Jenerali Ulimwengu ashauri Makonda ashitakiwe kwa kuvamia kituo cha Clouds

Jenerali Ulimwengu ashauri Makonda ashitakiwe kwa kuvamia kituo cha Clouds

Huwa namkubali sana huyu mzee kwani siku zote si mtu wa kumumunya mumunya maneno.
 
Ashtakiwe wapi? miungu imeshika hatamu kesi itafunguliwa wapi ?
 
Generali Ulimwengu Yeye alipovuliwa Uraia mbona hakwenda Mahakamani?

Clouds wameshasema wamefunga Mjadala
 
Tupige kazi jamani anko wa chattle hataki kusikia kelele zetu
 
Akihijowa na DW mchana huu Jenerali Ulimwengu ameshauri Makonda ashitakiwe...

==============================================

Amesema ni tukio linaloweza kufanywa na viongozi ambao wanajiona hawana mipaka katika utawala wao.

Amesema mkuu wa mkoa amelewa madaraka na kwa kufanya tukio hilo ameonyesha kwamba hana kitu chochote kinachoweza kumzuia. Amewaomba wananchi kupata sauti zao katika kutetea haki zao.

Amesema suala la Makonda kuwajibishwa linategemea na mtu aliyemchagua ambaye ndiye kiongozi wa nchi kwa hiyo Raisi akiona kwamba kuna haja ya Makonda kuwajibishwa basi amuwajibishe ili iwe fundisho na kwa viongozi wengine.

Source; DW Swahili
Inatakiwa kutoa tafsiri sahihi ya "Uvamizi" hakuna uvamizi wowote uliofanyika, acheni kutumia maneno mazito kutafuta attention. Uvamizi unahusisha kutumia nguvu, hakuna nguvu zozote zilizotumika pale .... RC anahitaji ulinzi wakati huu kuliko wakati wowote, kuna kundi la mashaibiki wa sembe wanachafua hali ya hewa tu. Ni jambo la kutamka excemption tu kwa RC kwa yaliyotokea na kuomba msamaha kwa walioathirika kama wapo basi... Mnataka kusimamisha dunia kwa hili tu.
 
Huyo Ulimwengu mwenyewe tumemuhifadhi tu sio Raia asituletee mafujo ya kwao!
 
Mwanzaaa mukweba, JPMeeee mukweba, makondaaaa mukweba, gwajimaaaa mukweba, wangoshaaaa mukweba
 
RC makonda amefanya uvamizi mkubwa mno na mnyanganyi. amechukua clip kwa nguvu bila kuomba kwa flash yake. hii siyo unyanganyi na uvamizi? acheni ujinga nyie
 
Tuna katiba mbovu sana kumbe. Huyu akishinda, basi tutarajie kupata viongozi wa namna hii wengi kwasababu wanajua hakuna kinachozuia kuwa viongozi wa hovyo. Sijajua utitiri wote huu wa vyombo vya usalama una manufaa gani kwa mumlinda na kumtetea mtu ambaye katiba inayompa mamlaka ya kulindwa kwake haifuati na haitaki. CCM katika hili mnafanya dhambi kubwa sana ya kutowatendea haki watanzania. Sasa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ndiye anayevamia watu, ni nani atakayekuwa salama jiji hili?
 
Akihijowa na DW mchana huu Jenerali Ulimwengu ameshauri Makonda ashitakiwe...

==============================================

Amesema ni tukio linaloweza kufanywa na viongozi ambao wanajiona hawana mipaka katika utawala wao.

Amesema mkuu wa mkoa amelewa madaraka na kwa kufanya tukio hilo ameonyesha kwamba hana kitu chochote kinachoweza kumzuia. Amewaomba wananchi kupata sauti zao katika kutetea haki zao.

Amesema suala la Makonda kuwajibishwa linategemea na mtu aliyemchagua ambaye ndiye kiongozi wa nchi kwa hiyo Raisi akiona kwamba kuna haja ya Makonda kuwajibishwa basi amuwajibishe ili iwe fundisho na kwa viongozi wengine.

Source; DW Swahili

Huyo Drug baron Ulimwengu hata yeye siku zake zinahesabika!
 
Back
Top Bottom