JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

Kuna pipeline huko watu wamepiga dola bilioni moja wamegawana, habari ikija kubumbuluka wabongo watazimia.Hizi habari za escrow zitaonekana kama pesa ya kumpa mtoto anunue njugu.

Pia watu wanachimba mafuta off of Mtwara mwaka wa pili huu, sie tunaambiwa wanafanya "exploration".

Hiyo ya kuchimba mafuta nilishaipata siku nyingi,tukaongeaongea humu na akina Pasco lakini wapi,exploration ya deep sea Tanzania itawezea wapi kufuatilia?!
Ila Kiranga utakuwa umekosea,ni dola Bilioni au?!
Umeconvert hii value into tsh mkuu?nasikia jasho jembamba!
 
Last edited by a moderator:

Shilingi bilioni moja hela ya mtoto wa Rugemalira kufanya shopping ya weekend tu hiyo.

I am talking USD.
 
Last edited by a moderator:
Sasa Mkuu Invisible tuwekee dude lote basi na Annexture zake usisahau page xote na zile zilizonyofolewa...mkuu wa nchi si kasharuhusu liwekwe hadharani? Litatufaa sana kwa reference
 
Mwenye ukurasa huo nauomba tafadhali!

Rejea: "Kufuatia kupokea nyaraka hizo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa Ripoti ya CAG iwekwe hadharani kwa ajili ya umma kuweza kuisoma na kujua nini hasa kimesemwa na kupendekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Rais Kikwete ameelekeza kuwa Ripoti hiyo itangazwe kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi na kwenye mitandao ya kijamii, ili Ripoti hiyo iweze kupatikana kwa Watanzania wengi" - Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais [9 Desemba 2014]
 
Asanteni, nimeshaipata, kumbe ni zile za wakati ule tulizoambiwa zimenyofolewa!

Ndugu Invisible , tafadhali ziweke pamoja hapo kwenye ukurasa wa kwanza kabisa na sio huko katikati au uziunganishe kabisa na ripoti yote kwenye ambato maana hazimo humo (i.e. ukurasa wa 14 na 24 na pengine zile zingine za mwisho ambazo bado sijazifikia nazo hazimo)
 
Fuatilia post #12 na #19 Invisible aliziweka mapema tu kipindi kile
 
Last edited by a moderator:
Wakati kukiwa na taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari kuwa akaunti ya escrow iliyofunguliwa benki kuu ( BOT ), kwa mujibu wa makubaliano yaliyofanyika julai 5, 2006, zilikuwa sh bilioni 306.6, kabla kutolewa kwa fedha hizo mwaka 2013, taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ( CAG ), imethibitisha sio kweli.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya CAG , ambayo Rais Kikwete ameagiza iwekwe hadharani, ili Watanzania waisome na kuielewa, katika ukurasa wa 40 mpaka 42 imebainika kuwa kiasi cha fedha kilichokuwa katika akaunti hiyo, kilikuwa Sh bilioni 182.7. Ambapo TANESCO iliweka kiasi cha sh bilioni 142 na wizara iliweka sh bilioni 40.7, taarifa hiyo ilieleza.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa, kama akaunti hiyo ingekuwa na sh bilioni 306.6 basi TANESCO wangepaswa kuweka kiasi cha sh bilioni 123.9 zaidi ya fedha zilizowekwa katika akaunti hiyo.

Kutokana na hali hiyo, mpaka sasa IPTL inaidai TANESCO sh bilioni 123, ambazo ni nyingi kuliko kodi ambayo TRA inaidai IPTL, ya sh bilioni 26.9.
 
hatuiamini serikali tena, haya ni majizi tu hayasafishiki. Tutakula nao sahani 1
 
Back
Top Bottom