Uko huko Facebook WoS?
Wakati mwingine huwa nadhania ni mimi tu ambaye siko huko...
Tushakosa vya kujadili sasa, tunalinganisha Social Network na Forum?
Kuna watu wanashinda Facebook na kuna watu wanashinda JF? Tofauti ni nini?
Wewe ndo huna cha kuchngia.Wote wliochangia ni wajinga siyo? Haya mwenye akili leta vya kuchangia.
Umejaribu TWITTER?Kwa muda mfupi nilioshiriki hapa JF, nimeona kama hapa ni pazuri kuliko kwenye FACEBOOK.
Hapa JF, mada huchambuliwa kwa umakini mkubwa.
Taarifa muhimu hupatikana kwa haraka sana.
Members wana takwimu za kila aina.
Hapa JF hapajakaa kihuni huni.
Members wa JF, wanatunza heshima zao.
Sasa nitaanza kuwajibika kuiendeleza forum hii.
BIG UP waanzilishi wa JF.
Uhuni wa facebook ni upi? JFHapa JF hapajakaa kihuni huni.
Mkuu jina lako limenivutia sana KYACHAKICHE! ungekuwa mchezaji 'one day' mtangazaji angekata ulimi,.... kama ndiyo unakata chenga na mtangazaji anakutaja mfululizo!! Kyachakiche, Kyachakiche,Kyachakiche,Kyachakiche.....x10!
Lakini safi sana mkuu! hongera, napenda sana majina ya kiafrika.
Exaud:MZIZI,
Kweli hili jina la KYACHAKICHE liko kama KITANZA ULIMI (tongue twister).
Exaud:
Mbona ni jina la kawaida sana mkuu! Hebu ona hili " ITETEI LYA KITEE"