Jerry Silaa amesahaulika ama ni upepo?

Jerry Silaa amesahaulika ama ni upepo?

Yaani JK kweli ni chiboko yao, huyu jamaa ni msanii na anajuwa haswa kulostisha watu. Mawaziri wake wote wamesahaulika kwa muda mfupi tu, wengine wanazidi kukesha kwa waganga kupinga matokeo ya ubunge majimboni mwao ili wabahatishe kuchaguliwa tena uwaziri. Kikwete oyeee, sambaratisha babake.

Kama yule aliyekuwa tamisemi kapotezwa mbaya,ila ki ukweli hakuwa na sifa hata chembe,sasa hivi anahangaika tu bungeni na ushungi wake
 
Mimi ni moja ya watu ambao niliamini kijana huyu alie wahi kuwa Meya wa Ilala angechomoza na kutamalaki katika hawamu hii ingawa alikosa ubunge jimbo la Ukonga, swali langu kubwa nikipi hasa kimempoteza haraka kijana huyu kwenye ulingo wa siasa?Maana baada ya kukosa ubunge wengi tulitegemea atachomoza kwenye uRC na uDC.
Alikuwa mfuasi mtiifu kwa lowassa,alipinga waziwazi kukatwa kwa lowassa
Tukio lile limemuharibia vibaya sana heshima yake
 
Kama yule aliyekuwa tamisemi kapotezwa mbaya,ila ki ukweli hakuwa na sifa hata chembe,sasa hivi anahangaika tu bungeni na ushungi wake
yule hata mie nimefurahi kukalia benchi,alikuwa mjivuni sana.
 
Mkuu nmepata kusikia stivu nyerereee yule msanii anasema
"ambao hatukuokota nao kuni ndo wameenda kuota moto"
statement kali sana hiyo...mana jamaa walikuwa kama majuha majukwaani wakitegemea return
watavuna walichopanda
 
Jerry Slaa
Mama Sofia Simba
Dr Nchimbi
Ndiyo walio ongoza mgomo ktk sekretarieti Kuu kupinga kuenguliwa jina la Lowassa bila kupigiwa kura!
Watu hawa watatu hawatakiwi kabisa ndani ya CCM kwa sasa
Mama Simba atakatwa kuwania uenyekiti wa Wanawake CCM ili asiingie Bungeni mwaka 2020!Husna Mwalima Mbunge aliyemuangusha Kafulila Kigoma ndiye atachukua nafasi yake
husna alimwangusha kafulila ama alimuibia kafulila
 
Alikuwa mfuasi mtiifu kwa lowassa,alipinga waziwazi kukatwa kwa lowassa
Tukio lile limemuharibia vibaya sana heshima yake
Mwanaume unatakiwa ukipiganie unachokiamini mpaka mwisho Jerry alifanya vizuri sana akuwa mnafiki Na chama alikipigania vizuri sana alipata Kura nyingi za ubunge japo alipitia wakati mgumu Wa kupoteza mzazi kipindi cha kampeni mwacheni ajipange upya kupoteza baba kupoteza jimbo mgombea uliyemtetea kufanyiwa mizengwe kuhama chama kapitia wakati mgumu katika siasa na huo ndio uanaume siyo mnafiki siyo mtu Wa matamko ili aonekane
 
Mimi ni moja ya watu ambao niliamini kijana huyu alie wahi kuwa Meya wa Ilala angechomoza na kutamalaki katika hawamu hii ingawa alikosa ubunge jimbo la Ukonga, swali langu kubwa nikipi hasa kimempoteza haraka kijana huyu kwenye ulingo wa siasa?Maana baada ya kukosa ubunge wengi tulitegemea atachomoza kwenye uRC na uDC.
Hawamu hii hiache hivyo hivyo
 
Kuna kitu hakimkijui kuhusu huyu kijana, Jerry alikuwa anaishi kwa nguvu ya waganga wa kienyeji kafanya mengi mabaya kwa ajili ya nafasi nguvu umaarufu na cash
Lakini kama tujuavyo uchawi wa maagano na makafara hautokesheki, Jerry akaanza kuchoka, maamuzi yake mengi yakaanza kuonekana si sawa HAKUSHTUKA bado mzee akafariki hapo ndo akaonja uchungu wa ushirikina! Yaliyofuatia yanajulikana
 
Sio kweli mkuu. Jerry yuko cohort ya 21 ambayo bado inaendelea na masomo
Mkuu niliongea nae pale akiwa cohort ya 20 na Mama Jaji Dr Fauzia
Commercial Laws kidogo zilikuwa zinamsumbua
Labda walimkamata na ww ndiyo ukamkuta

Anyway labda mm ndiyo mechanganya!
 
I just wish mgejua kuwa Jerry is somewhere preparing himself to rise in a bigger professional position. Don't always have prejudicial negative attitudes. At least I write with confidence kwamba Jerry Silaa hajapotea but us somewhere prepared for come back again

Kwenye SIASA ndio kashapotea
 
siasa za makundi zina risk kubwa ingawa zinalipa...
nadhani alichagua kundi la kukosa
 
husna alimwangusha kafulila ama alimuibia kafulila
Alimuangusha kwenye sanduku la kura na ndiyo maana Kafulila alishindwa kuishawshi Mahakama Kuu kanda ya Tabora itengue ushindi wa Mama Mwilima!

Asubiri 2020!
 
Back
Top Bottom