Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,398
- 3,907
Akemea tabia wa Wakurugenzi kuvizia Wananchi wajichange kisha ndio kuwapelekea huduma za kijamii kama Vituo vya Afya na Shule.
Karibu wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amewataka Mwenyekiti wa Halmashauri kushirikiana na Mkurugenzi kuhakikisha Kituo cha Afya cha Mwembeni kinajengwa na kuanza kutoa huduma kwa Wananchi ndani ya Mwaka huu wa 2024.
Mwenezi Makonda ametoa maagizo hayo leo tarehe 20 Januari, 2024 akiwa katika muendelezo wa ziara yake Wilayani Pangani mkoani Tanga.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, Mwenezi Makonda amekemea tabia ya Viongozi hasa Wakurugenzi kuwavizia Wananchi hadi waanze kuchangishana fedha zao wenyewe kujenga zahanati au kituo cha Afya kisha wao ndio watoe fedha kukamilisha ujenzi huo.
"Hamuwezi kusema mnawachangia Wananchi wakati fedha za Serikali zinatokana na kodi ya Wananchi " Alisema Mwenezi Makonda.
Mwenezi Makonda amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi hakitasita kuchukua hatua kwa kiongozi yeyote aliyepewa dhamana ya kufanya kazi kutokamilisha wajibu wake.
#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee
PIA, SOMA:
Maagizo na matamko mengine ya Paul Makonda
- Mwenezi Makonda ampatia tsh milioni 2 kijana mjasiriamali mwenye kujiendeleza kibiashara
- Makonda: Siasa imemlipa Mbowe kajenga kasri
- Makonda ambananisha meneja TANROADS Geita: Ahoji ni lini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama - Kakoro (km 60) utasainiwa ili ujenzi kuanza
- Paul Makonda: Lissu mjanja ameona maandamano hayana maana
- Makonda: Mbinguni walimchukulia fomu Rais Samia. Adai Mbowe anajua kama Samia ametumwa na Mungu
- Makonda: Wafanyabiashara huichangia CCM kwa kuogopa wasiletewe TRA, TAKUKURU, uhamiaji ama Polisi
- Makonda: Stendi mpya Iringa ipewe jina la Chongolo