Jerry Muro: Tundu Lissu njoo uone

fe22e80adb3320d8f7e685176c9cc246.jpg



Ccc to gere milo mbona mwatuchanganya tushike lipi
 
Mbona inasemekana hilo jina siyo lake? Yasemekana huyo asili yake ni ile kanda yetu pendwa anakotoka Yohana mbatizaji.
Inawezekana mkuu ile kanda haiwez kuwa kilaza kama huyu.
Mwanamme mwenye tabia za kike kule hakunaga ukimkuta ujue huyu mlowez.
 
Huyu jamaa vipi? Yanga ilikushinda siasa ndiyo kabisaa, acha wanaojua siasa wafanye siasa, tafuta kazi nyingine. Usitake kuibukia kwenye migongo ya wengine, wewe na Lissu wapi na wapi kuruta wa danger coy.
Kuruta anafosi nae apande kidogo. .
 
Anaandika Jerry C. Muro

Taifa la Tanzania limeingia katika Historia ya Dunia Kufuatia Kampuni ya Barrick Gold kukubali kwa mara ya kwanza Kugawana asilimia hamsini kwa hamsini 50/50 ya Faida katika uzalishaji wa Dhahabu nje ya Asilimia 16 ya Mrahaba na Kodi ambayo taifa itapata.

Nimedadisi katika nchi mbalimbali ambazo Barrick wamefanya uwekezaji kama huu na kugundua Tanzania ndio nchi pekee ambayo imethubutu na kufanikiwa katika hili, Hongera Tanzania Hongera Rais Mzalendo Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli katika kurekebisha kwa vitendo makosa ya watangulizi wako, huu ndio Uongozi unaoacha alama tukufu, naamini kwa sasa watangulizi wako wanafuraha kubwa ya kuona umesahihisha kwa vitendo pale walipokosea.

Muafaka Baina ya Tanzania na Barrick umewaacha "bila nguo" tena nasisitiza "bila nguo kama mnyama" wale wote waliokuwa wakisubiri Tanzania ipelekwe mahakama ya kimataifa kutokana na kuchukua hatua za kuzuia makinikia, kwangu nasema shame on you najua wamenielewa na wamesikia, Leo Tanzania imepata Shilingi Bilioni 700 kama hela tu ya kujenga uaminifu, bado nasubiria tupate kodi yetu, tupate Mrabaha wetu, kisha tugawane faida hamsini kwa hamsini.

Nimefarijika sana na kauli ya Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwataka wawekezaji wengine wote katika Sekta ya Madini kujitafakari na kuanza kufuata uelekeo wa makubaliano kama Haya na Barrick, sasa tutaanza kuvuna neema kwenye Tanzanite, Almasi na kisha tutaingia kwenye Gesi na Mali asili zingine, Haya ni mafanikio makubwa katika kipindi cha takribani miaka miwili ya Uongozi wa Mhe Magufuli, naamini akimaliza miaka Mitano ya kwanza na ile mingine lazima Tanzania tutakuwa "Donor country"

Naomba nimalize kwa kufikisha salamu kule Nairobi, mwambieni kulikuwa na sababu ya Mungu kumuweka hai ili aje ashuhudie ukuu wa Mungu kupitia Mhe Magufuli, lile alilosema haliwezekani kwa sasa limewezekana na Hatimae Mhe Magufuli ameibuka shujaa na kinara wa kielelezo cha Rais Bora Africa anaepigania rasilimali za nchi yake, Mungu alisema Muombee sana "adui" yako aishi miaka mingi ili Ashuhudie Baraka za Mungu kwako, Hatimae maombi yetu yamejibu sasa.

Wasalamu
Jerry C. Muro
Dodoma, Tanzania
20/10/2017
Jamaa kaaibika sana, kaamua kunya stand usiku huku akijua hakuna umeme tuu ila watu wapo wengi.Sasa umeme umerudi ndio anajiona alivyo na nini maana ya watu kumwona ktk hicho kitendo.Huyu ndie anashidnana na Lissu. Sasa bariki wameamua kuondoa hio nia njema.
 
Tatizo nchi hii watu wengi ni waj..nga sana
Kwa kukadilia yaweza kuwa 98.6% ya Watanzania ni wajinga sana kuliko kawaida,,. Unapewa taarifa ya kuwa utalipwa Tsh.700,000,000,000 wakati ulikuwa unadai Tsh.425,000,000,000,000 kisha unashangilia kuwa umeshinda????,,

Ushauri,, Watu wafundishwe kutofautisha kati ya MILLION na BILLION, BILLION na TRILLION, na pia
Ujinga ni pale unapopata hitimisho la jumla ( general conclusion) kwa kutumia takwimu za mbele na kuziacha takwimu za nyuma, watu tuliaminishwa tunawadai ACCACIA TRILLION 425 leo wanasema KAMA itawezekana watatupa BILLION 700 halafu watanzania weeengi wanashangilia ,, mh!!????
 
We na siasa wapi na wapi ?au ndo njaa umejazwa pesa upambane na wapinzani ?Mimi nakujua vizuri sana tumesoma na kukua pamoja acha kujifanya unajua
 
Back
Top Bottom