Mama Lishe jiandaeni kuporwa masufulia ya ubwabwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,373
217,432
Mwaka 2015 baada ya wananchi kuunganisha nguvu na kumshinda Shetani , kwa mara ya kwanza tangu kuumbwa kwa mbingu na ardhi Jiji la DSM lilikombolewa kutoka kwenye mdomo wa Mamba .

Tangu mwaka huo hakuna mama lishe wala baba lishe aliyenyang'anywa sufuria la maharage au wali kwa kisingizio cha kipindupindu ama chochote , hali imekuwa shwari mno tofauti kabisa na kipindi kilichopita ambapo Jerry Silaa aliyekuwa Meya wa Ilala alisimamia kikamilifu dhuluma dhidi ya wajasiliamali wadogo , Katika kipindi cha uongozi wa UKAWA jijini hakuna mali yoyote ya jiji iliyouzwa kifisadi au kinyemela kama ilivyouzwa UDA chini ya Meya wa ccm Didas Masaburi .

Sasa ni dhahiri juhudi kubwa zinazofanywa za kununua madiwani zimelenga kurejesha utawala wa ccm jijini DSM , Ni bahati mbaya kwamba wakirudishwa hawa mambo yao yote yatarudi kama awali , amani iliyopo jijini itatoweka kama walivyoipoteza mwanzo kwa kugawana ugali waliowanyang'anya mama lishe Wajane , Dhuluma zote zitarejea kama awali .

Poleni Mama Lishe , Poleni wakazi wa Jiji .
IMG-20180811-WA0018.jpg
 
Tuliambiwa tumeipenda wenyewe so labda tutahamisha mitaji kama wale wakubwa. Ila utapitaje mpakani na tumeimalisha ulinzi na huna barua ya ruhusa kutoka makao makuu!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom