Jeshi la wananchi Egypt lampindua Rais Morsi

Jeshi la wananchi Egypt lampindua Rais Morsi

Siasa za Misri wanazijua wao hata sijui huwa wanataka nini toka enzi za kina Sadat.

Kama wewe hujui wanachokitaka wao watakuwa wanajua.

Kama sie wenyewe hata hatujui tunachokitaka nchini mwetu tutajuaje wanachotaka watu wengine kwenye nchi zao?
 
Hongereni sana wananchi wa misri kwa kazi nzuri sana mliyofanya..
 
;......... what goes around....... comes all the way .... ???????
 
What if Morsy akikomaa?

unajua maana ya mapinduz ya kijeshi.utakomaa wakat jeshi limechukua nchi tayari na jamaa amekatazwa kusafiri nje yeye na wenzake kuna mashtaka asuburi kufunguliwa. ilo ndio jeshi la wananchi
 
Generali Abdul Fatah Khalil Al Sisi ndie Mkuu wa majeshi ya nchi hiyo na mwenyekiti wa SCAF yaani baraza kuu la vyombo vya ulinzi na usalama.

Pia yeye ni waziri wa Ulinzi wa Misri.

Al Sisi pia ni Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Misri.

Raisi wa Misri yeye ni Kamanda mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama.
 
Hapana Mkuu. Jeshi au mapinduzi yoyote yakishachukua TV au radio ya taifa ina maana kuwa serikali inayopinduliwa haina tena means ya kufanya mawasiliano na ulimwengu. State house ni jina tuu, what matters ni kuteka means zote za communication.

Nimekusoma mkuu
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ndugu wanajf.

Kuna taarifa kuwa Jeshi la nchi ya Misri limemvua madaraka Rais na kutangaza kuwa Mwanasheria mkuu atashika hatamu za uongozi kwa sasa

Yeyote mwenye taarifa kamili atuhabarishe tafadhali..


WAPI TANZANIA???????
 
Hatimaye Rais wa Misri ndugu Mohamed Morsi amepinduliwa na jeshi la nchi hiyo,Jeshi limesitisha katiba na kumvua madaraka rais huyo,Limetangaza mwanasheria mkuu kuchukua wadhifa huo kwa muda,

source:Aljazeera,Press Tv,BBC World,DW
 
Siasa za Misri wanazijua wao hata sijui huwa wanataka nini toka enzi za kina Sadat.

mkia wa mbuzi unapiga pale unapofikia, na uwezo wa akili yako ni mdogo uwezi kujua mambo makubwa kama haya! Kule amna kujipendekeza au kuchukua buku 7 lumumba!
 
Ni kweli ila kuna mengi ya kujifunza hasa tukiiangalia katiba mpya. Pale Jeshi linapokuwa chombo huru kutoka kwenye kamba za siasa na likiwa na nidhamu huwa linapaswa kufanya kazi hii. Chanzo kikubwa ukiacha siasa za Morsi za majivuno, ni kitendo walichokifanya polisi kuuwa raia wake wenyewe?!! What a mess up!

Afrika hakuna kujifunza kutokana na makosa ya jirani au makosa ya nyuma hata siku moja! Watawala wa kiafrika huwa wanadhani yanayowakuta wenzao ni isolated cases, kwamba wao hayawahusu!
 
Egypt army commander suspends constitution

2013-07-03T192006Z_265182390_GM1E974090P01_RTRMADP_3_EGYPT-PROTESTS.JPG

.


26 minutes ago
Politics



CAIRO (Reuters) - The head of Egypt's armed forces issued a declaration on Wednesday suspending the constitution and appointing the head of the constitutional court as interim head of state.

In a televised broadcast, flanked by military leaders, religious authorities and political figures, General Abdel Fattah al-Sisi effectively declared the removal of elected Islamist President Mohamed Mursi.

Sisi called for presidential and parliamentary elections, a panel to review the constitution and a national reconciliation committee that would include youth movements. He said the roadmap had been agreed by a range of political groups.
(Reporting by Yasmine Saleh and Tom Perry; Editing by Alastair Macdonald)
 
Hatimaye Rais wa Misri ndugu Mohamed Morsi amepinduliwa na jeshi la nchi hiyo,Jeshi limesitisha katiba na kumvua madaraka rais huyo,Limetangaza mwanasheria mkuu kuchukua wadhifa huo kwa muda,

source:Aljazeera,Press Tv,BBC World,DW
jeshi litamvuaje madaraka rais huyo aliechaguliwa kidemokrasia?
 
Hatimaye Rais wa Misri ndugu Mohamed Morsi amepinduliwa na jeshi la nchi hiyo,Jeshi limesitisha katiba na kumvua madaraka rais huyo,Limetangaza mwanasheria mkuu kuchukua wadhifa huo kwa muda,

source:Aljazeera,Press Tv,BBC World,DW

Hiyo ndo nguvu ya umma, viwazi wa lumumba mpo hapo?
 
Kama wewe hujui wanachokitaka wao watakuwa wanajua.

Kama sie wenyewe hata hatujui tunachokitaka nchini mwetu tutajuaje wanachotaka watu wengine kwenye nchi zao?

Na kwa kuongezea tu jeshi la Misri lina heshima kubwa sana kwa wananchi wa Misri na hata wakiwa mitaani wananchi wanajisikia kuwa wana jeshi la kuwasaidia na sio kuwakimbia.

Ni hivi majuzi tu SCAF limepewa kiasi cha dola 1.3 bilioni na Marekani kuliimarisha kijeshi. Jana na leo jeshi hilo limeingia mitaani kwa mara ya pili kufuatia wakati ule walipojitokeza kuunga mkono wito wa wananchi kwamba Hosni Mubarak aondoke.

Walichofanya ni kumtoa Mubarak na kuhakikisha unafanyika uchaguzi ambao ndio uliomchagua Mursi na sasa ni wao ndio wanaingilia tena na kumtoa Mursi, kuweka serikali ya mpito na wiki chache zijazo kutakuwa na uchaguzi mwingine.

Ni jeshi moja la ajabu sana.
 
Back
Top Bottom