JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

Wee ni mpuuzi kweli. Wana exemption ya tax wangeenda kunegotiate?. Umevurugwa wewe.

Naona sasa unaanza kuhororoja, soma vizuri hapo juu, au nirudie?

Hayo ni maneno ya Mboma kwenda Wizarani, na ni kitu cha kawaida kabisa, kuonesha unachotakiwa kulipa ni hiki, na hiki ni kodi.

Sasa hapo Wizara ndiyo intakiwa kulipa hiyo kodi au kama wataisamehe basi itabaki hukohuko kwao, kwa maana nyingine, hata ukiletewa invoice leo hii, unaoneshwa unachodaiwa bila VAT na unaoneshwa unachodaiwa na VAT, sasa kama wewe una exemption ndiyo unaipeleka si muuzaaji.

Hebu fikiri japo kiduchu. Mlipa VAT ni mnunuzi si muuzaji na muuzaji akikupa Invoice anabainisha hilo.

Hivi jamani hizi shule huwa mnaenda kufundishwa ujinga?
 

Umenizalilisha mkuu... Ila ngoja utaona nilichomaanisha. kwa hizo nondo narudia ni ngumu kumeza... sijashawishika. anyway kwa vile invisibo anaziunga mkono ngoja basi woote tukubali tu kwamba ni nooma!!
 
Mkuu suala hilo halichanganyi kabisa. Intaegemea unaliangalia kwa jicho gani na upana upi.

1)Kuna fedha za umma za wazi zilizoibiwa(direct or indirect)

2. Kama si fedha za umma, kuna masilahi ya umma yametumika au kutumiwa kwa jambo lisilo la umma(endapo tutakubaliana si suala la umma)

3) Kuna ukiukwaji mkubwa sana wa maadili. Iweje suala lisilola umma(kama tunakubaliana) liwahusishe vingozi wa ngazi za juu, moja kwa moja au kwa kupitia?

4)Kama umma hauna masilahi, kwanini kuna kujuhudi za kuficha suala hili kwa kutumia ofisi kama za waziri mkuu, mwanasheria mkuu, Ikulu(kupitia katibu kiongozi n.k.)

Kubwa Zaidi jiulize, kama umma hauna masilahi, kwanini taarifa isiwekwe wazi ili serikali ijisafishe? Kwanini kuna dana dana nyingi zisizo na kichwa wala miguu, tena zingine zikihusisha taasisi nyeti kama mahakama?

Sio suala la pesa tu, hili ni corruption. Hebu angalia corruption ni kitu gani halafu uje utuambie wapi kuna confusion katika suala hili.
 
mimi wanyofoe kurasa zoooote ila watakazo ila nataka kuona majina yote ya walioiba fedha hizi! a to z... izo mbwembwe zingine walaaaah... nataka nione majina tuuuh.... shenxi kabisa hawa
 

Kijana, kasema hizi ndio zilizonyofolewa, ni nini usichokielewa hapo?

Ripoti ipo, wala hilo silikatai, ila nnachosema mbona hii iliyowekwa hapa sioni wizi wowote? Na hii ndiyo ilisemekana imenyofolewa kwa kuwa ina mambo makubwa ndani yake?
 
Halafu mijizi yenyewe mingi ni mikristo, huyu Fox ameshakuwa kibaraka wa wakatoliki.

Matola, umeamua kubadili mada naona. Yaleyale ya ccm na babu wa loliondo. Hutaweza mkuu, acha watu waendelee kuchakata ESCROW na si UDINI.
 
INVISIBLE. Wengi tuna hamu ya kujua kilichoko ndani ya ya ripoti ya uchunguzi ya CAG. Tunaomba utuwekee hapa ripoti nzima ukurasa kwa ukurasa na tuwaone hao wanyofoaji wataishia wapi?
 

I recon, kama mzigo wa pages zilizoibwa ni hizi zilizomwagwa hapa basi watakupa wameiba placebo! Invisible tafadhali fafanua!
 
naomba mtu wa 37 awe ni mwana JF, kwani nchi hii inamilikiwa na watu 36 tu?
 
Kijana kasema hizi ndio zilizonyofolewa, ni nini usichoielewa hapo?

Ripoti ipo, wala hilo silikatai na nnachosema mbona hii iliyowekwa hapa sioni wizi wowote? Na hii ndiyo ilisemekana imenyofolewa kwa kuwa inamambo makubwa ndani yake.

By lusungo

Soma vizuri ikibidi urudie huku umetuliza akili kuanzia hapo kwenye tahadhari ya TANESCO.... makubaliano Kati ya IPTL na TANESCO juu ya kiasi gani kilipwe halafu tafuta kiasi kilicholipwa baada ya makubaliano hayo then tafuta Kama kodi halali ililipwa.....

Inahitaji fikra ya juu kuelewa kilichomo humo Kama ndo mwenzangu na mie Wa nyimbo za kitorondo utaambulia patupu.....

Usione watu wazima wapo busy mpaka wanakosa usingizi ukadhani ni mambo mepesi....



sina la kuongezea!!!
 
Hii nchi ilishazikwa kilwa miaka ya 60 huko,na hii TAnzania iliyopo ni msukule tu,mbona kuna makubwa zaidi yaa hilo

Fukuto la bomba la gesi ndio balaaaaaaaaaaaaaaaaaa..........
 
Invisible bana! Nikikwambia una-Troll sijui utanipiga ban au utaniachia.
 

Si mchezo,,, lugha ya mkoloni noma.... Kumbe siijui hii lugha.. yaani sijaelewa kabisa!!!
 
Na wewe unakuwa mtu wa kuingizwa mkenge kirahisi.utajuaje ripoti imechomolewa kabla ya kusomwa?je ikisomwa yote si utajishushia hadhi?ungeacha wanyofoe halafu umwage ndio ungeonekana shujaa



Invisible
Hajakosea chochote ila ametoa tahadhari tu kuwa wanachofanya au kama wamedhamiria kukifanya waache ripoti ipo kwa watu,waache bunge lifanye yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…