MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 34
- 30
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa anastahili pongezi kwa kutafsiri kwa vitendo maelekezo ya Ibara ya 74 ilani ya uchaguzi ya CCM ya maaka 2020 - 2025 inayosimamiwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan iliyotaka serikali kuweka mikakati madhubuti ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na ustawi wa watu wote kwa kuzingatia sera, sheria, miongozo na taratibu za uendelezaji wake.
Kupitia uendeshaji wa Kliniki ya Ardhi mafanikio makubwa yamepatikana kwani imetoa fursa ya kuwasikiliza wananchi wenye migogoro ya ardhi, kutoa utatuzi wa mashauri ya migogoro ya ardhi yaliyodumu miaka mingi, kufanya utambuzi wa wamiliki halali wa kisheria wa viwanja vya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini, utoaji hati kwa wananchi wenye kumiliki ardhi papo kwa hapo pamoja na kuwadhibiti mabwenyenye waliokuwa vinara wa uporaji wa ardhi za wanyonge. Hongera sana Mhe Jerry Silaa kazi iendelee!