya, usafiri, sheria na utawala, michezo, n.k."

Napenda kuainisha majibu yagu ya awali na kuwajulisha wasimamizi na wafatiliaji mnakasha huu huu, kuwa kila nyanja imesheheni nakshi na fasaha na tawimu teletele, kweny "post" hii ntaanza na moja la "uchumi" na post zifuatazo ntawasilisha yanayohusu mengineyo kama yalivyo kwenye swali:

Uchumi wakati wa Nyerere;

Ikumbukwe kuwa, wakati Mwalim Nyerere anapewa madaraka ya nchi hii uchumi wa Tanganyia ulikuwa mzuri sana hususan katika kilimo, Tanganyika ilikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao nje ya Tanganyika katika Afrika, Nyerere kwa muda mfupi tu akatutoa huko na kutufikisha kuwa waagiizaji wakibwa wa chakula.
Under his Presidency, Tanzania slipped from being the largest exporter of food in Africa to the biggest importer of food.

Source: Mwalimu Nyerere | Julius Nyerere; Life Times Legacy

Tanzania slipped from being the largest exporter of food in Africa to the biggest importer of food.

Source: Julius Nyerere - New World Encyclopedia

Kwa kifupi kwa kuwa hatumzungumzii Nyerere, na "sources" zipo nyingi sana zinazoonesha jinsi uchumi wetu ulivyoporomoka sana wakati wake, naomba atakae a google "economy collapsed during Nyerere" atajionea mwenyewe maana nikianza kuyabandika hapa tutatoka nje ya mnakasha.Kwa kifupi, hatuna cha kujivunia katika uchumi wakati wa Nyerere tuliushuhudia ukiporomoka kwa kujaribu kwake kufata mfumo wa ujamaa ambao ulishindwa kabisa.

Uchumi wakati wa Mwinyi;

Ikumbukwe kwamba Mwinyi ndiye alikuwa "savior" wa waTanzania mpaka akapewa jina la "Ruksa" kwa sababu ni yeye aliyetufungulia milango ya uchumi huria ni yeye aliyeleta maamuzi ya kufunga mashirika ya umma yaliyokuwa yananyonya uchumi wote wa Tanzania kwa kupewa ruzuku hata yanapofanya vibaya. Kwa kifupi Mzee Mwinyi alikuwa na kazi ngumu sana ya kutuondoa kwenye lindi la umaskini na kutuanzishia mfumo mpya wa uchumi ambao tunaendelea nao. Kwa hilo tumsifu Mzee Mwinyi:

During Mwinyi's terms Tanzania took the first steps to reverse the socialist policies of Julius Nyerere. [2] He relaxed import restrictions and encouraged private enterprise.

Soma zaidi: Ali Hassan Mwinyi - Wikipedia, the free encyclopedia

In 1986 the newly-appointed Mwinyi Government embarked on a broad-based Economic Recovery Program supported by the International Monetary Fund (IMF) and the World Bank. This was reinforced by an Economic and Social Action Program in 1989. Under these two programs, Government worked to dismantle the system of state controls and promote private sector expansion--including liberalizing the trade and exchange system, eliminating price controls and most state monopolies, and opening the financial sector to private sector participation. Rehabilitation of key infrastructure was also made a priority, particularly roads, railways, and ports.

Source: Foodnet-Uganda > Market Information

Uchumi wakati wa Mkapa;

Mkapa kwenye uchumi aliendeleza aliyoyanzisha Mwinyi nae akatia mkazo kwenye kukaribisha wageni kuwekeza tukaona "influx" ya makampuni makubwa ya kigeni yakipewa vitalu vya uwindaji, ardhi kubwa za kuchimba madini, Ulikuwa ni muelekeo mzuri kiuchumi kinadharia.

Kosa kubwa nilionalo ni pale "corruption" ya hali ya juu ilipokithiri wakati wa Mkapa, hususan baada ya kifo cha Nyerere. Madudu wmengi au karibu yote yanayoibuka sasa utakuta yameanzia au yemetendeka wakati wa Mkapa; EPA, KIWIRA, BOT, RADAR, kuainisha machache. Sina mengi ya kumsifu kwani kipindi chake cha mwisho aliharibu sana kwa kutuacha Kiza na kwa tuhuma nyingi za ufisadi zilizodhihirika "immediately" baada ya kuondoka kwake madarakani na mpaka leo bado zinatutesa.

Uchumi wakati wa Kiwete;

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ana kila sababu za kujivunia katika uchumi wakati wa madaraka yake, kwa uchache kuhusu uchumi ni haya hapa yakiambatana na takwimu zilizo wazi kabisa:

Asalaam Aleykum,

kwanza nawapongeza kwa mara nyingine tena wale wote ambao wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, nawapongeza na wale wengine wote wasiopo kwenye mfungo lakini wanauheshimu mwezi huu, wanaheshimu uamuzi wetu wakufunga na tunawashukuru zaidi kwa kutupa hamasa sisi tulio kwenye swaum.

Natamani kuingia moja kwa moja kwenye kujibu swali la kwanza, lakini uungwana hauniachi kufanya hivyo bali unanilazimisha kutoa pongezi zangu za dhati kwa walioubuni mnakasha huu. Natoa shukrani zangu pia kwa mshiriki mwenzangu wa mnakasha huu al maaruf Matola kwa kukubali kushiriki, halikadhalika natoa shukrani zangu kwa wote waliojitolea kuufatilia mnakasha huu.

Naanza:

Kwanza kabisa napenda kuelezea kuwa nimefurahi sana kuwa swali limelenga moja kwa moja kwenye kulinganisha madaraka ya Rais wa sasa mpendwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na awamu zilizopita za "Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa". Kama swali linavyojionesha "ana yapi ya kujivunia aliyofanya katika kipindi cha miaka aliyokaa madarakani?" katika nyanja tofauti, hususan "uchumi, afya, usafiri, sheria na utawala, michezo, n.k."

Napenda kuainisha majibu yagu ya awali kuyapanga kama yalivyo:

Uchumi wakati wa Nyerere;

Ikumbukwe kuwa, wakati Mwalim Nyerere anapewa madaraka ya nchi hii uchumi wa Tanganyia ulikuwa mzuri sana hususan katika kilimo, Tanganyika ilikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao nje ya Tanganyika katika Afrika, Nyerere kwa muda mfupi tu akatutoa huko na kutufikisha kuwa waagiizaji wakibwa wa chakula.

Under his Presidency, Tanzania slipped from being the largest exporter of food in Africa to the biggest importer of food.

Source: Mwalimu Nyerere | Julius Nyerere; Life Times Legacy

Tanzania slipped from being the largest exporter of food in Africa to the biggest importer of food.

Source: Julius Nyerere - New World Encyclopedia

Kwa kifupi kwa kuwa hatumzungumzii Nyerere, na "sources" zipo nyingi sana zinazoonesha jinsi uchumi wetu ulivyoporomoka sana wakati wake, naomba atakae a google "economy collapsed during Nyerere" atajionea mwenyewe maana nikianza kuyabandika hapa tutatoka nje ya mnakasha.

Kwa kifupi, hatuna cha kujivunia katika uchumi wakati wa Nyerere tuliushuhudia ukiporomoka kwa kujaribu kwake kufata mfumo wa ujamaa ambao ulishindwa kabisa.

Uchumi wakati wa Mwinyi;

Ikumbukwe kwamba Mwinyi ndiye alikuwa "savior" wa waTanzania mpaka akapewa jina la "Ruksa" kwa sababu ni yeye aliyetufungulia milango ya uchumi huria ni yeye aliyeleta maamuzi ya kufunga mashirika ya umma yaliyokuwa yananyonya uchumi wote wa Tanzania kwa kupewa ruzuku hata yanapofanya vibaya.

Kwa kifupi Mzee Mwinyi alikuwa na kazi ngumu sana ya kutuondoa kwenye lindi la umaskini na kutuanzishia mfumo mpya wa uchumi ambao tunaendelea nao. Kwa hilo tumsifu Mzee Mwinyi:

During Mwinyi's terms Tanzania took the first steps to reverse the socialist policies of Julius Nyerere. [2] He relaxed import restrictions and encouraged private enterprise.

Soma zaidi: Ali Hassan Mwinyi - Wikipedia, the free encyclopedia

In 1986 the newly-appointed Mwinyi Government embarked on a broad-based Economic Recovery Program supported by the International Monetary Fund (IMF) and the World Bank. This was reinforced by an Economic and Social Action Program in 1989. Under these two programs, Government worked to dismantle the system of state controls and promote private sector expansion--including liberalizing the trade and exchange system, eliminating price controls and most state monopolies, and opening the financial sector to private sector participation. Rehabilitation of key infrastructure was also made a priority, particularly roads, railways, and ports.

Source: Foodnet-Uganda > Market Information

Uchumi wakati wa Mkapa;

Mkapa kwenye uchumi aliendeleza aliyoyanzisha Mwinyi nae akatia mkazo kwenye kukaribisha wageni kuwekeza tukaona "influx" ya makampuni makubwa ya kigeni yakipewa vitalu vya uwindaji, ardhi kubwa za kuchimba madini, Ulikuwa ni muelekeo mzuri kiuchumi kinadharia.

Kosa kubwa nilionalo ni pale "corruption" ya hali ya juu ilipokithiri wakati wa Mkapa, hususan baada ya kifo cha Nyerere. Madudu wmengi au karibu yote yanayoibuka sasa utakuta yameanzia au yemetendeka wakati wa Mkapa; EPA, KIWIRA, BOT, RADAR, kuainisha machache. Sina mengi ya kumsifu kwani kipindi chake cha mwisho aliharibu sana kwa kutuacha Kiza na kwa tuhuma nyingi za ufisadi zilizodhihirika "immediately" baada ya kuondoka kwake madarakani na mpaka leo bado zinatutesa.

Uchumi wakati wa Kiwete;

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ana kila sababu za kujivunia katika uchumi wakati wa madaraka yake, nnadiriki kusema kuwa hakuna nyanja ambayo Kikwete hajavunja rikodi zilopo kabla yake katika kuyatimiza. Kwa uchache kuhusu uchumi ni haya hapa yakiambatana na takwimu zilizo wazi kabisa:

1. USIMAMIZI WA UCHUMI JUMLA:

Ukuaji wa Uchumi Katika kipindi cha miaka minne (2005 – 2009). Uchumi umeendelea kuimarika na Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.2 kwa mwaka katika kipindi hicho. Ukuaji huu wa uchumi ulichangiwa zaidi na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika sekta za: Bidhaa za viwanda; ujenzi; fedha; na mawasiliano na uchukuzi.

2. PATO LA MTANZANIA;

Pato la Mtanzania limekuwa likiongezeka katika kipindi chote cha awamu ya nne kutoka Dola za Kimarekani 392.8 mwaka 2005 hadi dola 525.2 mwaka 2008.

3.MWENENDO WA RIBA;

Viwango vya riba vimeonesha mwelekeo mzuri hasa kuanzia mwaka wa fedha 2006/07, ambapo riba kwenye amana za akiba zimekuwa zikiongezeka, wakati riba zinazotozwa kwenye mikopo zimekuwa zikipungua. Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2009/10 wastani wa viwango vya riba kwa amana za akiba za muda mfupi (hadi mwaka mmoja)ulikuwa asilimia 8.92 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.21 katika mwaka wa fedha 2003/04.

Katika kipindi hicho, wastani wa viwango vya riba vilivyotozwa na benki za biashara kwa mikopo ya mwaka mmoja ulipungua hadi asilimia 13.93 kutoka asilimia 15.75. Kutokana na mwelekeo huo wa riba, tofauti kati ya viwango vya riba kwenye amana za mwaka mmoja na viwango vya riba kwenye mikopo ya mwaka mmoja ilishuka kutoka 10.54 mwaka 2003/04 hadi 5.01mwaka 2009/10, sawa na kushuka kwa asilimia 47.5.

4. BIASHARA YA BIDHAA NJE;

Mauzo ya bidhaa nje yaliongezeka kwa asilimia 3.2 hadi kufikia dola za Kimarekani 2,697.6 milioni mwezi Novemba 2009. Ongezeko hilo lilichangiwa na mauzo ya dhahabu kwa asilimia 9.0 hadi kufikia dola 1,023.8 milioni, tumbaku kwa asilimia 35.3 hadi kufikia dola 151.4. Aidha, mauzo ya kahawa nje yaliongezeka hadi kufikia dola 117.2 milioni, sawa na asilimia 29.0.

5.MAPATO YA NDANI;

Katika kipindi cha miaka minne, Wizara ya Fedha na Uchumi, kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanya marekebisho ya mifumo na viwango vya baadhi ya kodi. Hatua hii imesaidia kuweka mazingira mazuri zaidi ya uzalishaji kurahisisha ukusanyaji wa kodi. Aidha, wigo wa kodi umeongezeka katika kipindi hicho.

6.KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MIKOPO;

Mikopo iliyotolewa na mabenki kwa sekta binafsi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi iliongezeka kutoka shilingi bilioni 1,571.0 mwezi Desemba 2005 hadi shilingi bilioni 4,710.2 mwezi Juni 2009, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 34.5 kwa mwaka. Mwezi Oktoba 2009 mikopo hiyo ilikuwa imefikia shilingi bilioni 4,836.0. Aidha, wastani wa riba kwa dhamana zote ilishuka kutoka asilimia 16.4,

7.KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI;

Mifuko ya Dhamana ya Mikopo (Credit Guarantee Scheme): Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dhamana wa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME Credit Guarantee Scheme) ambao unaratibiwa na Benki Kuu kumeboresha mazingira ya wenye mitaji midogo na ya kati waweze kupatamikopo kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha. Tangu mfuko huu uanzishwe, jumla ya SMEs 48 zimepata udhamini wa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.054. Kati ya wajasiliamali hao, sekta ya uzalishiji inaongoza ikifuatiwa na sekta za ujenzi na kilimo. Ili kuleta ufanisi zaidi, mwaka huu Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 10 kuongeza mtaji wa mfuko wa wajasiliamali wadogo na wa kati.

Kuongeza fedha katika Mfuko wa Uwezeshaji Kiuchumi wa wajasiriamali wadogo (Mfuko wa JK) kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB. ilitoa kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB (Shilingi bilioni 5.25) na CRDB (Shilingi bilioni 5.25). Kiasi hiki kiliwezesha kutolewa kwa mikopo ya Shilingi bilioni 37.17 ikiwa in asilimia 118 ya Shilingi 31.5 zilizotengwa kutolewa na benk hizo mbili.

Hayo ni baadhi tu ya mafanikio ya kujivunia ya kiuchumi Tanzania na yapo mengi sana, kuanzia mabarabara ya nayoendelea kujegwa hivi sasa, mitambo ya uzalishaji umeme inayoendelea kujengwa hivi sasa, kiwanda kikubwa cha chuma kinachoendelea kujengwa hivi sasa.

Licha ya hayo kuna msukumo ulifanyawa na Kikwete wa makusudi kabisa katika kuendeleza sekata ya mali asili na katika kipindi chake tumeona makampuni makubwa duniani yakivumbuwa gas ya asili kwa kiwango kikubwa sana na hili ni jema sana katika uchumi wetu wa siku za usoni. Hapa nnadiriki kusema kuwa wa kabla yake "uchumi walikuwa nao lakini waliukalia", Kikwete kabadili hilo badili ya kuukalia kausimamia kidete na matokeo hakuna asiyeyajuwa, Tanzania economy inabadilika kutoka kilimo kuwa namba moja kwenda kwenye Gas ya asili.

Hapo nimegusa uchumi tu, dakika kumi hazitoshi kuelezea mengi mema ya Kikwete.
 
Asante kwa jibu lako Mkuu Zomba, unapewa dakika kumi zingine za kukamilizha jibu lako, na kama hata hizo hazito tosha, basi mema mengine unaweza kutuletea baada ya mjadala huu. Karibu.
 
Post ya kwanza iligusa uchumi, post hii inagusa afya, kwa uchache ili nisiwa kere wasomaji;

Kuongezeka kwa jitihada za afya kumepelekea awamu ya Kikwete kujivunia kuweka rekodi ya Taifa katika kuzidisha "life expectancy" ya Mtanzania kutoka miaka chini ya 50 mwaka 2005 na kabla, na kwa sasa kufikia zaidi ya miaka 57.

1. Kuongezeka kwa jitihada za kupambana na magonjwa ya mlipuko;Elimu juu ya magonjwa ya kuambukkiza na yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii juu ya kujikinga na magonjwa mapya yanayojitokeza kama vilel ebola, marbug, Homa ya bonde la ufa na Homa ya mafua makali ya nguruwe.
Wizara imeendelea kuhamasisha jamii juu ya magonjwa milipuko kwa kutoa vipeperushi zaidi ya laki moja kwa nchi nzima pia imetoa elimu kwa umma kupiti vyombo mbalimbali vya habari kama vile radio, televion, magazeti na mabango ambayo yamebandikwa barabarani yakieleza mbinu za Kukabiliana na magonjwa ya milipuko.
2. Kupungua kwa vifo vya watoto wachanga na Mama wajawazito;

  • Chanjo zimeendelea kutolewa kwa watoto wote bila malipo. Chajo mpya imeongezwa aina ya ‘HiB Vaccine' chanjo hii ianajumushwa na chanjo nyingine 4 zilizokuwa zinatolewa kwa pamoja sasa zimekuwa tano na kuitwa chanjo ya Pentavalent (DPT –HB-Hib). Katika mwaka 2009 watoto waliopata chanjo ya surua ni asilimia 93%, DPT-HB3 asilimia 85%, OPV asilimia 88%.
  • Huduma za kliniki zimeboreshwa kwa ununuzi wa vifaa vya kupima mimba, uzito, upatikanaji wa dawa, kufundisha watoa huduma
  • Huduma kwa wajawazito na huduma za kujifungua pamoja na huduma kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano zimeendelea kutolewa bila malipo aktika vituo vya Serikali.
  • Vifaa mbalimbali vya huduma ya uzazi na kliniki wakati wa ujazito vimepelekwa katika hospitali 86 na vituo vya afya 50 kwenye mikoa 20. Aidha machakato wa kupeleka vifaa vya uzazi na kuhudumia watoto katika vituo 200 vya vya afya unaendelea.
  • Ununuzi wa pikipiki za miguu mitatu (ambulance) kwa ajili ya usafiri wa kina mama wajawazito unaendelea na pikipiki 400 zitanunuliwa.
  • Ujenzi wa Zahanati katika kila kijiji unaendelea kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM). Kati ya mwaka 2008/09 hadi 2009/10 zahanati 400 na vituo vya afya 78 vimejengwa.
3. Kuimarika kwa vita dhidi ya UKIMWI na Malaria;

  • Hali ya maambukiza nchini kiwango cha asilimia 5.7.% ya watu wenye umri wa miaka 15 – 49 (THMIS 2007 – 2008). Hali hii ni pungufu ukilinganisha kiwango na kiwango cha 7.7.% cha watu wenye umri kama huo iliyotolewa (THIS 2003 – 2004). Hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na Kampeni ya upimaji iliyozunduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Dr. J. K. Kikwete Julai 2007.
  • Hadi 2009 Disemba Kliniki 909 zinatoa Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI. Watu waishio na virusi vya UKIMWI 632,086 wamesajiliwa katika kiliniki hizo na 322,783 katik ya hao wanapata dawa za kupunguza makali ya viruasi vya UKIMWI.
  • Huduma za kupunguza maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto inatolewa katika vituo vya Tiba 3,626
  • Jamii inaendelea kuelimishwa kupitia vyombo mbali mbali vya upatikanaji habari ikiwa ni pamoja na machapisho, sinema vipindi vya radio, Televisheni na sanaa.
Ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu

  • Mwaka 2008 ni takribani 50% ya kaya hapa nchini zilikuwa na vyandarua vyeneye dawa ya kudumu (NGAO). Ili kuongeza kasi Serikali imeamua kugawa bila malipo ili ifikapo mwishoni mwaka mwaka 2011 killa sehemu ya kulaala iwe chandarua chenye dawa ya kudumu. Mwaka 2008 Serikali ilianzisha kampeni ya kugawa bila malipo vyandarua kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5. Hadi kufikia mwezi Aprili (2010) watoto takriban milioni 9 wamegawiwa vyandaru vyenye dawa ya kudumu. Kampeni hii imekamilika katika mikoa yote.
  • Kuanzia mwezi wa nane mwaka huu 2010 kuna kampeni ya pili ya kugawa bila malipo vyandarua 14.6 milioni kila kaya itapewa vyandarua viwili au zaidi,
Upuliziaji wa Viuatilifu Ukoko katika Kuta

  • (indoor Residual Spraying)
  • Kampeni hii imeanzia mkoa wa Kagera mwaka 2007 katika Wilaya ya Muleba, na Wilaya ya Karagwe 2008. Mwaka 2009, afua hii ilitekelzwa katika wilaya zote za mkoa wa Kagera kuanzia mwaka huu (mwezi Agosti, 2010 kampeni itaendelea itajumuisha pia mikoa ya Mara na Mwanza.
  • Kampeni hii imeanzia mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuwa mikoa hii ndiyo inaongoza kwa maambukizi ya malaria ifuatatiwa na mikoa ya Kanda ya Pwani
Tiba ya malaria kwa dawa mseto

  • Dawa mseto kama Alu ndiyo dawa bora za kutibu malaria kwa sababu ufanisi wake wa kuponya uko juu (aslimia 95%)
  • Hapa nchini wagonjwa wa malaria wanaokwenda kutibiwa katika vituo vya huduma ya afya vya Serikali wanatibiwa bila malipo au huchangia gharama kidogo kama Sera ya uchangiaji ilivyo.
4. Kutolewa kwa huduma za upasuaji wa moyo nchini;

  • Wagonjwa 168 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo
  • Wataalam wa upasuaji wa moyo wameongezeka, WAUJ ilipelekea jumla ya wataalam 27, nchini india na Israel kusomea upasuaji wa moyo na sasa wote wamerudi nchini wakiendelea na kutuoa huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
  • Ujenzi wa kituo maalum cha matibabu ya moyo umeanza kaktika hospiotali ya Taifa Muhimbili, WAUJ inashirikiana na Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mrisho J. Kikwete, na unatarajiwa kumalizika miezi kumi na nne ijayo. Kitakuwa ni kituo bora katika Afrika Mashariki na kati.
5. Kukamilika kwa ukarabati wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na upatikanaji wa vifaa vya kisasa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini

  • Karibu majengo yote ya Hospitali ya Taifa Muhimbili yamekarabatiwa na vifaa vya kisasa vimekwea vifaa hivyo ni CT Scan ya Kisasa, Magenet Resonance Imaging (MRI) ya kisasa, Digital, radiograph Sysytem, USS na Fluroscopy. Mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo zimeshafungwa.
  • Vifaa vya kisasa vimewekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
  • Idara ya Huduma za magonjwa ya Dharura imeimarishwa kwa kuwa na wataalam na vifaa tiba vya kisasa
  • Vituo vingi vya kutolea huduma za afya hapa nchini vimepatiwa vifaa vya kutibu wagonjwa
6. Kuimarishsa upatikanaji wa haki za watoto

  • Kukarabati majengo na kutoa vifaa katika mahabusi za watoto na shule ya maadilisho Irambo.
  • Kukamilisha ujenzi wa mahabusu ya watoto Mtwara.
  • Kukarabati chuo cha Walezi wa Watoto Kisangara.
  • Kutoa mafunzo kuhusiana na haki za watoto katika jamii.
  • Kuimarisha utaratibu wa utojai huduma kwa watotot walio katika mazingira hatarishi.
  • Kutoa huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi
  • Kuweka viwango vya utoaji wa hududma kwa toto walio katika mazingira hatarishi.
7. Kuimairisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu na wazee

  • Kukamilika kwa sera ya wazee
  • Kukamilisha sera ya watu wenye ulemavu
  • Kupitishwa kwa sheria ya walemavu 2010
  • Kukarabati nyumba za vyuo vya ufundi kwa watu wenye uelemavu.
  • Kukarabati majengo ya makazi ya wazee
  • Kuhamasisha jamii kuhusiana na utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kutoa nyenzo (vifaa) za kujimudu kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kuwajengea uwezo wazee na watu wenye ulemavu kwa kuwapa mitaji midogo midogo.
 
Kuhusu usafiri nadhaani hakuna asiyejuwa kuwa leo Tanzania kwenda Mwanz a na Bukoba huna haja ya kupitia Kenya, labda uende kwa kazi zako tu lakini si kwa lazima.

Barabara zaidi ya Kilomita 11,000 zilizojengwa, zinazotekelezwa kujengwa zikiwa kwenye awamu mbali mbali. Haijawahi kutokea kabla ya Kikwete. Zote pamoja na za Mkoloni hazifikii za miaka 7 ya Kikwete.
 
Point of interruption, Mwali PC yangu imenigomea kabisa Network muda mfupi tu baada ya kuingia kwenye thread, kwahiyo nitajibu maswali kwa style ya papo kwa papo sina tena muda wa kundaa mtililiko wa Kibunge. imebidi nikimbilie kwenye Internet Cafe.
 
Last edited by a moderator:
Point of interruption, Mwali PC yangu imenigomea kabisa Network muda mfupi tu baada ya kuingia kwenye thread, kwahiyo nitajibu maswali kwa style ya papo kwa papo sina tena muda wa kundaa mtililiko wa Kibunge. imebidi nikimbilie kwenye Internet Cafe.
Pole sana kwa yalio kukuta.
Basi naomba ujibu swali la kwanza. Una dakika ishirini kujibu swali hilo, baada ya hapo utapewa nafasi ya kumuhoji Zomba kuhusu jibu lake. Karibu.
 
Kuhusu sheria na utawala, kwa mara ya kwanza Tanzania tumeona ongezeko la mahakimu, majaji, na kupunguwa kwa kesi kwa kiasi kikubwa sana mahakamani.

Kwa ufupi, tuna tuzo ya kimataifa ya Utawala bora Tanzania wakati wa Kikwete, hatujawahi kuipata wakati wowote ule.

Mwali niendelee? nna mengi sana.
 
Kuhusu sheria na utawala, kwa mara ya kwanza Tanzania tumeona ingezeko la mahakimu, majaji, na kupunguwa kwa kesi kwa kiasi kikubwa sana mahakamani.

Kwa ufupi, tuna tuzo ya kimataifa ya Utawala bora Tanzania wakati wa Kikwete, hatujawahi kuipata wakati wowote ule.

Mwali niendelee? nna mengi sana.
Asante sana mkuu, muda wako umeisha, labda unaweza kuyaweka hayo mengine baada ya maswali kumi na tano kumalizika. Asante sana kwa majibu ulio toa.
 
Ntajibu swali la kwanza kama ifuatavyo bila kuwachosha wafuatiliaji na bila kumlisha mtu takwimu za kufikrika;

Kwanza JK amefanikiwa sana katika awamu yake kuanzia 2005 mpaka sasa kubwa zaidi kukuza uhuru wa vyombo vya habari licha ya kuendele kuwepo kwa sheria kandamizi katika sheria ya Usalama wa Taifa.

Pili tukienda kwenye swala la uchumi hapa mimi nitashindwa kumpa credit yoyote kwa sababu hahutajiki kuwa mchumi kufahamu kwamba wkti JK anakbidhiw nchi tulikuw na pesa ya kutosha, kasi ya ukuaji uchumi ilikuwa ni ya kuridhisha na mfumuko wa bei ulikuwa chini, sasa hapa nashindwa kuelewa JK nitamsifu kwa lipi!

Ingetosha kunieleza nieleze mafanikio ya Serikali ya CCM tangu awamu ya kwanza mpaka hii awamu ya nne kwa kweli ningekuwa na mengi ya kuelezea serikali ya CCM ilivyofanikiwa na kw kweli yapo ya kujivunia, lakini kwa JK napata shida kidogo, maana mimi sipo hapa kwa ajili ya kutoa takwimu za kusadikika kuhusu maisha ya Watanzania.

Na mafanikio ya kipekee aliyoyapata JK, ni kuwa ndio Rais pekee kipenzi kuwahi kutokea nchi hii kuwa kipenzi cha watawala wawili mfululizo Rais Bush na Rais Obama, haya ni mfanikio mkubwa sna kwake.
 
Asante kwa jibu lako Mkuu Matola. Sasa kambla ya kuendelea na swali la pili, una swali lolote ungependa kumuuliza Zomba kuhusiana na jibu alilotoa hapo juu (Natumai ulipata muda wa kusoma post zake zote tatu). Una dakika tano kuandaa na kupost swali lako. Karibu
 
Back
Top Bottom