JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

..Labda tuwajibu wale wanaosema kuwa hawaoni kitu kwenye attachments za invisible.....

..kwa wanaofatilia kwa makini sakata hili watakua wamebaini kuwa hawa PAP waliolipwa pesa za escrow tayari si wamiliki halali wa IPTL bali ni matapeli...

..Ni matapeli kwa kuwa tayari wamegundulika kuwa wamefoji hati miliki ya 70% share za mechmar ili waweze kuchota hela za escrow...Wamefoji hatimiliki hiyo kwa kuonyesha TRA kuwa eti wamenunua 70% ya share za mechmar (aliyekua mmiliki halali) kwa sh. mil.6 tu toka kwa piperlink.....yaani sh.mil.6 kununua 70% ya share zote za IPTL(pamoja na mitambo yote!!)..

.Piperlink ni kampuni iliyodai kukabidhiwa jukumu la muflisi wa mechmar...Hawa piperlink nao hawana hti miliki ya share za mechmar kwani walinyang'anywa miliki hiyo kwenye kesi kule Virgin islands baada ya kugundulika kuwa walitaka kumiliki share za mechmar kitapeli.....na hivyo mahakama ikaamuru kuwa ati miliki hiyo wapewe SCBHK waliokuwa wanawakopesha hela IPTL wakati huo.....

..that said..kwa kwa kuwa imethibitika kuwa PAP si wamiliki halali wa IPTL....maana hata hizo 30% ya share walizowalipa VIP(kina James Rugemarila)zimetokana na pesa walizolipwa na BoT baada ya pesa za escrow kukwapuliwa nao...


..Sasa basi..hata nyaraka PAP walizosainishana na serikali(GoT)...yaani ile agreement ya release of funds na pia ile indemnity deed (kinga ya madai)..zoote hizi zinakua batili automatically na hazina nguvu ya kisheria tena....maana hawa PAP si wamiliki halali wa IPTL...na kwa mana hiyo hata makubaliano yao na serikali yanakosa uhalali wa kisheria automatically..

..that said...ile wanayodai ni kinga kwa serikali (indemnity)haitakua na nguvu ya kisheria panapo madai .....maana aliyesaini deed(yaani PAP)tayari kagundulika ni tapeli.....sasa umeona wapi tapeli/mwizi anatoa kinga ya kisheria kwa anaemtapeli????...kama imefika mahali watu wanasema hawa PAP wakamatwe na mitambo itaifishwe....watapataje hawa nguvu ya kisheria kwa madai kwa serikali??

...that said...kutokana na yote hapo juu..tayari SCBHK(kupitia wanasheria wao) wameshawaandikia tanesco wakiwapa siku 30 wawe wamerudisha pesa yote kwenye escrow account..maana wamegundua kuwa tanesco wamevunja makubaliano ya mkataba wa awali walipofungua escrow account...kwamba tanescow wamekubali pesa ya escrow kulipwa kwa third party (PAP)ambae hatambuliki kwenye mkataba wa awali wa ufunguzi wa acc. hiyo...


....Angalizo..... kuna watu kama Muhongo na Maswi...wamekua wanabeza ushiriki wa SCBHK kwenye sakata hili ....huku wakisahau kuwa hawa SCBHK ndio wamepelekana na tanesco hadi Mahakama ya kimataifa kuhusu tarrifs za umeme wa IPTL...leo eti kina Maswi wanasema hawawatambui???haya ni maajabu mengine ya watendaji hawa wa utawala huu....

.....Labda niwahoji wanaowatetea hawa PAP....kwamba PAP walikuja TZ na mtaji kiasi gani ili wainunue IPTL iliyokuwa na matatizo??mana tunaambiwa eti hawa PAP ni wawekezaji...mtuambie je walikuja TZ na mtaji kiasi gani ili kununua hisa zote za IPTL iliyokuwa na mgogoro???


.jibu hamtakua nalo aslani....maana PAP hawakuja na mtaji TZ..bali walipanga wapige hela za escrow ndipo wazitumie kununua hisa za IPTL...na wamefanikiwa kununua 30% ya hisa za kina Rugemarila(VIP) kwa kutumia hela ya escrow waliyolipwa na BoT. ...Huu ni utapeli wa kiwango cha juu..


....PAP wameshindwa kuzipata kihalali 70% share za mechmar....kwa kuwa walikosa hati miliki halisi....ikabidi wafanye forgery ili wachote hela BoT....napo wakafanikiwa....Lakini sasa wamebambwa...


,....Tutafakari...huu mchezo waliofanya PAP ni kama ilivyokua kwa Richmond..methodology za wizi wao hazitofautiani sana...

Unapiga porojo kama vile sisi hatujui kusoma? hati ya dhamana imetolewaa na IPTL, kasome tena juu.

Umeulizwa Mechmar hawakuwa hata na mlinzi kwenye mali na mitambo yote hiyo? umekwepa kujibu.
 
Unapiga porojo kama vile sisi hatujui kusoma? hati ya dhamana imetolewaa na IPTL, kasome tena juu.

Umeulizwa Mechmar hawakuwa hata na mlinzi kwenye mali na mitambo yote hiyo? umekwepa kujibu.

...chu.pi zimewabana eh!!na bado....mi huwa sijibu post zako kibaraka wa majizi....I will keep on ignoring dogs like you...
 
Hakuna lolte,mihela yote TANESCO inayovuna kutoka kwa wananchi ni ya kwao.Hizo ndizo mbinu zenyewe.
Ukifuatilia kwa makini haya madudu utashangaa nani ni mmiliki TANESCO. Hii taasisi imekuwa kama mbuzi wa jalalani. Yaani serikali inajiweka nayo mbali kabisa kama haiihusu!!!
 
We waache wajidanganye lakini mwisho wa siku UKWELI utajulikana tu,ifahamike Kuwait hili sakata la IPTL limeibuliwa muda muafaka!
 
Kiukweli hili suala la escrow bwana mkubwa linamhusu moja kwa moja kwani haiwezekani na wala haingii akilini kwa kiasi kikubwa cha pesa kama hiki kupigwa ndani ya nchi na rais wa nchi anatolea maelezo mepesi tu ya kuwa yeye haelewi mambo hayo kama alivyosema siku alipokuwa anawahutubia wanachi pindi alipowasili uwanja wa mwalimu JK Nyerere.

lakini pia napata shida kubwa sana pale niliposikia taarifa ya jana ya kuwa serikali bado wanaendelea na uchunguzi na pindi utakapokamilika hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika, kwangu mimi napata shida katika hili kwani uchunguzi wa suala hili ulishafanywa na CAG na TAKUKURU lakini leo serikali wanasema wanafanya uchunguzi swali langu ni je huo uchunguzi unaofanywa na serikali unatumia vyombo gani hasa?

Na kama wanawatumia TAKUKURU wale wa mwanzo walifanya kazi gani? au ndo utaratibu wa kufunika kombe kuruhusu mali ya wananchi kuliwa na watu wachache
 
Ccm ni chama cha wezi wanao subiri kupigwa mawe
 
Inahitaji tuweke "utanzania" kando ili kuwa na ujasiri huu.

Kuna pipeline huko watu wamepiga dola bilioni moja wamegawana, habari ikija kubumbuluka wabongo watazimia.Hizi habari za escrow zitaonekana kama pesa ya kumpa mtoto anunue njugu.

Pia watu wanachimba mafuta off of Mtwara mwaka wa pili huu, sie tunaambiwa wanafanya "exploration".
 
Kuna pipeline huko watu wamepiga dola bilioni moja wamegawana, habari ikija kubumbuluka wabongo watazimia.Hizi habari za escrow zitaonekana kama pesa ya kumpa mtoto anunue njugu.

Pia watu wanachimba mafuta off of Mtwara mwaka wa pili huu, sie tunaambiwa wanafanya "exploration".

Shenzi zao kabisa ngoja mpaka shetani atawahukumu
 
Back
Top Bottom