Kwa kuwa Zitto yupo humu sasa hivi, naamini ataangalia mapungufu yao(Sisiem) yalipo ili CHADEMA wayatumie kama silaha ya kuombea kura, hasa kwenye vipengele walivyoviita "KERO NA MATATIZO". Waangalie kila kata Sisiem iliona kero gani ili na wao wawaeleze wananchi ahadi hewa za Sisiem tangu 2005.Currently Active Users Viewing This Thread: 51 (33 members and 18 guests) Opaque, aflongotiki, Andy2000, Arnold, BabaH, BINTI SAYUNI, Cola, gunge211, jkileo@hotmail.com, Kakunkuna, kicheruka, Kimeo, Kinyamana, kitatange, Kite Munganga, Liganga, majige, mkwegi, mnyalandi, Mr. Zero, Mtindiowaubongo, Mukalabamu, mutua12, Mwananzuoni, njilembera, n_sikana, Pasco, power to the people, Recta, Sebo, tafaboy, TooGood, Zitto
Rev. Kishoka,
Ikiwa hapa JF kuna asilimia 60 (hesabu ya kufikirika) hawaamini kuwa Rostam ni fisadi kwa sababu ati hakuna ushahidi.. Vipi wananchi wa Busanda wanaweza kufikiria kinyume!
Tukubali tu mkubwa yaishe.. NDIVYO TULIVYO!
Asante MMKJJ kwa tathmini yakinifu.Nimesoma majibu yote yaliyotolewa na watu mbalimbali kufuatia ripoti hii ya "kanzi".. Kuna kitu kimoja hata hivyo ambacho watu wanasahau au hawajazingatia umuhimu wake. CCM ni chama cha siasa.
CCM siyo shirika au kampuni fulani, ni chama chenye malengo ya kisiasa. Malengo hayo yanahitimisho moja tu nalo ni kutawala. Mambo mengine yote yanazunguka kwenye hilo moja.
Maana yake nini?
Maana yake ni kuwa CCM wana utaalamu wa kufanya siasa. Ndani ya CCM tangu enzi na enzi wamejifunza suala zima la propaganda na sanaa ya siasa. Tangu enzi za vita baridi CCM imepeleka makada wake Chezch, Yugoslavia, Romania, Urusi na hata Uchina na katika kilele cha kuwaandaa viongozi wake kilianzisha Chuo cha Chama pale Kivukoni (siku hizi kina shughuli nyingine nasikia).
Maana yake ni kuwa CCM kinaelewa maana ya siasa na mikakati ya siasa.
CCM hadi hivi sasa ukisoma vizuri utaona kuwa wame concede Katoro na na mji mwingine, kwenye makao makuu kama walivyofanya Kiteto mjini. Kura za CCM hazitatoka mjini bali vijijini.
Nilizungumza na Mbunge mmoja jana ambaye aliniambia kitu kimoja cha uhakika sana kuwa ushindi wao utakuwa ni wa asilimia 70! Akanieleza reasoning yao kuwa Chadema na CUF (ambao alisema nao wanapata wafuasi wengi tu) watagawana kura za mjini na CCM watakomba kura za vijijini ambako a. CCM inajulikana hata usingizini na b. wapinzani ndio wanaibukia wakati wa kampeni.
Kwa maneno mengine ni kuwa CCM wanajua wapiga kura wao; na hicho ndicho ripoti inasema. Kwamba, pamoja na matatizo yao yote hao wananchi kama yalivyoanishwa wao CCM bado wanaleta tumaini zaidi kuliko wapinzani. ni ya yale yale ambayo yametokea mijini ambapo watu wanaipigia kura CCM na siyo mgombea.
Zitto katika hotuba yake ile iliyowasisimua wengi alikuwa anajaribu kuwapa wana Busanda sababu nyingine ya kupiga kura. Lakini cha kusikitisha ni kuwa mara nyingi ushindi wa namna hii hautokei wakati wa kampeni ni kabla ya kampeni!
CCM wanalitambua hili vizuri na wana utalaamu wa kulifanyia kazi.
Hata hivyo, wapinzani wanahitaji kitu kidogo sana kuweza kubadilisha mwelekeo wa ushindi kwani wao wanahitaji kushinda angalau asilimia 50 za kura za vijijini na kushinda asilimia angalau 60 ya kura mijini basi ushindi utakuwa wao. Nje ya hapo, CCM wakishinda, nitakuwa mtu wa mwisho kushangaa.
Tusione umati kwenye mikutano tukatafsiri kura; vitu hivyo viwili havihusiani!