Maelezo kwa ufupi juu ya clip ikionyesha wanajeshi katili wakiua raia

100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
3,622
12,051
Hii clip nimeiona kutoka kwenye uzi alioanzisha mdau anaitwa GoldDhahabu wenye kichwa cha habari Hawa wanajeshi katili ni wa wapi? .

View: https://streamable.com/ly7v6f

Kuna maelezo mengi tofauti na sehemu kubwa si sahihi.

Tukio linaonyesha raia ambao wamefungwa mikono na kuzibwa macho wakikokotwa na askari, pasipo raia hao kujua wanaelekea wapi au pengine wakifahamu wanaelekea mahala salama wanaangukia kwenye shimo lililoandaliwa tayari na kupigwa risasi vichwani, baada ya askari hao kumaliza kuwapiga risasi mmoja baada ya mwingine, askari hao wakiwa wameshatanguliza matairi ya gari kwenye shimo, wanawasha moto na kuteketeza miili hio.

Hili tukio lilitokea 16 April 2013 nchini Syria katika mji mkuu Damascus, askari wanao onekana kutekeleza unyama huo wanatokea kitengo cha intelijensia katika jeshi la Syria (Military Intelligence Directorate (Syria)), na specifically hao askari wapo katika kitengo kinachohusika na ukatili, utesaji na mauaji pasipo huruma. Yaani kwenye Syrian Military Intelligence kuna hiki kitengo kwa ajili ya utesaji, mauaji na ukatili wa kila aina unaoufahamu.

Syrian Military Intelligence ipo chini ya raisi, inaendeshwa na Bashar Al Assad mwenyewe, kitengo hiki kimekuwa kimetumika pia kwenye siasa hasa kuwakandamiza wale wanaotaka kuleta upinzani lazima cha moto utakiona.

Hii clip imevuja mwaka 2022, inasemekana kuna mtu alipata access ya laptop iliyokuwa na clip hii, akacopy na kuihifadhi, inasemekana ni askari wa Syria.
Aliyetambulika kwenye hii clip ni Major Amjad Yousef ambae anaonekana kuwapiga risasi raia hao pasipo huruma, askari huyu katili inasemekana amejiunga na jeshi mwaka 2004, baadae baada ya mafunzo akajiunga na branch 227 katika Syrian Intelligence Service kitengo maalumu kwa ajili ya utekaji, kutesa na kuua hasa wapinzani katika serikali ya Syria.

Kwa ufupi hao raia wanauliwa kikatili inasemekana hawana kosa, kilikuwa ni kipindi cha mapigano ambapo waasi walikuwa wanakaribia eneo hilo, hivyo askari hao walitaka kuonyesha mfano kwa yeyote ambae atajaribu kuwa upande wa uasi. Raia hao inasemekana waliishi karibu kabisa na eneo ambalo kulikuwa na upinzani.

Raia waliouawa wakati huo ni 41, waliouawa kwenye hilo shimo. Hata hivyo inasemekana waliouawa wengine ni wanakadiriwa 200 au 300 katika maeneo mengine

Baada ya clip kuvuja, Amjad alikamatwa na serikali ya Syria 2022, Amjad amekamatwa pasipo warrant na hajafikishwa mahakamani, wachambuzi wa mambo wanasema kukamatwa kwa Amjad ni kuzuia waliojihusisha na unyama huo waliopo ngazi za juu wasifahamike.

Serikali ya marekani ilitoa sanctions juu ya Amjad Yousef mnamo March mwaka huu 2023 , secreatry of state Anthony Blinken alisema vikwazo hivyo ni kwa ajili ya mauaji hayo yaliyofanyika.
 
Hii clip iliniumiza, na sasa nimeumia zaidi kwa kufahamu kwamba waliouawa hawakuwa na hatia!

Amjad hastahili kuwa hai mpaka hivi sasa, na ingependeza zaidi endapo wangepatikana wote waliotekeleza ukatili huo katika clip.
Wengine walifariki vitani, kwenye vita na machafuko yaliyokuwa yakiendelea askari wengine kwenye hio clip walifariki, huyo Amjad ndiye alikuwa kiongozi hapo.
 
Hii clip iliniumiza, na sasa nimeumia zaidi kwa kufahamu kwamba waliouawa hawakuwa na hatia!

Amjad hastahili kuwa hai mpaka hivi sasa, na ingependeza zaidi endapo wangepatikana wote waliotekeleza ukatili huo katika clip.
Mtu katili namna hiyo kifo cha haraka ni kumfanyia favour maana ni kumpumzisha, anapaswa kupitia mateso makali ya taratibu mpaka pale mwili utakaposhindwa kuvumilia hali hiyo (kufa kwa mateso).

Ulikuwa ni unyama wa hali ya juu sana, usioweza kuvumilika. Sio Syria tu, serikali nyingi za dunia zina vitu vya ajabu sana ambayo vinafanywa kwa siri za kiwango cha juu.
 
Sahihi, serikali nyingi wana vitengo maalumu jeshini kufanya kazi za namna hii.
 
Mtu katili namna hiyo kifo cha haraka ni kumfanyia favour maana ni kumpumzisha, anapaswa kupitia mateso makali ya taratibu mpaka pale mwili utakaposhindwa kuvumilia hali hiyo (kufa kwa mateso).

Ulikuwa ni unyama wa hali ya juu sana, usioweza kuvumilika. Sio Syria tu, serikali nyingi za dunia zina vitu vya ajabu sana ambayo vinafanywa kwa siri za kiwango cha juu.
Nakupia nchi zilizoendelea, zenye demokrasia huu ujinga hakuna. Uko huku huku kwenye vi-nchi vyenye watalawa wasiopenda demokrasia.
 
Ni kweli mkuu. Ndiyo maana huwa nashangaa watu wanaosema eti demokrasia siyo muhimu kwenye nchi.
Demokrasia tatizo watu wanafahamu ni uongozi tu serikalini hasa uraisi, lakini demokrasia ni pana sana, kuanzia uongozi wa juu hadi maisha ya raia mmoja mmoja, hakuna balance of power kama hakuna demokrasia. Wanajeshi na askari wanakua na mamlaka ya juu kuliko raia. Mnaishi kama wanyama wafugwao.
 
Nimeangalia hadi mwisho ila imeniumiza.. haswa anapowaachia waone kama wanaweza kutembea kuendelea mbele then wanaanguka na paap..

Mola ndie atahukumu wa kuhukumiwa, na hivi wanajiweka juu ya wengine maishani.
 
Hivi hawa washkaji wana familia kweli huko nyumbani yaani watoto au mke aseee !! Watu huwa wanasema kufanya kazi mochwari ni kipengele ila hii kazi ni ya moto asee naona bora hata anayenyonga wafungwa ana nafuu ! Hii kazi hata ukiiacha lazima upate Post Traumatic Disorder.

Hiki kitengo hata kwetu hapa kipo kweli ?
 
Back
Top Bottom