Jeshi la Polisi: Ukipewa dhamana polisi kutoka ni bure usitoe pesa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari kuomba rushwa pale ambapo Mtuhumiwa anapokamatwa na kupewa dhamana na Ndugu zake kwa kumtaka atoe chochote katika Vituo vya Polisi.

Akiongea na Wakazi wa Kata ya Kamoge Wilayani Bukombe Mkoani Geita Katika ziara aliyofanya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella, Jongo amesema ni marufuku Mwananchi kutoa kitu chochote kwa Askari endapo Mtuhumiwa atapewa dhamana na Ndugu zake kwa kutimiza Masharti.

"Jamani ehee kuingia Polisi bure kutoka hela hili jambo marufuku mbele ya Uongozi wangu Mimi Bibi yenu, ukiingia Polisi bure kutoka bure, wewe ukitoa hela umetoa rushwa na sitakubali nawaachia namba yangu ya simu mniambie huyo Askari anayedai hela kutoka ndani ya kituo cha Polisi Mimi sasa hivi nimehama kwenye Ubibi nitakuwa Shangazi”

RPC Jongo amesema baadhi ya Askari wamekuwa wakilichafua Jeshi la Polisi huku akiahidi endapo watagundulika atawachukulia hatua za Kisheria huku akiwataka Wananchi kutoa taarifa mapema kwa atakayeendelea kufanya hivyo.
 
Kwani unaambiwa kua toa hela?

We unawekewamazingira tu, unatoa mwenyewe.

Trafiki mwenyewe huwa haombi hela, ila anakiwekea mazingira, utajua mwenyewe utoe 20 au akuandikie 90, happy utajiuliza utoe hiyo 90 wakale watawala au 20 ale yeye. Huyo afande anazuga tu, vituoni kuna namba hadi za IGP, yeye ni nani?
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari kuomba Rushwa pale ambapo Mtuhumiwa anapokamatwa na kutimiza masharti ya dhamana kwa kumtaka atoe chochote katika Vituo vya Polisi

Akiongea na Wakazi wa Kata ya Kamoge Wilayani Bukombe amesema, "Jamani ehee kuingia Polisi bure kutoka hela hili jambo marufuku mbele ya Uongozi wangu Mimi Bibi yenu, ukiingia Polisi bure kutoka bure, wewe ukitoa hela umetoa rushwa na sitakubali"

Amewaachia Wananchi namba yake ya Simu ili kutoa taarifa mapema kama matukio ya aina hiyo yataendelea kufanya hivyo

Chanzo: Millard Ayo
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari kuomba rushwa pale ambapo Mtuhumiwa anapokamatwa na kupewa dhamana na Ndugu zake kwa kumtaka atoe chochote katika Vituo vya Polisi.
a Wananchi kutoa taarifa mapema kwa atakayeendelea kufanya hivyo.
🤣🤣🤣🤣Kule huambiwi toa hela mzee, kule ni figisu ndo zitaendelea mpaka utaona utoe hela ili tu utoke!!!
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari kuomba rushwa pale ambapo Mtuhumiwa anapokamatwa na kupewa dhamana na Ndugu zake kwa kumtaka atoe chochote katika Vituo vya
Shida ya polisi bana hakwambiii utoe helaa

Ila we mwenyewe unawapa hela mambo yasifikie

Mahakamani
 
Baadhi ya wananchi ukute walikua wanapiga hadi makofi,utadhani walikua Marekani,wamerudi jana,hawajui tabia zilizopo kwa baadhi ya askari.
Watanzania kwan huwajui wataambiwa.. watanzania nyie ni wapumbavu kbs na watapiga makofi balaa 🤣🤣🤣🤣
 
Huwezi tenganisha rushwa na polisi wa Tanzania. Hata kama una taka akuelekeze njia lazima umpe rushwa.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Labda ifanyike hivi: Polisi wa Tanzania wahamishiwe Rwanda, na wa Rwanda waletwe Tanzania. Hayo yakifanyika, huenda hiyo kero itatoweka.
 
Katika makamanda wanafki pamoja na huyu ye mwenyewe ukute aliwekwa hapo Kwa kutoa rushwa shupid hamna kitu hapo
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari kuomba rushwa pale ambapo Mtuhumiwa anapokamatwa na kupewa dhamana na Ndugu zake kwa kumtaka atoe chochote katika Vituo vya Polisi.

Akiongea na Wakazi wa Kata ya Kamoge Wilayani Bukombe Mkoani Geita Katika ziara aliyofanya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella, Jongo amesema ni marufuku Mwananchi kutoa kitu chochote kwa Askari endapo Mtuhumiwa atapewa dhamana na Ndugu zake kwa kutimiza Masharti.

"Jamani ehee kuingia Polisi bure kutoka hela hili jambo marufuku mbele ya Uongozi wangu Mimi Bibi yenu, ukiingia Polisi bure kutoka bure, wewe ukitoa hela umetoa rushwa na sitakubali nawaachia namba yangu ya simu mniambie huyo Askari anayedai hela kutoka ndani ya kituo cha Polisi Mimi sasa hivi nimehama kwenye Ubibi nitakuwa Shangazi”

RPC Jongo amesema baadhi ya Askari wamekuwa wakilichafua Jeshi la Polisi huku akiahidi endapo watagundulika atawachukulia hatua za Kisheria huku akiwataka Wananchi kutoa taarifa mapema kwa atakayeendelea kufanya hivyo.

Millard
 
Ye yupo kwenye kinyozii... Uzuri habari inajitosheleza,, ameongea kwenye ziara ya mkuu wa mkoa
 
Back
Top Bottom