Jeshi latanda Mjini Songea

Updates...


Risasi zaanza kusikika katikati ya Mji.
 
Nimepita na bodaboda naona njia nzima za mjini kuna wanajeshi wenye silaha na magari mengi sana, naambiwa njia ya Namtumbo wameweka road blocks za kutosha, Ruhuwiko kule kuna bodaboda wamesimamishwa, mbele ya hospital ya mkoa (Homso) zimepaki defender za kutosha zenye bendera nyekundu, kila anayehisiwa vibaya anasimamishwa hasa wa magari anasimamishwa na kuhojiwa/kupekuliwa...nasogea karibu na bank ya NMB naona wameanza kupiga mabomu ya machozi sijajua chanzo, nimeamua kusogea Mambo Leo kidogo kula, nitarudi mjini baadaye kupata taarifa kamili.
 

nipo mtini
 


Mkuu nipo vijana Pub nimetulia tu, hakuna anayependa kuzurura nje kwa sasa, hali ni tete...
 

Mbinu za kijeshi za kizamani old fashioned za Marne ya 19
 

Ok! Kidogo umeeleweka Mkuu, mimi nipo nje ya mji, nimeingia JF ndo nikakuta hii mada
 
Hakuna vita tz.wanakaa bure mpaka wanakuwa wambeya nao . Kama plisi ! Hayo ni mazoezi wasije kuzidi kuoza.
 
Huwa mnasema Nchi haitakalika (MBOWE), sasa hayo manyunyu tu mlishakuwa na hofu ahhahhhah??? Usiogope kijana tuko kwenye mazoezi ya kawaida

Cargo;
Weye ni cargo kweli kweli tena ya ndizi mbivu zilizoshaanza kuharibika. Kila kitu lazima umtaje Mh. Mbowe. Wadhani risasi zikirindima ni UKAWA tu watakufa au kukimbia hovyo. Unahitaji maombi na maombezi makali ka yale ya kwa Gwajima yakuondoe holo Sukule lililo akilini mwako. Tena naliona kwenye paji la uso. Maccm yakiisha kupokea buku saba huwa yanawehuka.
Ndo maana mkawatuma policcm kuua huko njombe ati kuwatishia watu wasiishi kwa raha zao. Nyinyi ptuuuu. Ati wako kwenye mazoezi, mazoezi mjini? Adui anakaa mjini?? Weye ni mji.nga, tena mjingerer, tena mjingestiiiiiii. Umeniudhi sana
 
Kwa taarifa nilizo zipata toka kwa moja ya rafiki yangu ambae mi mjeda kule songea kaniqmbia ni kwa sababu ya mapungufu yaliyo jitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kula kuna kasoro zimetokea hivo imeleta sinto fahamu na kupelekea wanainch kutaka kuandana hivo serikali imepeleka jesha kusambalatisha vikundi vya aina yoyote kuepuka vurugu.
 

Ila hakukuwa na ishara yoyote ya maandamano, imebakia kuwa siri ya Jeshi hakuna anayefahamu.
 
wanajiandaa na possibility ya urban warrfare october
 
Umeongeza chumvi bodaboda zipo kama kawa na mambo yanaenda kama kawa ila ni kweli jwtz wapo wengi mitaani
 
Taarifa ambazo nimezipata sasa hivi ni kwamba hayo ni mazoezi ya kawaida ya JW ikizingatiwa kuwa tunakaribia kabisa miezi ya kampeni ns uchaguzi hapo Octoba. Najuzwa kuwa kuna kundi la watu ambao wa ni JW waliigiza kama raia wanao andamana na ndipo wakavamiwa na JW wenzao walio full combat na silaha za kivita kwa lengo la kuwadhibiti wandaamanaji. Kwa bahati mbaya pia inasadikika kuna mama lishe mmoja alipata msituko na alizimia na akakumbizwa hospitali ya mkoa.
My Take: Kama hayo tunayo ambiwa yakawa ni ya kweli ni kwa nini JW lifanye mazoezi ya silaha za kivita maeneo ya mjini na kibaya zaidi pasipo kutoa taarifa za awali kwa wananchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…