JWTZ liwe na kitengo cha elimu kwa raia, kuna upotoshaji mkubwa kulihusu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
38,269
47,485
Wiki iliyopita katika mizunguko yangu ya kusaka noti nilipanda daladala iliyokatiza Kurasini, kuna mahali magari yakasimama kuruhusu wanajeshi wengi waliokuwa wakivuka barabara kwa makundi huku wakiimba nyimbo zao.

Kama mnavyojua Watanzania ni watu wanaopenda na wazuri sana kuanzisha soga popote hata kama hawafahamiania, basi soga au stori za kupoteza muda kuhusu jeshi na wanajeshi zikaanza kwa mshwashwa mkubwa kila upande,

Wa kwanza niliyemsikia alikuwa ni kondokta, yeye alisema hao ndio wenye nchi yao tutulie tu wapite hatuwezi kushindana nao.

Mzee Mwingine aliyevalia kaunda suti wa miaka kama 55 hivi akasema tuogope sana watu waliofundishwa kuua tu, hao ni watu huwezi kushindana nao kabisa!, alikuwa akiyarudia haya maneno kila mara. Pia akaongezea hao watu wakipewa amri ya kuua mahali popote ni lazima kutekeleza bila kuhoji!

Mwanaume mwingine wa makamo akasema hapo huwezi kutofautisha kati ya mwanaume na mwanamke, cha ajabu mimi nilikuwa naona tofauti hiyo tena niliona mabinti wengi tu warembo sana katik hao wanajeshi.

Mwingine alisema kukitokea taharuki au sintofahamu yoyote kubwa katika nchi wao ndio kila kitu na hadi polisi wanageuka kuwa raia!

Katika hayo mastori pia kulitokea jinsi gani zamani wanajeshi walivyokuwa wababe wakichapa watu mitaani.

Mwingine akasema jeshini hakuna sheria ni amri tu!

Itoshe kusema mengi niliyoyasikia yalikuwa ni upotoshaji mkubwa, mtazamo finyu, uongo na chumvi nyingi kuhusu jeshi. Mastori ya aina hii yamejaa mitaani na kwenye vijiwe vya kahawa, hiyo inamaanisha jeshi linahitaji uwekezaji mkubwa katika elimu kwa raia kuwapa mwanga kidogo kuhusu historia, maisha ya wanajeshi na majukumu muhuimu ya jeshi ili kuondokana na vihiyo makanjaja wapotoshaji
 
Mkuu, hivi ndivyo watanzania wengi wanavyoamini! Na jeshi na watawala ndivyo wanavyotaka wananchi waamini, hivyo, katu hawatatoa elimu. Unajua watu wengi bado wanaishi kwenye mawazo ya utumwa, wananchi wanajiona wao ni watumwa wa dola. Haya ni maisha nchi zilizoendlea walioyoishi enzi za Nepaleon. Kinachotakiwa kufanywa kugeuza mfumo wetu wa elimu, ili graduates wamalizike wakiwa wamefundwa vitu vya maana na kuelimika na siyo kukariri.
 
Maaskari wa JWTZ wanapenda kufanya fujo mtaani na ubabe wa kipumbavu.

Binafsi niliwahi kupigwa na maaskari wa JWTZ bila sababu YEYOTE.

Siku nchi ikiingia kwenye changamoto ya kiusalama tutanguna na adui kuwapiga miti hawa malimbukeni.
sio kweli kuna sababu embu funguka tujue kosa lilikuwa la nani?
 
Wiki iliyopita katika mizunguko yangu ya kusaka noti nilipanda daladala iliyokatiza Kurasini, kuna mahali magari yakasimama kuruhusu wanajeshi wengi waliokuwa wakivuka barabara kwa makundi huku wakiimba nyimbo zao.

Kama mnavyojua Watanzania ni watu wanaopenda na wazuri sana kuanzisha soga popote hata kama hawafahamiania, basi soga au stori za kupoteza muda kuhusu jeshi na wanajeshi zikaanza kwa mshwashwa mkubwa kila upande,

Wa kwanza niliyemsikia alikuwa ni kondokta, yeye alisema hao ndio wenye nchi yao tutulie tu wapite hatuwezi kushindana nao.

Mzee Mwingine aliyevalia kaunda suti wa miaka kama 55 hivi akasema tuogope sana watu waliofundishwa kuua tu, hao ni watu huwezi kushindana nao kabisa!, alikuwa akiyarudia haya maneno kila mara. Pia akaongezea hao watu wakipewa amri ya kuua mahali popote ni lazima kutekeleza bila kuhoji!

Mwanaume mwingine wa makamo akasema hapo huwezi kutofautisha kati ya mwanaume na mwanamke, cha ajabu mimi nilikuwa naona tofauti hiyo tena niliona mabinti wengi tu warembo sana katik hao wanajeshi.

Mwingine alisema kukitokea taharuki au sintofahamu yoyote kubwa katika nchi wao ndio kila kitu na hadi polisi wanageuka kuwa raia!

Katika hayo mastori pia kulitokea jinsi gani zamani wanajeshi walivyokuwa wababe wakichapa watu mitaani.

Mwingine akasema jeshini hakuna sheria ni amri tu!

Itoshe kusema mengi niliyoyasikia yalikuwa ni upotoshaji mkubwa, mtazamo finyu, uongo na chumvi nyingi kuhusu jeshi. Mastori ya aina hii yamejaa mitaani na kwenye vijiwe vya kahawa, hiyo inamaanisha jeshi linahitaji uwekezaji mkubwa katika elimu kwa raia kuwapa mwanga kidogo kuhusu historia, maisha ya wanajeshi na majukumu muhuimu ya jeshi ili kuondokana na vihiyo makanjaja wapotoshaji

Hakuna uongo hapo hata kidogo.

Jeshi ndio nchi.
Ukitaka maelezo tofauti na hayo ndio unataka upotoshaji wènyewe.
Hata huko Ulaya au mbinguni kazi za jeshi na hizohizo tuu.
 
Back
Top Bottom