I know they have nothing to do na wananchi wa kawaida zaidi ya kuwafaidisheni wewe na maswaiba zako, ambao ni mafisadi wakubwa
Unaweza kulithibitisha hili na ukiwataja maswaiba?
Serikali ya mtaa madafu
Nimekuwa diwani kwa miaka 6 sasa na ninaheshimu misingi ya utawala bora. Mambo ya mtaa huamuliwa na wana mtaa wenyewe kwenye mikutano yao ya mitaa. Michango, miradi, mapato na matumizi yanafanyika huko. Unaniingizaje kwenye maswala ya serikali ya mtaa wa madafu. Kama hamuafiki hayo myaraise kwenye mkutano wa wananchi. Lakini na sisi tunaangalia uwezekeno wa kuziwezesha ofisi za mitaa maana kwa sasa zipo zinazotoza pesa wananchi kwa kisingizo cha kuendesha ofisi.
Mradibwa majibmzambarauni ulibuniwa na kuendeshwa na MMDO chini ya serikali ya mtaa wa madafu. Naamini kama mwananchi wa madafu unahaki ya kufika ofisini kwa mwenyekiti kupata maelezo.
Viwanja vya kinyerezi
Halmashauri imetwaa eneo la ekari 1600 kwa ajili ya zoezi la upimaji viwanja. Kati ya eneo hilo ekari 800 ni mabonde, barabara na huduma za jamii. Ekari 800 tu ndio zinazofaa kwa viwanja. Tathmini ya fidia imefanyika na viwango ni kati ya 500,000-94m. Kuna mazoea ya viwanja kutolewa burevna serikali au miradi ya viwanja kuwa subsidized na serikali jambo ambalo halifanyiki. mradi huu lazma ujighatamie wenyewe. Swala la kugharamia mradi kwa mkopo ndio miradi yote mikubwa inavyogharamiwa. Gharama ya kuhudumia squatter ni kubwa. Cost of living ya mwananchi wa squatter na wa surveyed area ni tofauti kubwa. Matokeo yake tunakuja kokopa Worldbank kuupgrade slums kama vingunguti. Yawezekana wapo wataoshindwa kumudu difference kati ya fidia na bei ya viwanja, niliomba orodha wananchi wakaopt kwenda mahakamani.
Swala la ubunge wa ukonga nimeshalisema.
Tuna mbunge mzuri mhe. Mwaiposa na kazi yetu kubwa ni kumsaidia kuleta maendeleo. Swala la kukaa Tokyo ndio kazi ya siasa kushiriki makundi ya kijamii. Kwa kuwa mtoa hoja anakuwa Tokyo hawezi kujua ni vijiwe vingapi vya kahawa , tangawizi, camp na mikusanyiko mingine. Unavyofika kwa wanywaji wakati mwengine unanunua bia wakati mwengine hununui. Wala haina impact wala milage yoyote ya kisiasa.
QUOTE=Brigedia;3101011]JERRY SLAA NA MIKAKATI YAKE YA KUTAFUTA UBUNGE JIMBO LA UKONGA 2015:
Siku zote kiongozi bora wa uma ni yule anayekubali kukosolewa na kujisahisha pale inapobidi ili kuboresha ufanisi wa kazi yake. Jerry utake usitake kwenye hili lazima tukukosoe kwa facts, wewe umekuwa diwani katika kata ya ukonga kwa muda mrefu na hiki ni kipindi chako cha pili ambapo awamu ya kwanza ulikuwa naibu meya na sasa ni meya kamili lakini hakuna chochote kile cha maana ulichokifanya pamoja na mbunge wako wa awali Makongoro Mahanga na sasa Mama Eugene Mwaiposa ambaye amekuwa kama mbunge wa viti maalum na si wa jimbo. Sihitaji kuzungumzia takwimu ulizozitoa humu ndani because I know they have nothing to do na wananchi wa kawaida zaidi ya kuwafaidisheni wewe na maswaiba zako, ambao ni mafisadi wakubwa. Hatuyafanyi haya kwa kukukomoa bali tunakukumbusha wajibu wako. Naomba niweke record sawa humu JF ili watanzania waelewe haya tunayoyazungumza wananchi wenzako wa Ukonga:
Suala la huduma za serikali za mitaa Ukonga:
Hii ni changamoto kubwa ya kwanza ambayo inakela sana wananchi wa Ukonga na maeneo mengine ya Manispaa ya Ilala. Katika maeneo yote Wenyeviti wa serikali za mitaa ya Ukonga ambao wote ni maswaiba wako wazuri unaowatumia kukupigia kampeni za kuusaka ubunge 2015, wamejifanya miungu watu na wanataka waabudiwe na wamekuwa wafujaji wazuri wa fedha za uma. Mathalani rafiki yako mkubwa ndugu Alfred Kipondya, mwenyekiti wa mtaa wa Madafu ambaye ni kinara wa kuwachangisha wanachi michango isiyokuwa na kichwa wala miguu. Mmekuwa mkishirikiana nae kula pesa za miradi mbalimbali ya uma kama huu wa maji Mzambarauni kama ambavyo nimeelekeza hapo chini. Hali kadhalika unatueleza mmeongeza magari ya kuzoa taka ya municipal council ilihali wewe na Kipondya mnaendelea kuwachangisha wananchi kila kaya 3,000Tshs fedha ambazo zinaingia katika kampuni yenu binafsi, na hili ninakuombeni acheni mara moja mkija kwetu na wafungulia mbwa. Mbaya zaidi umekuwa ukiwashinikiza wenyeviti pamoja na watendaji wa serikaliza mitaa wakusanye 2,00Tshs kwa kila mtu anayekwenda kwa ajili ya kusainiwa document yoyote ile, ili muulize vizuri swaiba wako Kipondya hatokaa anisahau pale aliponiomba hela kwa ajili ya kunisainia document hukuakitaka kunipa risiti ya cash book yenye muhuli wa serikali ya mitaa. Wananchi huwa tunajiuliza Ilala Municipal Council kwenye hayo makusanyo mnayokusanya si kuna fedha mnazorudisha zitumike katika ofisi zetu za kata pamoja na serikali za mitaa, zinafanya kazi gani?? Jamani mbona hamtuonei huruma? Gharama za maisha zimepanda acheni kutunyonya sana.
Suala la Mgogoro wa Ardhi Kinyerezi:
Halmashauri ya Ilala imepitisha mpango wa upimaji wa viwanja kwenye maeneo ambayo watu wanaishi kule kinyerezi, ambapo mmewaambia wananchi wachangie gharama za upimaji ambapo katika kila square metre moja wanatakiwa kuchangia shilingi 1500. Ukishindwa kulipia gharama kwa ajili ya upimaji unanyanganywa eneo na unalipwa fidia. Na unajua fika kesi iko mahakamani ambapo wananchi wanapinga gharama ya uchangiaji na hali kadhalika mnajua fika kabisa hata kama mtu akishindwa kulipa gharama za upimaji, gharama za ufidiaji haziendani kabisa na gharama ahalisi za ardhi. Mwanasheria wako wa manispaa ya Ilala aliieleza mahakama kuu mbele ya Judge Shangwa kwamba fedha hizo mnazotaka kuwalipa wananchi mmezikopa bank. So mnataka hizo interest ndio wananchi wawasaidie kulipa?? Huu ni mradi ambao una harufu ya ufisadi na wewe unahusika moja kwa moja kwenye hili pamoja na maswaiba zako.
Mradi wa maji Ukonga Mzambarauni:
Mh mstaiki meya Jerry Slaa hili linaniuma sana kwani lina nigusa sana na watu wa Ukonga hawatokaa walisahau milele katika kipindi chao chote cha maisha yao hapa Duniani. Wananchi wote walichangishwa shilingi 5,000 Tshs kwa kila kaya kwa ajili ya mradi huu tena uchangiaji huo ulikuwa ni wa lazima kwa ajili ya kuondoa shida ya maji, na mkawaambia wananchi mtawasambazia mabomba kuanzia pale mzambarauini kwenda sehemu zingine mbalimbali kama Madafu,Mombasa, Gongo la Mboto, Mwisho wa Lami, mpaka Mazizini. Hivi huwa ukipita pale Mzambarauni roho huwa haikuumi kuona mmekula pesa za wananchi na huduma hakunailiyopatikana?? Muogopeni mwenyezi mungu tendeni haki panapostahili.
Mkakati wako wa kuusaka Ubunge Jimbo La Ukonga-2015:
Hongera sana kwa kushiriki kikamilifu kupigania kupatikana kwa jimbo la Ukonga ambalo linaongozwa na very weak candidate Mh Eugene Mwaiposa,ambaye anafahamu kuwa hiki ndiyo kipindi chake cha mwisho na hatorudi tena kwenye nafasi hiyo. Kwa hili naomba nikupongeze kwa kuona umuhimu wa kuwa na jimbo letu la Ukonga, dhana ambayo tuliamini itasaidia kutuletea maendeleo eneo letu la Ukonga, lakini hali imekuwa tofauti kabisa zaidi ya kuwa chaka la watu kuvuna pesa. Nashukuru umekili kuwa kama kugombea ungegombea 2010 kwani ulikuwa moja ya waasisi wa kupatikana kwa jimbo. Lakini ukweli wenyewe wa hili uko moyoni mwako, na ninajua dhamira yako inakusuta kwenye hili. Chanzo cha wewe kutogombea ubunge 2015 kinafahamika wazi kwa wale tunaofutailia. Mshauri wako mkubwa siku zote amekuwa ni mzee wetu mpendwa Balozi Patrick Tsere (Kipenzi cha vijana) ambaye ulifanya nae kazi akiwa kama DC wa Ilala na wewe ukiwa kama naibu Mstaiki meya. Unafahamu vizuri jinsi ambavyo walikuwa hawaelewani na mstaiki meya wa wakati huo na sababu kubwa ilikuwa ni uelewa pamoja na elimu ndogo aliyonayo mheshimiwa huyo kwa hiyo walikuwa wakipishana mzee Tsere muda wote. Hali iliyopelekea Mzee Tsere kukutumia wewe zaidi kwenye masuala mengi, hili unaweza ukabisha ila likowazi ulisafiri sana kwenda ziara za nje kwa sababu hiyo tu. Ili fika mahali mambo yakawa hayaendi kwa ajili ya mgogoro huo,ndipo Mh Rasi alipoona amsimamishe kazi Tsere na baadaye kumpangia nafasi ya ubalozi Malawi (rejea maneno ya Mh Raisi siku anamwapisha Tsere Ikulu). Na ni mzee Tsere aliyekushauri usubiri kwanza usiingie kwenye ubunge uongoze Ilala Municipal Council. Sasa mikakati yako ya kuusaka ubunge wa jimbo la Ukonga umeizindua katika ma Bar mbalimbali na kijiwe chako kikubwa cha kukusanya taarifa ni Mangi Bar (Tokyo) ,chini ya swaiba wako mkubwa na tapeli namba moja Saidi Dezo. Hutopata kula za Ukonga kwa kuwanywesha watu bia ndugu yetu, chapa kazi tukuvalue kwa uadilifu na uwajibikaji wako. Majuzi ulikuwa Kampala International University-KIU,kwa ajili ya mkakati huoo na umemwaga hela ukiamini vijana wanakupenda la hasha yawezekana hizo ni ndoto za buriani. Umri wako ulionao bado ni mdogo, weweni kijana mwenzetu cha kushangaza umekuwa na lugha za kejeli hali kadhalika dharau kubwa watu, hasa vijana unatuona tuko kijiweni. La hasha yawezekana sasa tukawa hatuna cha kukusaidia ila japo salamu tutakuona kiongozi wetu unatujali. Umediriki kuanza kuchangisha fedha kwenye mitandao na sehemu mbalimbali (ushaidi tunao) kwa ajili ya mambo mbalimbali ya Jimbo la Ukonga lakini badala ya kutimiza lengo la uchangishaji huo badala yake umekuwa ukiyafanya hayo mambo kisiasa. Haya yote yana mwisho wake ndugu yetu tunakuomba utimize wajibu wako kama ambavyo tulikupa ridhaa ya kutuwakilisha.
Asante
Brigedia