kibol
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 4,636
- 2,880
hicho kipande chenye red nimekipenda sana mkuu wangu.Absolutely; nadhani watu wanasahau tu kuwa mapinduzi ni njia pia ya kuleta utawala; lakini ni njia ya mwisho. Mapinduzi yanaweza kuwa ya watu (popular revolution) au ya kijeshi (military). Na yote hayo yanaweza kuwa ya damu au ya kutokumwaga damu. Mapinduzi yaliyomuondoa Mubarak yalikuwa ni ya watu na hayakuwa na umwagikaji damu; haya ni ya jeshi na so far hakuna umwagikaji damu.
Mapinduzi ya jeshi hasa yanapofanyika kwa kumwaga damu damu inamwagika kwelikweli. Hata hivyo katika hili jeshi halikwenda hatua zote za kinadharia za kufanya mapinduzi. Limempa mtawala nafasi kubwa ya kujirekebisha na akakataa; hata leo hii hili haikuwa lazima kama Morsi angekuwa na hekima ya kusikiliza na kusoma alama. Watu wengi wanafikiria - kwa makosa - kuwa kwa vile mtu kachaguliwa na wengi basi anaweza kufanya lolote, popote na kwa vyovyote bila kujali maslahi na madai ya minority group. Hili ndio kosa la Morsi na la viongozi wengine wengi ambao walijikuta wanalazimishwa kutoka madarakani kwa mapinduzi.
Kuchaguliwa tu hakukufanyi uwe wa demokrasia. Jinsi gan iunatawala na jinsi gani unalinda maslahi ya minority group.
