JF Exclusive: Ka-Nzi kwenye kikao cha kampeni ya CCM, Busanda!

Wana JF,

Namshukuru Mzee Mkjj na ka inzi kake kwa kutuletea hii habari. Lakini kwa mtizamo wangu wa haraka haraka kutokana na minute za kikao naona kuna mapungufu mengi sana sijui ni ya matatizo ya mwandishi au imefanyika makusudi ili kudanganya umma kwa kuisambaza kupitia kwa Mkjj ili kutudanganya (danganya toto waswahili wanasema). Kuna mambo ya msingi hayapo kwenye minute za hiki kikao,

1. Nani alikuwa mwenyekiti!!!
2. Nani alikuwa katibu wa kikao!!!
3. Nini yalikuwa maazimio ya kikao kwa ujumla? Yaani walipokea taarifa kutoka kwenye kata halafu mkutanio ukaisha?
4. Mbona kikao hakikuzungumzia mikakati ya jumla ya kuongeza % ya ushindi?

Ndo maana mi nikasema aliyeandika hii report hajui alichokuwa anafanya, Wizi mtupu...........

Hakuna kitu hapo, wajiandae kufunga virago!
Hakuna simile kwa mafisadi, jamani tumeisha ambiwa enough is eno..

Sasa kama wao wenyewe wanaji eavaluate kwa asilimia 60? si waweke asilimia 80 za kishindo?
 
Ipo wapi ripoti ya tathmini ya vyama vingine?au picha tunazooneshwa zatosha kuwa ripoti?... atleast hawa mafisadi wanakutana na kujadili yao... the so called serious opposition wanafanya nini? au nasi tunasubiri tukishindwa tuseme CCM walishapanga kuiba na kujiwekea 60% ushindi?...

Vyama vya Upinzani vinavyoshiriki lazima wafanye tathmini ikiwa daily or weekly or whatever...Muhim tathmini yao ijenge kuchukua hilo Jimbo.
 
Hapo wakuu naona hicho kikao kinatuambia jambo. Kwanini waseme wanayajua tayari matokeo wakati tukio lenyewe bado?

Pili ni utaratibu gani huu? Nadhani hapa Vyama vingine vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi huu wana haki ya kudoubt na kupinga ushiriki wa CCM katika uchaguzi huu kwa kuwa inaonesha tayari wanajua matokeo, kitu ambacho sidhani kama ni sahihi in any way?
 
Ipo wapi ripoti ya tathmini ya vyama vingine?au picha tunazooneshwa zatosha kuwa ripoti?... atleast hawa mafisadi wanakutana na kujadili yao... the so called serious opposition wanafanya nini? au nasi tunasubiri tukishindwa tuseme CCM walishapanga kuiba na kujiwekea 60% ushindi?...

Vyama vya Upinzani vinavyoshiriki lazima wafanye tathmini ikiwa daily or weekly or whatever...Muhim tathmini yao ijenge kuchukua hilo Jimbo.

- Mkuu chuma heshima mbele sana kwa maoni yako, ninasema hivi nimeisoma hiyo ripoti, naomba mwenye uelewa zaidi ya wangu anisaidie kuona waht is wrong na hiyo ripoti ya kikao, kwani sijaona hata mahali penye kasoro, wamekutana kikao cha kampeni na kutathimini hali halisi ya kampeni yao na kuweka mambo yote wazi,

- Mimi ninaamini huenda hata wameilikisha makusudi kwa sababu hiyo ripoti imekaa vizuri sana kwa maoni yangu, au? Ila kwa anayeelewa zaidi naomba ufafanuzi zaidi of what is wrong na hiyo ripoti?

Respect.

FMES!
 
Percentage za kura zilizotolewa ni utabiri tu na sio kila siku kile kinachotabiriwa hutokea, na bado najiuliza ni kigezo gani kimetumika kupata hivi viwango, sidhani kama kulikuwa na kura za maoni! Cha ajabu pale ambapo wanaona ni maji ya shingo, hawajatoa figure yoyote.
Kali zaidi ya yote ni hii kauli kuhusu Katoro.."Umoja wa vijana ukae imara kuthibiti vitendo vya vurugu vya chama cha CHADEMA", bado najiuliza kwa kutumia njia zipi? kivipi? Hii ndio kazi yao? Polisi hawatoshi? Na fujo zikitokea CCM wanakimbilia kulaumu vyama vya upinzani kumbe giza likiingia wanakusanyika na kuwapa maelekezo vijana wao wajichulike sheria mkononi!
 
- Mkuu wangu labda uweke mfano wa jinsiw alivyovunja sheria so far, yaani ni hilo la muhimu kutoka hii ripoti? Si nimesikia Chadema ndio waliowakamata watu huko Busanda? au?

FMEs!
 
- Mkuu wangu labda uweke mfano wa jinsiw alivyovunja sheria so far, yaani ni hilo la muhimu kutoka hii ripoti? Si nimesikia Chadema ndio waliowakamata watu huko Busanda? au?

FMEs!

Kwanini fujo za Chadema zizibitiwe na Umoja wa vijana? And how? Kisheria ukifanyiwa fujo unaripoti polisi na kuwaachia wao ndo wafanye kazi yao na sheria ichukue mkondo wake.
 
Percentage za kura zilizotolewa ni utabiri tu na sio kila siku kile kinachotabiriwa hutokea, na bado najiuliza ni kigezo gani kimetumika kupata hivi viwango, sidhani kama kulikuwa na kura za maoni! Cha ajabu pale ambapo wanaona ni maji ya shingo, hawajatoa figure yoyote.
Kali zaidi ya yote ni hii kauli kuhusu Katoro.."Umoja wa vijana ukae imara kuthibiti vitendo vya vurugu vya chama cha CHADEMA", bado najiuliza kwa kutumia njia zipi? kivipi? Hii ndio kazi yao? Polisi hawatoshi? Na fujo zikitokea CCM wanakimbilia kulaumu vyama vya upinzani kumbe giza likiingia wanakusanyika na kuwapa maelekezo vijana wao wajichulike sheria mkononi!

Mkuu, nimeshangazwa pia na hesabu hizi za kura, [kama kura zingepigwa tarehe 12/05/2009, CCM ingepata 61.5%] Hawa watu wako serious au? Huenda wanajua namna tofauti ya nguvu ya kura yenyewe.
 
one thing we must appreciate...ni kuwa atleast CCM wanaonyesha wana muelekeo fulani wa kuchambua matatizo na nini kifanyike.....hilo tu pekee ni hatua pekee ya kusolve tataizo na hatimaye wanaweza hata kutathmini na kujua %ges za ushindi
 
Kwanini fujo za Chadema zizibitiwe na Umoja wa vijana? And how? Kisheria ukifanyiwa fujo unaripoti polisi na kuwaachia wao ndo wafanye kazi yao na sheria ichukue mkondo wake.

- Mkuu KNS, fujo za chadema, according to hii habari zimethibitiwa na Polisi kama sheria inavyosema na sio Vijana wa CCM kama unavyodai, wakati mwingine tutumie ushahidi uliopo kuliko imaginations soma hapa chini:-

Viongozi wa CHADEMA wakamatwa Geita

na Edward Kinabo, Geita

[Source: Tanzania Daima]

VIONGOZI wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani hapa, juzi jioni walikamatwa na polisi jirani na kituo kikuu cha mabasi mjini hapa, wakituhumiwa kumshambulia muuza magazeti, Abbas Omari.

Viongozi hao ni Katibu Mkuu wa chama hicho wilayani Geita, Rogers Ruhega (34) na Katibu wa Kata, Paul Vincent (33), ambao walikamatwa wakidaiwa kumshambulia muuza magazeti huyo katika eneo lake la biashara.

Muuzaji huyo wa magazeiti alifungua RB namba GE/IR/1055/2009 katika kituo kikuu cha polisi wilayani Geita, akielezea kushambuliwa na viongozi hao.

Viongozi hao wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, jana asubuhi, walisema chanzo cha tukio hilo ni kunyofolewa kwa habari zinazohusu wasifu wa mgombea ubunge wa CHADEMA, Jimbo la Busanda katika gazeti la Tanzania Daima Jumapili
.
 
Mwanakijiji,

Je inawezekana CCM wanajivunia kitu ambacho sisi tunakataa kuamini au kukikubali?

Katika kila kata, pamoja na malalamiko kuwa kuna shida, CCM bado wanajihakikishia ushindi wa Asilimia si chini ya 60 (60%). Je ina maan akuwa hawa 60% wameridhika na hali walizonazo pamoja na kulalamika na wako tayari kuendelea kuipa CCM hatamu?

Je ni kipi na wapi tunapokosea tunapopigana vita dhidi ya Umasikini, Ujinga na Maradhi na hata tukiongeza Ufisadi katika safari ya kujitegemea na kujiletea maisha bora, ikiwa 60% wanaridhika na uongozi ulioko ingawa bado wanalalamika kuwa hawapati mahitaji ya muhimu na lazima?

Ni kitu gani ambacho kinamfanya Mtanzania huyu (60%) ashindwe kubadilisha mawazo na hata kugoma kuendelea kupigia kura chama na Serikali ile ile ambayo inashindwa kuboresha maisha yake?

Jee ndivyo tulivyo?

Kwa nini basi nasi tuendelee kuburuzwa na hawa 60% walioridhika na Umasikini na Ufisadi?
 
Rev. Kishoka,
Ikiwa hapa JF kuna asilimia 60 (hesabu ya kufikirika) hawaamini kuwa Rostam ni fisadi kwa sababu ati hakuna ushahidi.. Vipi wananchi wa Busanda wanaweza kufikiria kinyume!
Tukubali tu mkubwa yaishe.. NDIVYO TULIVYO!
 
Sasa kama wao wenyewe wanaji eavaluate kwa asilimia 60? si waweke asilimia 80 za kishindo?

Kaka,

Hizo figa haziwekwi tu kama tombola; wao wana data ya waliojiandikisha, wana data ya nani yuko upandewao, na wana mipango kazi iliyowafikisha kwenye tathmini hiyo... ni jambo la kawaida kazi yoyote kupangwa na kukadiriwa achievement!! Their technical evaluation gave them the percentage, and they have shown a litle bit of quality by approaching huo uchaguzi kwa facts.... Ni mfano wa kuigwa na tuwe makini kutumia data kupanga; si ajabu walianzia katika mashina hivyo wanajua katika kila shina wangapi ni potential voters na affilitations zao kisiasa

Wanachotakiwa kuangalia ni namna ya kuendelea kuwashikilia hao 61% wasiteleze kutokana na sera zao potofu... Kumbuka Mrema alibebwa halafu akatupwa chini kama kiroba na kura za wabebaji wake

Hata vipima joto dunia nzima hutumumia mbinu kama hizo kupima temperature
 
Mwanakijiji,

Je inawezekana CCM wanajivunia kitu ambacho sisi tunakataa kuamini au kukikubali?

Katika kila kata, pamoja na malalamiko kuwa kuna shida, CCM bado wanajihakikishia ushindi wa Asilimia si chini ya 60 (60%). Je ina maan akuwa hawa 60% wameridhika na hali walizonazo pamoja na kulalamika na wako tayari kuendelea kuipa CCM hatamu?

Je ni kipi na wapi tunapokosea tunapopigana vita dhidi ya Umasikini, Ujinga na Maradhi na hata tukiongeza Ufisadi katika safari ya kujitegemea na kujiletea maisha bora, ikiwa 60% wanaridhika na uongozi ulioko ingawa bado wanalalamika kuwa hawapati mahitaji ya muhimu na lazima?

Ni kitu gani ambacho kinamfanya Mtanzania huyu (60%) ashindwe kubadilisha mawazo na hata kugoma kuendelea kupigia kura chama na Serikali ile ile ambayo inashindwa kuboresha maisha yake?

Jee ndivyo tulivyo?

Kwa nini basi nasi tuendelee kuburuzwa na hawa 60% walioridhika na Umasikini na Ufisadi?

Rev,

Wananchi bado tunaamini kama MAFISI (sorry to use this word) vile kwa mkono wa Binadamu.........kwamba siku moja vile vijisenti vya akina Chenge vitatusaidia...........hiyo kumpoteza Chenge maana yake we won't get that "HAND"............

sasa basi ni kazi kwangu, kwako kuwaelimisha wananchi kuwa.....lets fight to get our "HAND" back and protect it for our own benefit and for the future generation..........
 
Wakuu mimi nimeshindwa kuipata ripoti. naona inaniambia iko damaged and cant be repaired.
 
Mkuu Mwanakijiji,kuna mawili hapa,muhtasari huu unaweza kuwa genuine au ikawa ni deliberate leak ya ku mis inform watu hasa kwenye jamvi tukufu la JF.Napenda niamini kwamba ndani ya JF kuna wana CCM wazoefu wa valangati za uchaguzi,hao naomba watusaidie kwanza watueleze nini maana ya CP,huwa inahudhuriwa na nani na katika mazingira yapi,na kwa kawaida on average huwa na wajumbe wangapi na kipi hasa huwa kinaongelewa.Binafsi I doubt kama huwa ni kuongelea data na statistics,they must be discussing something bigger and deeper and could be hata minutes hawaandiki katika kutafuta ujanja wa ushindi,ma analyst twambieni maana naamini mmejaa humu ndani ya JF.
 
Uzuri ni kwamba mambo Tanzania hayakuharibika ghafla yalianza kuharibika taratibu na yanaendelea kuharibika taratibu na kufanya waliowemgi kuendelea kuona kila kitu ni shwari.
Matatizo ya Tanzania ni sawa na kubeba kiroba cha mchnga cha kilo 30 au godoro la sponchi wakati wa mvua. Kila hatua upigayo mchanga unayonya maji na kuongeza uzito bila wewe kutambua. Utatambua tu pale mchanga ukishiba maji na kuanza kuchuruzisha maji kwamba hujabeba mchanga tu bali umebeba rita zaidi ya 15 za maji.
Nchi zilizo pata Uhuru na kutumia Uhuru wao kuleta maendeleo ya wote viongozi wake waliwabebesha wananchi wao magunia ya sukari na chumvi katika safari yao ya tufani ya mvua. Mwisho wa safari hakibaki kitu kwani kila tone la maji sharti liondoke na uzito wa mzigo na si kuongeza mzigo.

CCM wakiweza kuondoa kero za watu walio nyimwa ulaji walioahidiwa kwenye vikaoa vya siri ni kweli watashinda.
Huko vijijini watu wengi wanauona uchaguzi kama msimu wa kuokota kumbikumbi au nzige, ni kitu cha kupita kama hukupata nzige wa kutosha subiri wakati mwingine.
Wengi pengine hujiuliza kwa nini CCM wanakwenda kupoteza muda huko na kulalama badala ya kuchagua mtu wamtakaye na kwenda kuwatangazia kisha kuwagawia hizo kofia na Tshirt.
Wengi hawaamini kwamba uchaguzi ni kitu cha kudumu, kwa hiyo kwao matokeo ya uchaguzi huisha baada ya mshindi kutangazwa na hayaendelei siku zote za maisha yao.

Ushindi wa 60% watapata tu endapo juhudi za kuwabana wale walofumbuka macho wasilete zao za kuleta na kuvuruga ushindi wap na juhudi za kufuta kiporo kwa kuwapa malimbikizo ya Tshs 10, 000 za 2005 na 15,000 za msimu huu zitazaa matunda.
Ahadi ni deni bila kujali sheria wala taratibu.

Maoni.

Huko Busanda Ushindi wa CCM unaweza fikia 85% iwapo CCM watabadili mbinu na kuamua kuanza kugawa Suruali nyeusi na mashati ya kijani kama lili la Rostamu na Malecela kwa kila mtu pale Busanda, viatu siyo muhimu kwa sasa labda 2015. Kwa akina mama wawape khanga za Urafiki siyo zile za India.
Wakiweza wawape na za ndani pia, yaani chupi, zenye nembo ya chuma ya Jembe na Nyundo kama nembo ya ile chupi maarufu ya enzi zetu ya 007 ya James Bond. Watengeneze za rangi mbalimbali ili watu waweze kuchagua rangi wanayotaka ili mradi tu rangi hiyo iwe kijani.
CCM wanaweza kuwa ni chama cha kwanza Duniani kushinda uchaguzi baada ya kugawa za ndani na jina la chama chao kuingizwa kwenye kitabu record za dunia cha Bia ya Ginesi.
 
Last edited:
Mkuu Mwanakijiji,kuna mawili hapa,muhtasari huu unaweza kuwa genuine au ikawa ni deliberate leak ya ku mis inform watu hasa kwenye jamvi tukufu la JF.Napenda niamini kwamba ndani ya JF kuna wana CCM wazoefu wa valangati za uchaguzi,hao naomba watusaidie kwanza watueleze nini maana ya CP,huwa inahudhuriwa na nani na katika mazingira yapi,na kwa kawaida on average huwa na wajumbe wangapi na kipi hasa huwa kinaongelewa.Binafsi I doubt kama huwa ni kuongelea data na statistics,they must be discussing something bigger and deeper and could be hata minutes hawaandiki katika kutafuta ujanja wa ushindi,ma analyst twambieni maana naamini mmejaa humu ndani ya JF.
ma-analysts gani unawataka wakuambiye zaidi ya hao ambao wameshachambua hapa tayari?
kila kitu/kazi inakuwa guided na data na statistics hakuna kingine, kama ulikuwa hujajua!
issues za nani apewe shi-ngapi na nani shi-ngapi huwezi kutegemea ikawekwa kwenye minutes, wanajua yaweza ku-leak kama hivi, kibarua kikaota nyasi sio!
hiyo ndiyo hali halisi.
 
Back
Top Bottom