Upotoshaji na uongo wa huyu Mchina siwezi kuukalia kimya

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,889
Kuna mada ina trend mitandaoni kumhusu mchina aliyetajirikia Tanzania na maoni yake kuhusu mafanikio yake na ujinga na uvivu wa Tanzania kwenye kufanya Kazi. Asili ya haya mazungumzo ni kundi sogozi la WhatsApp na aliyesambaza sijui ana agenda gani ama la ni mjinga mmoja asiyejua mengi kuhusu Wachina.

Kuna uwezekano mkubwa yalikuwa mazungumzo yasiyo rasmi kati ya wawili hao, lakini msambazaji akavutiwa nayo kiasi cha kuamua kuyatengenezea mada.

Haya mazungumzo yao yanaweza kumuweka huyo mchina kwenye hali ngumu kwa viongozi wengi wa CCM kwakuwa wanafahamiana vema na pengine wanaweza kujuta kumfahamu..japo kibongobongo shekeli humaliza kila aina ya udhia.

Nianze na haiba yake. Amejipa jina la kizungu kama wengi wafanyavyo, anajiita Thomas almaarufu Tom
Mfupi kipipa mwenye heshima za kujifanyisha na anayejua kujipendekeza hasa. Ana maneno mengi na mjuaji sana. Kisha muongo muongo sana.

Anapenda kujinyenyekesha kinafiki mbele ya viongozi wa CCM na serikali. Akiongea nao hupenda kupiga magoti na kuweka mikono kama anashukuru na kutoatoa asante bila mpangilio. Kwa mbinu yake hii kawashika viongozi wengi sana.

Anapenda mno kupiga picha na kila kiongozi anayekutana/kutanishwa naye. Ni mtu wa kujikomba mno. Hoja zake zimejaa uongo na upotoshaji mkubwa hebu tuzipitie moja baada ya nyingine.

1. Alikuja kama kibarua kwenye ujenzi wa uwanja wa taifa kipindi cha Benjamin Mkapa. Waliokuwepo wakati ule wanajua nini kilimtokea msimamizi wa ule ujenzi baada ya rais wao kuna kuuzindua.

Kwa kifupi ni kwamba rais wa China wa kipindi kile alipona viwango vya chini vya ule ujenzi. China ndio ilifadhili.. Kiasi cha pesa kilichoidhinishwa ni tofauti kabisa na kilichojengwa. Yule msimamizi alisafirishwa China na tuliambiwa alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika miradi ya ufadhili wa serikali ya China ambao kulikuwa na upigaji mkubwa mojawapo ilikuwa ujenzi wa uwanja wa taifa. Wizi wa malighafi za ujenzi.

Wizi wa pesa kwa baraka za wanasiasa viongozi wa chama chawala. Kulikuwa na mtandao wa wizi na upigaji kati ya wasimamizi wa kichina na viongozi wa kisiasa.

Mchina Tom anadai utendaji Kazi wake wa kutukuka ndio ulimfanya akapewa kazi ya kusimamia mtambo wa kusaga mawe (crusher) kuwa kokoto ulioko Lugoba Chalinze. Je, alisema huo mtambo boss wake aliupataje?

Ule ujenzi wa uwanja wa taifa ulihitaji kuwa na mtambo wake wenyewe wa kuzalisha kokoto. Huo mtambo na eneo la machimbo vilipaswa kuwa mali ya serikali baada ya ujenzi maana vilikuwa sehemu ya mradi. Ni nini kilitokea hadi ukamilikiwa na mchina? Tom hawezi kujibu hili swali.

Biashara ya kokoto iliyofanywa na boss wake Tom huku yeye akiwa msimamizi ndio ilizalisha mtaji wa kwenda kufungua kiwanda cha marine boards.. Tungekuwa na serikali majini hawa wote walipaswa kuwa gerezani.

SEHEMU YA PILI

Alipoulizwa kajifunza nini Tanzania akasema watanzania ni wajinga sana.. Muda mwingi wanautumia kulala na kusali! Je ni kweli watanzania Wote wako hivyo? Watu waliomfanya akafika hapo alipona ndio anawadhihaki kiasi hiki kweli?

Ana wafanyakazi wengi, ana wateja wengi wote ni watu wa kujituma lakini kawakejeli na kuwatusi wote hawa.. Hajui kusali sana kwa wabongo kumensaidia sana hata yeye kuishi na kufanya kazi kwa amani?

Anaendelea kusema watanzania hawana akili kwakuwa pesa yote wanayopata kwa tabu wanaimalizia kwa kucheza kamari ya mchina.. Huyu ni mpumbavu wa mwisho

Huku anasema watu ni wavivu hwafanyi Kazi huku anasema wanafanyakazi na kupata pesa kwa jasho...
Wachina ndio wapenda kamari no MOJA duniani mpaka wakawekewa sheria kali sana maana iliwafilisi wengi sana.

Hapa Tanzania wamekuta ni ruksa kucheza kamari, wameiboost kwa kiwango cha juu mno hii biashara.. Makasino yote mjini wateja asilimia 90 ni wachina. Na wengi hii michezo imewafilisi na kukimbia nchi wakiacha biashara wameweka dhamana

Anazungumzia matumizi ya simu muda wote! Huyu ni kiazi mbatata .. Waulize wasajili line wanavyofurahi wanapopata mteja mchina.. Wana matumizi makubwa ya bando na muda mwingi wako tiktok kuangalia ujinga. Ni mahiri wa kutumiana picha kwa kila wanachofanya.. Kama yeye hatumii sana simu hizo ni sababu zake binafsi.

Anawakandia wanasiasa (wa CCM) kwamba tunawaabudu na kuamini watatutatulia shida zetu... Hapa kaonesha unafiki wa hali ya juu na rangi zake halisi .. Kama hao wanasiasa ambao wengi ni rafiki zake watasoma bandiko lake watamuona JAU sana. .. Maana sijawahi kuona mtu mwenye kipaji cha kujipendekeza kama yeye.

Kamalizia kwa kuukandia mfumo wetu wa elimu lakini wasomi haohao wenye eimu anayoidiss ndio wanamsaidia mambo yake kila siku.

Anahitimisha kwa kusema TUSIPOBADILIKA WATAENDELEA KUTUNYOOSHA
Hapa nitawatag marafiki zake wanasiasa wa chama chawala

SEHEMU YA TATU NA YA MWISHO

Tuna viongozi wenye upeo mdogo sana na wanaoingilika kirahisi mno na hawa wageni kwasababu tu ya vizawadi vidogo vidogo sana bila kuwachunguza kwanza na kujua malengo hao

Mchina Tom ni matokeo ya viongozi wetu kukosa uzalendo, kukosa maono, tamaa ya mali na ubinafsi uliopitiliza
Nimeshakutana na mchina Tom kwenye vikao vinne tofauti, si mtu mwema kwa nchi getu maana kajawa na unafiki na uzandiki
Mbele ya viongozi wetu hujifanya mwema na mwenye heshima sana.. Mbele ya wachina wenzake huongea kila upuuzi, mwingine ukiwa wa kukera hasa..
Anazungumzia nguvu ya kuwa na picha ya pamoja na kiongozi fulani
Kuwa na Mawasiliano yake
Mianya ya ukwepaji kodi na mambo mengine mabaya kabisa
Mchina Tom hana mpango wa kurudi China, ana mpango wa kupata uraia wa Tanzania na kuweka makazi ya kudumu Iringa
Hatukatai wawekezaji.. Lakini tujiepushe kuwa wema kupita kiasi..

Sent using Jamii Forums mobile app

Video iko wapi ?
Nimeicopy kwenye group moja la Whatsap.. Soma

Jana kuna mchina nilikutanishwa nae ni CEO wa kiwanda cha uzalishaji wa marine boards, melamain boards, pliewoods na MDF ambacho wamekijenga pale Mafinga.

Nilimuuliza ABCs za maisha yake hapa Tanzania na akanambia yafuatayo.
1. Yeye alikuja Tanzania kipindi cha ujenzi wa uwanja wa mpira wa Benjamini Mkapa na alikuja kama kibarua wa kulipwa posho kwa siku.

2. ⁠Uwanja ulipoisha kwasababu alipokuwa kibarua alikua akijituma sana boss wake alimwamini na kumpa kazi ya kusimamia Makarasha Chalinze kama Foremen.

3. ⁠Walipomaliza mradi wa Chalinze yeye aliona kurudi china haiwezekani kwani kwa muda aliokaa TZ kaona fursa nyingi na utajiri mwingi.

4. ⁠Aliamua kumshawishi boss wake kwamba kama wao wanarudi china yeye anaomba abaki TZ aone fursa na ndipo alipoenda mafinga na kuona fursa iliyopo kwenye miti. Na akamwambia boss wake wafungue kiwanda yeye atakisimamia na atahakikisha mtaji unarudi na faida wanapata.

5. ⁠Boss Alikubali na sasa kile kiwanda ni kikubwa yeye ndo msimamizi na anamiliki billions of money .

NILIMUULIZA KWA MUDA ALIOKAA AMENIFUNZA NINI NDANI YA TANZANIA.

1. Alinambia nyie Watanzania ni watu wajinga sana kwasababu mnaamini kwenye miujiza kwakutumia muda mwingi kusali na kulala.

2. ⁠Fedha mlizotafuta kwa jasho mnachezea kamali/gulugulu alilotengeneza mchina mkiamini mtapata utajiri, akamalizia hakuna utajiri wa namna hiyo.

3. ⁠Hamjui matumizi ya simu, muda mwingi mnatumia simu kwa vitu vya kijinga akishangaa mtanzania anaweza kukupigia cm mara 20 mfululizo kama hupokei cm yake. Yeye Ana muda maalum wa kupiga cm na kupokea cm.

4. ⁠Mnaabudu na kuamini wanasiasa wanaweza tatua shida zenu kumbe wao ndo wanawategemea ninyi mtatue shida zao.

5. ⁠Mfumo wenu wa Elimu ni wa kijinga kwasababu haumuandai mtoto kuwa mbunifu na kutumia maarifa yake kubuni/ama kuzalisha bidhaa ili ziingie sokoni.

Alihitimisha kwakusema msipobadilika tutaendelea kuwanyoosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA TATU NA YA MWISHO

Tuna viongozi wenye upeo mdogo sana na wanaoingilika kirahisi mno na hawa wageni kwasababu tu ya vizawadi vidogo vidogo sana bila kuwachunguza kwanza na kujua malengo hao

Mchina Tom ni matokeo ya viongozi wetu kukosa uzalendo, kukosa maono, tamaa ya mali na ubinafsi uliopitiliza
Nimeshakutana na mchina Tom kwenye vikao vinne tofauti, si mtu mwema kwa nchi getu maana kajawa na unafiki na uzandiki
Mbele ya viongozi wetu hujifanya mwema na mwenye heshima sana.. Mbele ya wachina wenzake huongea kila upuuzi, mwingine ukiwa wa kukera hasa..
Anazungumzia nguvu ya kuwa na picha ya pamoja na kiongozi fulani
Kuwa na Mawasiliano yake
Mianya ya ukwepaji kodi na mambo mengine mabaya kabisa
Mchina Tom hana mpango wa kurudi China, ana mpango wa kupata uraia wa Tanzania na kuweka makazi ya kudumu Iringa
Hatukatai wawekezaji.. Lakini tujiepushe kuwa wema kupita kiasi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri sio kipimo sahihi sana cha uzembe au ujinga au mfumo mbovu wa elimu au kuwa wananchi wa nchi fulani hawazioni fursa, utajiri sio kipimo kabisa cha mambo hayo, sbb sio utajiri wote hupatikana kwa njia za haki au sahihi, utajiri mwingine hupatikana kwa njia za ajabu sana, ambazo ni kinyume na sheria, utajiri mwingine hata wa kuuza madawa ya kulevya, kukwepa kodi, wizi mkubwa, rushwa kubwa kubwa, vita huleta utajiri kwa wakubwa, kuuza viungo vya watu, human trafficking, au nchi nyingine kufanya spying kwa kutumia watu wake kuwekeza nchi nyingine, etc etc
 
Back
Top Bottom