Jenerali Ulimwengu ashauri Makonda ashitakiwe kwa kuvamia kituo cha Clouds

dafity

JF-Expert Member
Aug 16, 2008
1,858
2,059
Akihijowa na DW mchana huu Jenerali Ulimwengu ameshauri Makonda ashitakiwe...

==============================================

Amesema ni tukio linaloweza kufanywa na viongozi ambao wanajiona hawana mipaka katika utawala wao.

Amesema mkuu wa mkoa amelewa madaraka na kwa kufanya tukio hilo ameonyesha kwamba hana kitu chochote kinachoweza kumzuia. Amewaomba wananchi kupata sauti zao katika kutetea haki zao.

Amesema suala la Makonda kuwajibishwa linategemea na mtu aliyemchagua ambaye ndiye kiongozi wa nchi kwa hiyo Raisi akiona kwamba kuna haja ya Makonda kuwajibishwa basi amuwajibishe ili iwe fundisho na kwa viongozi wengine.



Source; DW Swahili

 
Ashtakiwe na nani wakati 'mungu' mwenyewe kamsifu na kumtia moyo kwa kazi hiyo.
Vyovyote vile, hiyo ndiyo option iliyobaki.

Kwa kuwa mteuzi wake ameshaamua kuwa hawezi kumfanya chochote hata kama akiiba mchana kweupe kwa kutumia silaha, lililobaki ni hilo tu.

Ila sina hakika kama hao waliokosewa (Clouds Media) wana nia hiyo maana sasa hivi wanambembeleza aende akaombe tena urafiki nao.
Muda si mrefu wataenda wao kuomba radhi kwa usumbufu waliomsababishia na kisha kuomba aendelee kuwa rafiki yao.
 
Hata mahakamani atalindwa tu maana mkulu keshajitoa muhanga haoni hasikii
 
Akihijowa na DW mchana huu Jenerali Ulimwengu ameshauri Makonda ashitakiwe...

Naona, kilichobakia huyo ulimwengu, afutiwe tu uraia maana naona kama bado hajaelewa mdundo wa mziki unavyoenda.

Ukicheza tofauti tu, basi kinachofuatia utakielewa ukiwa pekee yako.
 
Ha ha ha ha nacheka kwa dharaaaau, ya ngoswe tumuachie ngoswe, kama saiv yupo bedroom tusubir aingie bafuni kbs
 
Back
Top Bottom