TBC1 Kurasa Darasa: Kitabu Cha Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
''Baada ya suluhu ile ya Captain Eltz na Alexander Le Roy iliyomaliza vita ile, Muro Mboyo aliondoka Machame kuelekea Old Moshi.

Nyuma akiwa ameacha mke na mtoto mdogo wa kiume aliyeitwa Kirama Muro, ambaye mama yake alikuwa anatokea Kibosho. Jina la mama yake Kirama Muro lilikuwa Makshani Olotu.

Huyu Bi. Makshani Olotu baada ya Uislamu kuingia Machame alisilimu na jina lake jipya likawa Sauda.

Baada ya mumewe kwenda uhamishoni Old Moshi, taarifa zilimfika Makshani kuwa mtoto Kirama na yeye wanatakiwa wauawe.

Lakini katika mila za Wachagga ilikuwa mtoto mwenye baba yake hauliwi.

Mama yake akaamua kwa ajili ya usalama wake na wa mwanaye kutoroka kukimbilia kwao Kibosho na mwanaye kwa wazazi wake kunusuru maisha ya mtoto wake.

Alipofika Kibosho Makshani akachukuliwa kama mateka na Mangi Sina kwa hiyo Kirama Muro akalelewa katika nyumba ya Sina kama vile yeye mwenyewe alivyolelewa kwenye nyumba ya Mangi Shangali.

Swali linalojitokeza ni kwa nini ilitoka amri mtoto wa Muro Mboyo auwawe?

Bila shaka mtoto wa Muro Mboyo alitakiwa kufa ili kukata ule mnyororo wa jadi ambao ungempa madaraka ya kuwa Jemadari wa Vita pale atakapokuwa mkubwa. Hofu ikiwa asije na yeye katika nafasi ile akawa, ‘muasi’, hataki kutii amri kama baba yake.

Kwa hakika mtoto wa Muro Mboyo, Kirama Muro kwa kuepuka kuuliwa akiwa mtoto mdogo aliishi na akaja kuibadili historia ya Uchaggani pale aliposimama kuuingiza Uislamu Machame nyuma ya Wamishionari ambao kwa kipindi cha muda miaka 100 walifanikiwa kueneza Injili Uchaggani kiasi ikawapelekea wao kumini kuwa Uislamu hautopanda mlimani na kufika Kilimanjaro.''


View: https://youtu.be/UY1MpKd2cOk?si=ddQi9MW4qR14KXDE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom