Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,113
- 24,642
Akiwa katika mahojiano na kituo cha radio cha DW leo 31.12.2016 Jenerali Ulimwengu ameeleza ni kwa jinsi gani utawala huu ulivyo wa milipuko, kwamba inatokea matamko yanatolewa asubuhi kisha jioni yanabadilishwa.
Amebainisha wazi pia wafanyakazi wengi wa umma wanafanya kazi kwa uoga bila kujiamini ili wawafurahishe watawala kwa kuogopa kutumbuliwa.
Ameeleza pia jinsi ambavyo JPM alivyokiri hapo awali kuwa ameshindwa kwani alitamani muhula wa uongozi upunguzwe lakini baadaye akabatilisha na kusema ataaendelea.
Hii ni dalili tosha kwamba kwa yanayotokea kwa sasa hayataleta ufanisi mkubwa kama ilivyokuwa ikitarajiwa na wengi na kwamba itachukua muda sana kuweza kupata mustakabali wa hali iliyopo kwa sasa!