Mheshimiwa Meya,
Umenijibu hoja zangu katika post #83 ingawa huku tag ili kuweka majibu yako wazi lakini nimekuelewa.
Kwanza wewe ni kiongozi na unakutana na watu tofauti na wenye mitazamo tofauti.
Siku zote kiongozi hupaswa kuwa mvumilivu, mtulivu na mwelekezaji.
Nikifutailia hoja zako naona una jazba na hasira kana kwamba unashambuliwa.
Jambo moja linalokuweka hadharani kuliko watendaji wengine ni nafasi hiyo ukiwa msomi na kijana.
Mbiu ya viongozi vijana imepamba moto na wewe kama mmoja wao ni 'sample' ya kuthibitisha kama madai ya vijana kupewa nafasi za uongozi yana mamtiki au la. Kila unachokifanya ni 'template' ya kwanini vijana wanapaswa wapewe nafasi zaidi katika uongozi wa taifa
Inapotokea matarajio hayakidhi matokeo wanaokulaumu ni vijana wenzako kwa kuwa disappoint. Unachotakiwa ni wewe kuchukua maoni yao kama changamoto na kuyafanyia kazi. kuwadhihaki ni kauli ya kusikitisha sana na inaondoa hata matarajio kidogo waliyo nayo juu yako.
Ukiwa kama bado hujafika pale unapokusudia na kauli zako kama kiongozi zinabaki katika kumbu kumbu na huenda zikakuhukumu mahali usipotarajia. time will tell. Turejee kwenye hoja
Jerry;The point is mwaka mmoja si muda wa kutosha kuona "result"
Mwaka mmoja unatosha kwasababu hukuingia ofisini na kukuta ukumbi. Umekuta kila kitu zikiwemo sheria. Ulichotakiwa kufanya ni kuanza kurekebisha kile kibaya halafu unaweka mkakati wa mema.
Keenja anakumbukwa kwasababu uwepo wake ofisini ulitoa matokeo katika kipindi cha miezi mitatu. Nilikuwepo na nalifahamu vema hili. Hakufanya maajabu bali kusimamia na kuondoa uzembe. Badala ya kuwafukuza wafanya biashara kisutu katika korido, aliwaamuru watengeneze frame za kuweka bidhaa zao. period. Wapita njia wakawa na nafasi na wafanya biashara wakawa na nafasi.
Hili hakuhitaji miaka 5 kama unavyotaka iwe.
Keenja akakusanya mapato na ghafla tukaona pavement zinasakafiwa na kila mtu alijua ongezeko la mapato linatoa matunda yanayotarajiwa. Hakuhitaji miaka 5 wala kuandika sheria zilziopo kama uanavyodai.
Keenja ndani ya mwaka mmoja alirudiha nidhamu na Dar ikatajwa kama Jiji safi hata na wageni.
Tunapomuangalia Mzee Keenja na Kijana Silaa halafu tukasikiliza hoja zako, nashawishika kusema ujana tunaoupigia debe una walakini.
Kwanini ulalamike badala ya kusikiliza na kujifunza? kwanini usitumie usomi wako kutafuta suluhu?
Tajiri ni relative word, majukumu ya handeni na ilala hayaendani. Tuna mapato makubwa na majukumu makubwa vikevile
Nasema Handeni wana majukumu makubwa. Hawana miundo mbinu kama sewarage, maji safi, maji taka, nyumba n.k.
Jerry, huhitaji kujenga ghorofa 50 ili watu wajue unafanya kazi, unachotakiwa ni kufanya simple things in simple way in extra ordinary way. Unabahati hata serikali kuu ipo kwako, wewe unaongea na waziri hata rais tofauti na Meya wa Handeni.
Mapato yako ni chocheo la maendeleo sio kutafuta sababu kama 'relative word'. Ubunifu ndio unahitajika lakini kama umeamua kufanya kazi ' business as usual' kwa hoja ya Ogah, hewala
Kama unashindwa kuona umuhimu wa revenue kwa aina yoyote ya taasisi sintaweza kukuelewa
Najua umuhimu wake ndio maana nimesema kukusanya sio mafanikio ni wajibu wako from day one. Hata kama unakusanya bilioni 100 kwa siku, hazina maana kama bado Meya unaridhika maji yajae pamba house miaka 20 na wewe ukilijua hilo. Hatuhitaji kujua unafanya nini ofisini lakini tutahoji hivi Ilala kuna meya ikiwa sehemu kama Pamba house ameshindwa kuwasiliana na wahusika au idara zake na kutafuta suluhu. Pesa kwenye account ya jiji is not our problem, tunataka kuona hizo pesa unazi tranform vipi katika maisha ya wakazi wa Ilala
Wananchi wa halmashauri ya ilala wanamiliki 8% ya hisa DCB, ni benki yao. Na inamatawi mnne ilala anatoglo, tabata, ukonga na chanika. Nitajie bank nyingine yenye matawi manne ndani ya ilala
Ungefikiria kuongeza CRDB vijana, Lumumba na NMB ungekuwa na matawi zaidi. Sijasema kwanini bank ya watu wa Dar nimesema ongeza wigo. Tatizo hapa unacheza na karata ya kisiasa kujijengea uhalali lakini kiutendaji siasa haina nafasi. Let us hope wananchi wa Ilala wataridhika na hatua zako.
Narudia tena Ilala ni taasisi kubwa , mpango wa usafi ni document ya 20 pages na ina lot 6. Tano ni privatization na moja ni kutumia CBO za mitaa kufanya primary collection na malori ya halmashauri kufanya secondary collection. Na vilevile kutoa back up kwenye lot nyingine. Ndugu yangu sijui unatoka sekta gani lakini maeneo sensitive kama usafi 100% privatisation ni hatari
Sijasema privitization 100% nimesema kupunguza work load inabidi kuwe na privitization.
Kwa taarifa nimetoka sekta ya afya (public health) na nimewahi kufanya shughuli na taasisi kubwa za afya duniani. Kama ungekuwa msikivu huenda ungechota kitu. Pengine nikukumbushe kuwa unapozungumzia malori na ukusanyaji taka hujagusa tatizo, wapo mabwana afya, je unawatumia kama inavyopaswa? Unapoangalia suala la afya utagundua kuwa hakuna privitization 100% bali matumizi ya resource ulizo nazo na private sector. Angalia vitu in
wider prism na jifunze kutoka kwa wengine pia
Ni vyema uwe upost na hizo picha za " kuzungukwa nao" unless unacoment kwenye jambo la mtu usiyemjua. Leadership ethic act 1995 inaeleza wazi na sijaona baya nilolifanya, ni vyema kama unalo uliweke watu waone. Usiaminishe watu kwa hearsays!
Sio mara moja umeonekana ukiwa nao na sihitaji kuweka picha.
Kuonekana ukiwa umezungukwa nao si tatizo wala hoja ni haki na sahihi.
Jerry, unaposoma kitu kama sheria halafu ukaacha busara ni tatizo kubwa. Wale ma-miss walio na vichanga vyao Amana hospitali sakafuni hawajui Leadership act ya 1995. Kama hutatumia busara kufahamu kuwa uonekanao wako unaweza kuzua maswali hilo sina hoja.
Nafaham unajitahidi kufanya kitu kinaitwa 'PR' swali ni kuwa unaifanya ikiwa na busara? Hili sihitaji mjadala kwasababu ni ushauri kwahiyo nisingependa tulijadili tena. Ninachosema ni kuwa hawa watu wanaosema unauza sura wana hoja zao hebu wasikilize halafu jiangalie.