Jela miaka mitatu, kisa kanikataa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jela miaka mitatu, kisa kanikataa!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 30, 2011.

1. Mtambuzi

Mtambuzi Platinum Member

#1
Aug 30, 2011
Joined: Oct 29, 2008
Messages: 8,795
Likes Received: 1,247
Trophy Points: 280
Kwa kifupi sana ni hivi. Mwaka 1975 nikiwa mwalimu kijana bado, nilifanya jambo ambalo kwa wakati ule wala halikunisumbua ingawa lilikuwa baya sana. Bila shaka, wale wanaokumbuka mfumo wa elimu wa wakati ule wanajua kuhusu wanafunzi waliokuwa wanaitwa maripita ambao walikuwa ni wale wanaoanguka mtihani wa darasa la saba shule fulani na kwenda kudurusu darasa hilo kwenye shule nyingine.

Serikali ilikuwa inakataa kabisa wanafunzi kukariri tena darasa la saba au la nyuma yake baada ya kuanguka mtihani. Nikiwa shuleni kule Mbeya mwanafunzi mmoja ambaye baba yake alikuwa na urafiki na mkuu wa shule niliyokuwa nafundisha alikuja kudurusu darasa. Siku alipokuwa anakuja kuripoti, nilikuwepo mimi ofisini kama mwalimu mkuu msaidizi. Kijana huyo aliletwa na dada yake ambaye alikuwa anafanya kazi hospitali ya mkoa. Nilimpokea kijana yule nikijua kwamba anarudia shule.

Baadaya kumpokea na kujua dada yake anapofanyia kazi, niliona nami ningepata. Kama mkuu wa shule alipata fedha kupitia Yule kijana kudurusu darasa, nilijua na mimi ningepata rushwa ya mwili. Nilimwandikisha kijana huku nikisema kwamba, kudurusu darasa ni mbaya
sana. Yule dada wa kijana alisema ni kweli, lakini ni suala la kusaidiana.

Nilitania kwakusema, “nasi tukija kuomba msaada hospitalini itabidi tusaidiwe.” Yule dada alisema hakuna tabu. Basi kijana alianza masomo darasa la saba nami nilianza kumfuatilia dada yake kule hospitali ya mkoa. Nilifuatilia kwa miezi miwili bila mafanikio zaidi ya ahadi tu.

Nilijua kwamba, Yule muuguzi, dada wa yule kijana alikuwa anataka tu kuvuta muda ili mdogo wake amalize masomo ili anitolee nje. Ilibidi nimwambie kwamba, kama asiponikubalia ombi langu, mdogo wake ni lazima angeanguka mtihani kwani ningekwenda kuchongea mkoani kuhusu kudurusu kwake.

Yule dada aliniambia, kama hilo ndilo lengo langu, ni vizuri nikalifanya. Kuanzia hapo sikufuatilia tena na nilipania kumchongea Yule mdogo wake, jambo ambalo sikujua kwamba, lingemdhuru na bosi wangu, yaani mwalimu mkuu. Ni kweli nilikwenda mkoani na kutoa taarifa kisiri kwa wanaohusika.

Ukweli ni kwamba kijana Yule ambaye alikuwa na uwezo sana darasani alishindwa baada ya jina lake kukatwa na mkuu wa shule kushushwa cheo. Nilifurahi sana baada ya matokeo hayo. Nilikwenda kule Hospitalini kumjulisha Yule dada mtu kwamba mimi ndiye niliyemwangusha mdogo wake.

Yule dada alilia nikiwa hapohapo, huku moyo wangu ukiwa umeridhika. Jioni ya siku ile ile, Yule kijana alikuja nyumbani kwangu hapo shuleni na kuniuliza ni kwa nini nimemfanyia roho mbaya . Nilimwambia amuulize dada yake na kumsisitiza kwamba sio mimi bali ni sheria za
nchi.Yule kijana aliondoka huku akisema, Mungu ndiye anayejua kulipa au kutoa hukumu kwa haki . Nilicheka na kumwambia aende akafie mbali. “Dada yako ni ndege mjanja amenasa kwenye tundu bovu” Nilimpigia kelele. Aligeuka na kunitazama kwa muda, halafu aliondoka. Nadhani angekuwa na nguvu angeweza kunipiga ngumi nyingi sana, lakini hakuwa
na ubavu.

Miaka ilipita na nikawa nimesahau kabisa jambo lile. Ilikuwa ni miaka 25 baadae, mwaka 2000 ni kwamba mwaka 1995 niliacha kazi ya ualimu na kurudi kwetu Iringa. Nilianzisha biashara na kuwa mfanyabiashara. Mwaka huo 2000 nilipata matatizo ambayo yalinifikisha mahakamani.

Kesi iliendelea kwa mwezi mmoja, kabla ya kutolewa hukumu. Haikuwa kesi kubwa, wala ambayo ingenitisha kwa kweli, Haya hukumu yake kwa mujibu wa wanasheria ambao niliwauliza, hakimu alikuwa anaruhusiwa kutoa faini au kifungo cha nje. Sijui walinidanganya kunipa moyo au vipi.

Lakini siku ya hukumu hakimu alinihukumu kwenda jela miaka Mitatu adhabu ya juu kabisa ya kosa langu. Nilibabaika sana na wala sikuamini kama nimehukumiwa kwenda jela. Wakati nikipelekwa kufungiwa selo Yule hakimu aliyenihukumu alinijia na kuniambia.

“Siyo mimi, bali sheria za nchi. Nadhani safari hii dada yangu sio ndege mjanja tena.” Ilinichukua muda, lakini polepole akili ilizibuka wakati nikiwa jela mwezi wa pili, ambapo nilikumbuka lile tukio la mwaka 1975. Sijui nilihisi nini, lakini niliumia sana. Sipendi kukumbuka nilivyoishi kwa huzuni kule jela, nikijutia ufedhuli ule nilioufanya kwa kijana yule wakati ule.

Baada ya kumaliza kifungo changu, bado nikiwa na harufu ya jela nilikwenda nyumbani kwa hakimu yule na kubisha hodi. Alifungua mlango na kunikaribisha ndani kwake bila kinyongo. Nilimsalimia na kumwambia moja kwa moja . “Naomba radhi kwa yale niliyokufanyia wakati ule….”

Yule hakimu alinikata kalma na kusema, “hukufanya lolote baya, ilikuwa ni sheria kweli. Kama ambavyo nami nimetimiza sheria za nchi. Wala huna haja ya kuomba radhi, labda tu kwa sababu, wewe ulikuwa unalipa kisasi baada ya dada yangu kukukataa, wakati mimi sikutimiza wajibu wangu kwa kinyongo.”

Niliinuka na kutoka nje, nikielekea kwangu. Maisha yalikuwa ndiyo kwanza yanaanza na uzee umeingia . Kisa kujisahau.

2. Nemo

Nemo JF-Expert Member

#2
Aug 30, 2011
Joined: Feb 22, 2011
Messages: 661
Likes Received: 471
Trophy Points: 80
Du pole mkuu....................ama kweli hichi kisa chako kina dhihirisha ile methali ya "Aliye juu mngoje..............................."

3. Vin Diesel

Vin Diesel JF Gold Member

#3
Aug 30, 2011
Joined: Mar 1, 2011
Messages: 8,402
Likes Received: 737
Trophy Points: 280
Aliesema malipo ni hapa hapa duniani hakukosea...

4. Mtalingolo

Mtalingolo JF-Expert Member

#4
Aug 30, 2011
Joined: Aug 4, 2011
Messages: 2,188
Likes Received: 16
Trophy Points: 135
Duuh ni hadithi au story ya kweli? Pole sana kweli mla ndizi husahau, lakini mla maganda kamwe haji kusahau..

5. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#5
Aug 30, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,508
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
afadhali umetukumbusha. yaani huwa tunajisahau na kujiona miungu watu. usidharau mkubwa wala mdogo,at least do domething to help the other person. hongera kwa kulipa na kutambua gharama ya ulichokifanya

6. Mtambuzi

Mtambuzi Platinum Member

#6
Aug 30, 2011
Joined: Oct 29, 2008
Messages: 8,795
Likes Received: 1,247
Trophy Points: 280
Duh, hakinihusu mimi bana.....lakini ni kisa cha kweli kilimpata rafiki yangu, mie ni msimuliaji tu....

7. Kaunga

Kaunga JF-Expert Member

#7
Aug 30, 2011
Joined: Nov 28, 2010
Messages: 12,590
Likes Received: 797
Trophy Points: 280

Nami nilihisi hivyo; ungekuwa weye ungesimulia as if imempata jamaa fulani!

8. Shantel

Shantel JF-Expert Member

#8
Aug 31, 2011
Joined: Feb 7, 2011
Messages: 2,021
Likes Received: 24
Trophy Points: 0
kuna mwalimu mmoja pia wa chuo kimoja kipo town huko alim disco mwanafunzi sababu tu alimkataa
badae akaenda kusoma nje ya nchi, aliporudi alimkuta yule mwnafunzi yuko tra, mwanafunzi alihakikisha mwalimu anashindwa
kutoa mizigo yake yote

9. Yericko Nyerere

Yericko Nyerere Verified User

#9
Aug 31, 2011
Joined: Dec 22, 2010
Messages: 16,222
Likes Received: 3,782
Trophy Points: 280
Pole mkuu hili nifundisho kuu kwa wazayuni wa tz!

10. Rutashubanyuma

Rutashubanyuma JF-Expert Member

#10
Aug 31, 2011
Joined: Sep 24, 2010
Messages: 158,014
Likes Received: 416,608
Trophy Points: 280
mwosha huoshwa tu...........................hakuna ujanja hapo...................

11. henrygees

henrygees Senior Member

#11
Aug 31, 2011
Joined: Sep 8, 2010
Messages: 138
Likes Received: 21
Trophy Points: 35
be good to people when you are going up coz you may might them when you are going down

lucky dube

12. pascaldaudi

pascaldaudi JF-Expert Member

#12
Aug 31, 2011
Joined: Mar 25, 2009
Messages: 534
Likes Received: 3
Trophy Points: 0
E bwana mbavu sina!!!

13. Bujibuji

Bujibuji JF-Expert Member

#13
Aug 31, 2011
Joined: Feb 4, 2009
Messages: 35,303
Likes Received: 22,104
Trophy Points: 280
Fundisho kubwa sana

14. Mr Rocky

Mr Rocky JF-Expert Member

#14
Aug 31, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 15,186
Likes Received: 567
Trophy Points: 280
Duh kweli malipo ni hapa hapa duniani

15. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#15
Sep 1, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0

Ni kweli , pia ni vizuri kumwombea maisha marefu yule aliyekufanyia ubaya ili siku moja aje ajifunze kitu kutokana na ubaya wake. WATU WENGI {SIYO WOTE} WANAONA UFAHARI KUWANYANYASA WENZAO KWA KUTUMIA MADARAKA / UWEZO WALIONAO PASIPO KUGUSWA NA MATESO / MAUMIVU YA WAFANYIWAO UBAYA HUO.

16. TUNTEMEKE

TUNTEMEKE JF-Expert Member

#16
Sep 1, 2011
Joined: Jun 15, 2009
Messages: 4,582
Likes Received: 55
Trophy Points: 145
thanx ni fundisho ili

17. Elia

Elia JF-Expert Member

#17
Sep 1, 2011
Joined: Dec 30, 2009
Messages: 3,442
Likes Received: 3
Trophy Points: 135
Malipo duniani na inawezekana ndio kwanza ameanza kulipa bado haja maliza..... Asante kutukumbusha CHEO NI DHAMANA

18. M

Mwanaweja JF-Expert Member

#18
Sep 1, 2011
Joined: Feb 8, 2011
Messages: 3,576
Likes Received: 10
Trophy Points: 135
hili somo mkuu mwenye akili timamu atapatafundisho lakini akina wale ndio hivyo tena shukrani mkuu

19. Kimbweka

Kimbweka JF-Expert Member

#19
Sep 1, 2011
Joined: Jul 16, 2009
Messages: 8,608
Likes Received: 49
Trophy Points: 145
Huu utunzi wa hadithi utakufikisha mbali sana, hongera kwa utunzi

20. St. Paka Mweusi

St. Paka Mweusi JF-Expert Member

#20
Sep 1, 2011
Joined: Sep 3, 2010
Messages: 5,899
Likes Received: 96
Trophy Points: 145
MH...!!! What a coincidence.......

Loading...