Mshaurini Ajira Portal kuna nafasi za kazi yake ajaribu huko.JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.
Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.
Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.
Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.
Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.
Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.
Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.
Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.
Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com
Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.
Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.
View attachment 1125671
View attachment 1125673
View attachment 1125675
Maisha sio lazima kuajiriwaMshaurini Ajira Portal kuna nafasi za kazi yake ajaribu huko.
Pengine ana tatizoUnarudi nyumbani kuja kuangaliana na wadogo zako? Jamaa huyu mjinga!
Ndio shida ya samaki kusomea kuruka miti na ngedere kusomea kuogelea. Huyo alipaswa kusomea kilimo cha kisasa.
Jamaa ana tatizo la akili. Alikuwa na kazi nzuri, badala awachukue watoto zake, yeye anaona ni afadhali aache kazi, awafuate wadogo zake kijijini!
Sasa ufumbuzi gani ndugu si umeona amejishikiza kubeba mizigo?it is a puzzle indeed. But, hii sio mara ya kwanza kusikia hizi habari za wahitimu kukosa ajira,tuhangaike kutafuta ufumbuzi na sio kuignore magnitude ya hili tatizo..
Vyote unavyosema kafanyaElimu yetu ina mushikeli sana. Iko kwenye kupata ufaulu mkubwa kuliko kuelimika. Hivi telecom engineer atakosaje kitu cha kufanya? Hata kufundisha hesabu na physics basi. Yaani game limekataa kabisa mpaka kurudi nyuma mazima?
Chadema hao wanaokoteza vichaa vijijini waonekane wako na wanyongeSIJAJUA LENGO LA HUU UZI. NIMESOMA MARA MBILI MBILI LAKINI BADO SIJAJUA MAANA YA HUU KUWEPO HUU UZI HUMU. DIWANI KAENDA KUMUONA. KAENDA KUMUONA ILI IWEJE? HII HABARI UMEKUTA WAPI?
HUYO DIWANI HANA AKILI. HUU NI ZAIDI YA UDHALILISHAJI MAANA KAMA MTU HUTAKI KUMSAIDIA NI BORA UKAMUACHA NA MAISHA YAKE NA SIYO KUMUWEKA KWENYE MEDIA ILI WAPATE SIFA.
HUU UZI NIMEUSOMA ILA SIJAFURAHISHWA NAO KABISA. DADA YANGU UMEFANYA JAMBO JEMA LAKINI UMEFANYA UDHALILISHAJI PAMOJA NA HUYO DIWANI. MTU ANAHANGAIKA NA MAISHA YAKE AMEKONDEANA. WEWE UNARUSHA HUMU SIJUI UPATE LIKE AU NDIYO UJULIKANE ZAIDI?
KIUFUPI
WEWE, DIWANI NA HAO WALIOCHAPISHA HIYO HABARI WAMEFANYA TUKIO LA UDHALILISHAJI. KAMA MTU HUWEZI KUMSAIDIA ACHANA NAYE NA SIYO KWENDA KAMERA UPATE SIFA.
Sidhani kuwa issue ni kukosa ajirait is a puzzle indeed. But, hii sio mara ya kwanza kusikia hizi habari za wahitimu kukosa ajira,tuhangaike kutafuta ufumbuzi na sio kuignore magnitude ya hili tatizo..
Pole haitoshiMkuu najua sana hizo shida, zinaumiza, zinakatisha tamaa,...unadharaulika, unakejeliwa, unatukwana, unadhihakiwa, unanyanyaswa kwa maneno. Sitaki kukumbuka. Nampa pole. Dunia ni duara.
Ndo maana nkakwambia njoo na ujinga wakoMwanaume wa kweli anapambana mwambie afungue ata kiwanda cha kuchakata nyama kuwa mishikaki kijiweni kwake
Salute mkuu!!!Pamoja sana mkuu.
Hata Dua zetu zitamrahishia mipango yake kunyooka mapema, tuanze kwa kuweka maombi ili hata ukimhabarisha mtu asiwe na uzito wa kusaidia anapopaweza
Afu we mtoto naona unatafuta viboko vya wazee wanankooooMkuu nimefika hapa.
Ngoja nisome sasa .