Awali ya yote nikushukuru kwa kujitokeza na kujibu hoja.Pengine ni mwanzo mzuri.Ukiwa kama kijana watu wengi walitegemea kuona ukiwa karibu nao. Pili, elewa kuwa jumuiya ni mchanganyiko wa watu wenye fikra tofauti na lazima uwe katika nafasi ya ustahamilivu. Lakini pia imechangiwa na wewe mwenyewe kuwa na kauli zenye jazba.
Kwanza ifahamike kuendesha halmashauri ni taasisi kubwa iliyoundwa na kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, na si ukiwa meya unaweza ukaamka asubuhi na kuamua jambo au ukafukuza mtumishi au ukaajiri au ukaweka mkandarasi au kumfukuza anayeharibu
Nadhani hili ulilitambua wakati unagombea, na ni kwa mkakati wako ulijiaminisha kuwa una uwezo wa kukabiliana na changamoto zitokanzo. Unapolalamika inatupa picha kuwa upo 'on job training' hili jaribu kuliepuka
Kiufupi tuna matatizo ya rasilimali fedha, mfumo wa sheria na muingiliano madaraka wa taasisi za umma na uyendaji mbovu wa watendaji wa halmashauri. Tumetumia muda mwingi kwenye kuongeza mapato na kupunguza matumizi maana mambo mengi yanajitaji fedha
Jerry, unaongoza manispaa tajiri na yenye vyanzo vingi vya pesa kuliko mji,manispaa au jiji lingine kwa kuzingatia eneo. Hakuna tatizo la chanzo cha mapato labda utuambie kuna tatizo la ubunifu. Unaposema hayo, mtu atakuuliza meya wa halmashauri ya kule kwetu Handeni atasema nini.
Mfano: Soko la Ilala lililokuwa linakusanua 3-4m kwa mwezi sasa tunakusanya 9-10m. Eventually mapato yameongezeka toka 16B 2010/2011 mpaka 26B 2011/2012. Tumepunguza matumizi toka dev 40% vs recurrent 60% mpaka Dev 60% vs recurrent 40% kwa maelekezo ya kila shilingi moja senti 60 zihamishiwe dev account bila kuchelewa tofauti na taasisi nyingine zinazotumia kwanza recurrent zikibaki ndio zinaenda dev
Jerry, kukusanya mapato ni sehemu ya kazi za kila siku na ni wajibu. Kwahiyo kuongeza ukusanyaji wa mapato ni kuiwezesha manispaa kutimiza wajibu wake na sio mafanikio hata kidogo. Kama huko nyuma walikuwa hawakusanyi huo ni uzembe na usiweke wajibu wako katika mizani na uzembe. Hoja hii ni dhaifu sana na haina mashiko. Hata kama utakusanya bilioni 100 kwa mwezi hiyo ni kazi yenu wananchi wanataka kuona matokeo(results) na si wewe unasaini nini au unafanya vikao gani n.k. Wanataka kuona matokeo ya wewe kuwepo ofisini.
Tumekuwa halmashauri ua kwanza kuanzisha mfumo wa kukusanya mapato kupitia Bank ka kuitumia benki ya wananchi wa Dar es salaam kupunguza mianya ya kuvuja mapato
Hili pili ni wajibu kwasababu kulinda rasimali za jijij ni sehemu ya kazi zenu. Tunataka kuona, je kupitia mfumo huo kitu gani kimeweza kutokea. Tunardui pale pale (result).
Je ni kwanini bank ya wananchi na isiwe bank nyingine kama CRDB zenye matawi ili kuwapunguzia walipa kodi kazi za kutafuta bank yenye matawi mawili au matatu. Huoni kuleta huduma karibu na wananchi ni sehemu ya ufanisi.
Tunafanya mabadiliko mengi ya sheria ili kuendana na wakati na sasa sheria mpya ya usafi iko functional na pamoja na kubadilisha utaratibu wa kupata na kusimamia makandarasi wa usafi tulitarget 1st January tunze lakini tumechelewa mpaka 1st March kutakuwa na mabadiliko makubwa
Uwepo wa sheria haumaniishi ufanisi mzuri. Tunasheria za kila aina mfano ni sheria za rushwa lakini unaona nchi inavyotapeliwa kila uchao. Kuna sheria ya makazi lakini muziki kila nyumba kumi n.k. Wananchi wanataka kuona sheria hizo zinasimamiwa vipi ili kuleta matokeo. Hiyo ndiyo changamoto.
Hivi Jerry si kuna sheria ya afya inayozuia watu kujisaidia hovyo! mbona wapiga debe shule ya uhuru wana choo cha wazi, unataka kutuambia ukibadilisha maandishi basi wapiga debe wataacha kukojoa hovyo!!!
Tumenunua malori 9 ya taka kuongeza nguvu. Tunanunua greda 2 na moja tulilonalo yutakuwa 1st council sio tu kumiliki greda zaidi ya moja bali matatu kwa ajili ya kuchonga njia za mitaani ambazo ni unpaved
Je malori hayo yatabeba taka kama ilivyokusudiwa au yachukua vifusi vya mchanga kwa 'wazee'. Je, malori hayo yana usimamizi wa kutosha kuhakikisha kila lita ya mafuta na matengenezo yanafanyika kulingana na taratibu?
Umekiri kuwa manispaa ni taasisi kubwa, hivi huoni kuwa badala ya kununua malori, manispaa ilitakiwa iwe na utaratibu wa kueleweka na wa kisheria unaozingatia taratibu wa kuweka 'private sector' kufanya kazi hiyo? Kwa uzooefu wa nchi yetu serikali haiwezi kusimamia baadhi ya huduma na kwa mfumo wa soko tulilo nalo, kampuni binafsi zinaweza kufanya vema kama kuna utaratibu usioingiliwa na rushwa. Kazi ya manispaa iwe kusimamia wakandarasi wachache na si kila mtaa ili kutoa nafasi ya kufanya shughuli zingine.
Changamoto hapa ni rushwa na miradi ya wazee, na ndipo kiongozi makini angeweza kujitofautisha na sisi tukasem kweli anaweza.
Halmashauri ni taasisi inayofanya marketing and PR na katika hilo meya huwezi kumwacha kila aliyetumia neno "kuuza sura" ameonyesha uwezo wake finyu wa kufahamu mambo, kama wanavyosema wanazuoni "intellectuals discuss issues not personality" najua ni ngumu mtu akijiangalia umri wake na achievement alizorecord kukubali failure, ila it doesn't make u a better person kwa kushambulia wengine
Kauli kama hizi hazifai mheshimiwa Meya. Watu wote hawawezi kuwa mameya lakini haiwafanyi wajisikie hawana mafanikio. Unaposema hivyo una maanisha wananchi wako wasioweza kununua aspirini baadhi yao nao ni failure.
Nadhani hasira zimetawala na busara imeondoka, punguza jazba. Hapa unawakashifu wengi na sio uliyemkusudia
Mfano UDA inamilikiwa na Halmashauri ya jiji na mimi ni meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, unaniingizaje huko
Wakazi wa Ilala wanataka usafiri wa uhakika wa umma. Jukumu la usafiri wa umma katika manispaa ya Ilala lipo mikononi mwako. Kama UDA wanafanya hivyo kama Jiji, Ilala ni sehemu ya jiji na maamuzi mengi unahusika kwa njia moja au nyingine.
Unapojitoa ni kukwepa wajibu wako hueleweki. Sasa tuambie mbadala wa UDA uliopo Ilala ni upi.
Kwasababu kuna ufisadi UDA hiyo haifanyi utelekeze jukumu la usafiri ndani ya Ilala. Ndivyo Mameya wote wanavyofanya huko duniani kuliko na uwajibikaj
Mwisho mimi ni kijana na kama binadamu mwengine nina haki ya kusocialize na sioni mahusiano na kazi za umma. Naamini wapenda maendeleo wamenielewa, as usual na karibisha comments and critics
Unapokuwa kiongozi wa umma unakuwa umepeoteza sehemu kubwa sana ya uhuru wako. Wewe unakuwa ni mtu wa umma na kila jambo unalofanya linaangaliwa kama kiongozi na si Jerry. Mfano, ukimwaga chai hotelini hiyo ni habari kubwa hata kama kuna mtu amemwaga birika zima jirani na wewe.
Unahaki ya ku-socialize lakini ukumbuke kuwa unapokuwa katika social activities kuwepo na mstari wa kutenga social na social activies za kikazi. Unaweza kufanya hivyo kwa njia ya kuepeuka picha katika magazeti hata unapokuwa na shughuli binafsi. Hii ni gharama nyingine ya kujenga public image na popularity haiepukiki.
Jerry, unapkouwa na social activities za kikazi ukiwa 'umezungukwa nao' halafu wale wenye vichanga wamelala sakafuni pale Amana hospitali inawatatiza wadau. Think about that and try to make a sharp contrast between Silaa at home and Silaa at work.
Mwisho, kiongozi mzuri ni yule anayesikiliza watu wake wana hoja gani. Ni yule aliye tayari kuwasiliana nao ikibidi na asiye na jazba